Napenda kutoa wazo kwamba, kwakuwa tumeishi kwa udugu, umoja na amani, kwa miaka hii 50 na kwakuwa tumekuwa na muungano wa kipekee duniani, wenye mafanikio makubwa sana na kwakuwa sherehe hizi muhimu zimeangukia Jumamosi, na kwakuwa watanzania kuanzia Pemba mpaka Mtwara, Moshi, Bukoba na sehemu za nyanda za juu watakuwa wamechoka, basi Raisi kwa mamlaka aliyopewa atangaze Jumatatu tarehe 28 kuwa ni siku ya mapumziko ya kitaifa.