Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,682
- 149,885
Ukiwa hapa Dodoma hivi sasa ndio utajua hizi sherehe za kitaifa zinatumia gharama kubwa sana na kwa nchi hizi masikini kwakeli huoni tija ya uwepo wa sherehe hizi kila mwaka.
Maandalizi ya sherehe hizi za kiserikali yanagusa mambo mengi kuanzia maandalizi ya uwanja wenyewe, maandalizi ya gwaride, gharama za wageni,mafuta ya magari, ulinzi, mazoezi ya ndege za kijeshi, malipo ya washiriki, gharama za ndege kwa ajili ya kusafirisha viongozi wa kitaifa,n.k.
Nafikiri wakati umefika tupeleke sheria Bungeni sherehe hizi za kiserikali ziwe zinafanyika kila baada ya miaka 2 na si kila mwaka au kutegemeana na maamuzi ya mtu mmoja.
Hivi kuna logic gani ya kurusha ndege za kivita huku walipa kodi wanakabiliwa na upungufu wa madawa?
Kuna logic gani ya kukodishia viongozi wa kitaifa ndege huku baadhi ya viwanja vya ndege vikiwa vinahitaji kukarabatiwa, kupanuliwa,n.k?
Kuna logi gani ya kutumia mamilioni /mabilioni haya kila mwaka huku deni la Taifa linakuwa kila mwaka?
Jamani si lazima kuiga kila kitu bali mambo mengine tuache yafanywe na nchi ziliozoendelea na sio sisi nchi ombaomba huku hata Bajeti tunazopanga tunashindwa kuzitekeleza.
Vile vile siungi kabisa mkono maamuzi ya mtu mmoja kuamua sherehe hizi za kiserikali ziwepo au zisiwepo maana huu si utaratibu na huwezi kubana matumizi kwa style ukategemea kuleta tija kwa nchi hata kidogo.
Sherehe hizi kitaifa ziwe ni kila baada ya miaka miwili na hiyo miaka mingine ziwe zinaadhimishwa kwa style tofauti.
Kwa mfano,sherehe za uhuru kwa miaka mingine ziwe zinafanyika bila siku husika kuwa ni public holiday na baadala yake iwe ni siku ya kazi kama kawaida ili tujenge nchi ikiwa ndio malengo hasa ya kutaka kujitawala.
Kama sherehe za uhuru za mwaka 2015 ziliadhimishwa kwa watu kufanya usafi,kuna ubaya gani sherehe hizo kwa baadhi ya miaka zikawa zinafanyika kwa watu kuendelea kuingia makazini?
We need to change first before wa can change our own country.