Kwa waliopigania Uhuru ndio wanajua umuhimu wa siku hii kidhati, na baadhi ya wanasiasa wenye maono ya umoja dhidi ya taifa, ila itafikia hatua mungu akiwachukua hawa watu basi watakao kuja hawata thamini tena hii siku.
Sherehe ya uhuru mtu anaweza akaiona sio muhimu kwa mtazamo finyu na wajuu, ila sherehe hii ndio pekee raia wote wa tanzania na wenye asili ya tanzania, ambao wapo ndani ya nchi na nje ya nchi, hujumuika kwa pamoja kusherehekea either kwa kwenda kwenye viwanja zinapofanyika hizi sherehe au kwa kutazama luninga. Umoja huu sio wa kuchukulia wepesi.
Uzito wa sherehe hizi mtu hata ukitazama kwenye luninga tu jinsi watu/jeshi la polisi/jeshi la wananchi wanavyofanya maonesho yao (ufundi), MWILI HUA UNASISIMKA SANA. Na inashangaza mtu kuchukulia siku hii sio muhimu na kwa wepesi sana.
Itabakia kwenye kalenda na historia tusipo angalia.
Mtazamo wangu,