Ghazwat
JF-Expert Member
- Oct 4, 2015
- 23,718
- 66,276
View attachment 380454Safari ya kusherehekea basi mpya la shule ya upili ya wasichana ya Nyamagwa, iligeuka mauti baada ya basi hilo kuhusika katika ajali na kuwaua wanafunzi watatu katika eneo la Nyambunde, Bobasi, Kaunti ya Kisii.
Ajali hiyo iliyotokea mwendo wa saa nne asubuhi katika barabara ya Itumbe - Igare iliwahusisha wanafunzi wa kidato cha tatu.
Kulingana na walioshuhudia ajali hiyo, basi hilo lilikuwa likiendeshwa kwa mwendo wa kasi, ambapo dereva alipoteza mwelekeo na basi hilo kubingiria.
Bw Duke Nyabuto, dereva wa bodaboda alieleza kuwa basi hilo lilianguka katika mtaro uliopo kando ya barabara wakati dereva alipojaribu kuhepa kugonga matatu.
"Ilinilazimu nikimbie ili kuwasaidia waathiriwa ambao walikuwa wameumia sana na kuwapeleka katika hospital ya rufaa ya Kisii ". alisema.
Bw Charles Ocharo ambaye pia alishuhudia ajali hiyo alisema basi hilo lilikuwa limewabeba wanafunzi wengi kupita kiasi.
" Wanafunzi hao walikuwa wakipiga mayowe ya furaha huku gari likienda kwa mwendo wa kasi sana nimeshtuka kusikia kuwa wamehusika katika ajali "alisema Bw Ocharo
Wasamaria wema waliwakimbiza hospital waliohusika katika ajali hiyo wakitumia magari ya kibinafsi, malori na pikipiki.
Polisi walikuwa na wakati mgumu kuudhibiti umati ambao ulikusanyika katika lango kuu la hospital hiyo ya rufaa ya Kisii.
Kulingana na waziri wa afya wa kaunti ya hiyo Bw Geoffrey Otomu, hospital hiyo iliwapokea wanafunzi 69 huku 5 wakiwa katika hali mahututi.