Sherehe za kuzima mwenge Tanga - Live

Mpita Njia

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
6,997
1,163
Nipo na glasi yangu ya shurbati nikiangalia TBC1 wakileta live mambo ya kuzima mwenge kutoka mkwakwani Tanga. Kwa kuwa ninaweza kuwashushia, haya ndiyo yanayojiri hivi sasa.

Mapema, kulikuwa na misa ya kumbukumbu ya mwalimu Nyerere ambayo rais alitakiwa kuhudhuria lakini alishindwa kufanya hivyo na kumtuma kapuya kumwakilisha.

Baadaye alipoamka, alikwenda kukagua maonyesho katika mabanda ya vijana.

Hivi punde ameingia Mkwakwani na vijana wametumbuiza halaiki bomba. Walipoimba ule wimbo maarufu-NI WAJIBU TUMSUHUKURU BABA NYERERE, JK alishindwa kuvumilia akaamka kitini na kuanza kucheza sambamba ya midundo ya wimbo.

Hivi sasa kuna burudani za nyimbo za kienyeji, akina mama wa Tanga wanakatika kinoma-naona mmoja anakata viuno na chungu kinachowaka moto kikiwa kichwani Mh! mambo ya tanga hayo!
 
Mambo makubwa, wachina nao wamo. Hivi sasa wachina wanaonyesha utaalamu wa kuoigana kung-fu
 
Baada ya wachina kumaliza vitu vyao, sasa tunaendelea kuburudika na ngoma za tanga
 
Sijui hawa Vodacom wamefadhili vikundi vyote vya ngoma! maana kile cha kwanza walikuja wamevalia fulana za Voda, na kikundi hiki nacho kimevalia fulana za Voda vilevile!
 
Mh! jamani, hawa wadada wa Tanga, we acha tu! Naona wanakatika huku Abdulazizi akiteta na mama salma, sijui anamfafanulia kitu gani!
 
Sasa umefika wakti wa hotuba. Z'Bar inawakilishwa na waziriw a ajira-Asha Abdallah Juma-anasema kazi inayofanywa na JK kuongoza nchi kwa umahiri ni zawadi tosha kwa wazanzibari
 
Waliowahi kuwa wakuu wa mikoa wa Tanga nao wapo, akiwamo Mzee Kingunge
 
TICTS nao wamo, mzungu wao alipewa nafasi ya kuzungumza, ameintroduce hotuba kwa kiinglish amemwachia mswahili mmoja, nadhani Ngamilo huyu, anatoa salamu za TICTS
 
Nipo na glasi yangu ya shurbati nikiangalia TBC1 wakileta live mambo ya kuzima mwenge kutoka mkwakwani Tanga. Kwa kuwa ninaweza kuwashushia, haya ndiyo yanayojiri hivi sasa.
Mapema, kulikuwa na misa ya kumbukumbu ya mwalimu Nyerere ambayo rais alitakiwa kuhudhuria lakini alishindwa kufanya hivyo na kumtuma kapuya kumwakilisha.
Baadaye alipoamka, alikwenda kukagua maonyesho katika mabanda ya vijana.
Hivi punde ameingia Mkwakwani na vijana wametumbuiza halaiki bomba. Walipoimba ule wimbo maarufu-NI WAJIBU TUMSUHUKURU BABA NYERERE, JK alishindwa kuvumilia akaamka kitini na kuanza kucheza sambamba ya midundo ya wimbo.
Hivi sasa kuna burudani za nyimbo za kienyeji, akina mama wa Tanga wanakatika kinoma-naona mmoja anakata viuno na chungu kinachowaka moto kikiwa kichwani Mh! mambo ya tanga hayo!

Kumbe pamoja na uwezo mkubwa wa kupiga story, anaweza mambo mengine kadhaa?!

.
 
TICTS wanasema wamechangia sh mil 36 kwa miradi mbalimbali ya mwenge mwaka huu. Pia imetoa sh mil 1 kwa kila mkoa nchini wka ajili ya shughuli za maendeleo.
sasa ni zamu ya kapuya
 
Ameshaanza porojo zake, eti anasema wanyamwezi ni watu wa Tanga na ndio maana yeye, Mwapachu, Kigoda, wamefanana!
 
miradi (halisi) ya zaidi ya sh bil 90 imezinduliwa nchini kote wakati wa mbio za mwenge
 
Kwa taarifa tu, mbio za mwenge mwaka huu ziloizinduliwa Mei 29 na Pinda kijijini Msoga, bagamoyo-alikozaliwa JK
 
Mwakani uzinduzi wa mbio za mwenge utafanyika Mwanza na kuzimwa Mara. Sasa wakuu wanashuka jukwaani kuona mwenge ukiingizwa uwanjani
 
Sisi tunataka kuuwasha mwenge, na kuuweka juu ya mlima kilimanjaro, utuletee matumaini... wananikumbusha mbali hawa!!!!
 
Wakimbiza mwenge-Selemani Jecha, mkoa wa Magharibi Unguja, Mohamed Magati-Pwani, mkuu anaongea naye sana anapomkabidhi cheti---aaaaah huyu mtangazaji wa TBC anasemasema kiasi siwezi kusikia majina ya wakimbiza mwenge wengine
 
Bakia Abdallah Hamis-kaskazini pemba-ni binti huyu, Shanes Martin Nungu-kiongozi wa mbio za mwenge - anatoka ERuvuma. sasa anasoma risala
 
Back
Top Bottom