Zekidon
JF-Expert Member
- May 29, 2013
- 1,903
- 569
Kwa kweli huyu shemeji yenu simuelewi kabisa nini maana ya haya mambo anayoyafanya kwangu.
Nashindwa nimweke katika kundi gani, au ni adui anayenimaliza kimya kimya.
Nakumbuka wakati flani tukifanya kazi pamoja kabla ya yeye kuhama, alikua akisikia nimefanikiwa jambo flani kazini alinuna sana.
Kuna kauli moja ambayo naikumbuka mpaka leo, aliwahi kuniuliza " kwanini wewe hapa kazini proposals zako zote huwa zinakubaliwa" Nilinote tu na kukaa kimya.
Mwaka jana, mwisho ni mwa mwaka, tulikwenda kusalimia huko kwao, na katika kukaa huko, nikaona shamba nikanunua, sasa hivi majuzi nimekwenda kuangalia shamba, nimekuta anafanya ujenzi huko kwao. Yaani bila kuniambia anajenga kwao. Na wazazi wake wamahamia juzi tu.
Kumbe muda wote huo tunajibana, yeye anapeleka fedha kwao kujenga. Hili limenisikitisha sana, najiona kama nimetumika kwakweli.
Lakini ajabu nikifanya mambo yangu ya maendeleo, ananuna sana tu, nashangaa yeye akifanya yake hanishirikishi lakini mimi namshirikisha yangu naishiwa kuonewa kijicho.
Ukimwambia nafanya jambo flani la maendeleo, atanuna mno, nimekuja kugundua kumbe angependa lifanyike kwao na sio kwangu.
Hii tabia imenikera. Msaada nimfanyaje huyu shemeji yenu.