'Shemeji kaniuzia kesi' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

'Shemeji kaniuzia kesi'

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by SnowBall, Aug 21, 2012.

 1. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #1
  Aug 21, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Baada ya mihangaiko na shughuli nyingi za Jiji letu hili niliamua kujipumzisha sehemu moja ili nivute muda kabla ya kurejea nyumbani. Actually ni sehemu ambayo upande mmoja kuna TV kubwa na kwa sababu kulikuwa na mpira sikutaka kukaa sehemu ambayo kuna kelele nyingi kwa sababu mie sio mpenzi sana wa mpira.Hivyo nillingia ndani zaidi kwenye utulivu!

  Nilitafuta meza ambayo jirani yake kulikuwa na watu kama wa3 hivi na kwa sababu kulikuwa na kigizagiza sikuwatambua wahusika kwa haraka. Mhudumu alikuja na nikamuagiza ninachohitaji na wakati huo nilikuwa nabrowse hapa JF na kwa mbali niliona charge ya simu yangu ilikuwa karibu kwisha. So niliweka simu pembeni na kuanza kunywa kinywaji changu. Wakati napepesa macho vizuri kumbe wale waliokaa jirani kulikuwa na shemeji yangu (mke wa Rafiki yangu) tunayeheshimiana sana. Aliniona na alikuja kunisalimia na kisha kunieleza kuwa alikuja na rafikie ambaye pia alikuja na mpenzi wake (kulikuwa na mkaka kati yao)..hivyo walikuja kupata kinywaji kidogo na yeye alikuwa kamsindikiza shogaake.

  Sikujali sana na nilienda kuwasalimia kwa pamoja. Sikukaa sana na nikaondoka nyumbani. Kwa kuwa simu yangu ilikuwa imeisha charge nilicharge na nikalala. Asubuhi wakati nafungua simu yangu nimekutana na message hii 'Samahani sana shemeji yangu naomba katu usimwambie rafiki yako kama tumekutana leo hapa..'. Ilikuwa ni message ya shemeji na inaonekana aliituma jana hiyohyo sikuisoma kwa sababu simu yangu ilikuwa imeisha charge.

  Nimebaki najiuliza mchezo anaotaka kuniletea shemeji yangu!!..hasa nikizingatia kuwa alinitambulisha kuwa alimsindikiza rafikie kwa mtuwake...sasa iweje anipige mkwara??..Nimempigia simu rafiki yangu na ameniambia hayupo mjini kwa takribani siku tatu sasa na sijamueleza chochote..Hapa nilipo sijaijibu meseji na sijampigia simu shemeji kumuuliza chochote!!..Nimepanga nimyamaze kama meseji inavyosema but naona kama sitamtendea haki rafiki yangu..Lakini pia naogopa kama nita'expose' hii habari kwa rafiki yangu na kukawa na tatizo..nahisi nitakuwa..' more guilty'..Lakini kama alikuwepo m2 mwingine (kumbuka kulikuwa na watu wanangalia mpira) akaona na akasema kwa rafiki angu naona bado shemeji atajua mimi ndiye niliyemwambia mumewe..So,hapa nilipo i am really confused naona kama 'shemeji kaniuzia kesi bila kujijua'..

  Hebu wadau nisaidieni ili niiweze kuihandle hii issue b4 haijawa tatizo kwangu!!!
   
 2. Mr Rocky

  Mr Rocky JF-Expert Member

  #2
  Aug 21, 2012
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 15,186
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Mkuu SnowBall bar ni sehem wazi ambapo kuna watu wengi kwa wakati mmoja
  Kuonekana kama ataonekana kupo sana na wakati wowote hilo linaweza kufanyika
  Kama alivyokuomba we kaa kimya na mhakikishie kuwa hutofungua mdomo wako kumwambia yoyote ila mtahadharishe kuwa iwapo habari zake zitavuma kokote au jamaa yake ataambiwa aelewe kuwa hizo habari hazijaanzia kwako
  Na hata wewe ukija kuulizwa ili wewe usiwe chanzo cha yeye kukosana
  Na kwa nini anaogopa taarifa zake kuvuma
  Je kulikuwa na fishy business inaendelea pale move ambayo hata wewe hukuiona
  Maana kama alimsindikiza shogake anachoogopa ni nini kujulikana kuwa alienda sehem kama ile
  Maana sidhani kama jamaa amemkataza kwenda sehem za starehe kiasi kwamba aogope kuonekana
  Kama hakuna ubaya wowote ulioendelea sidhani kama una haja ya kuwa na wasi wasi
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 3. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #3
  Aug 21, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  silent is the answer.
  in case wakalipuana huko shauri zao
  hiyo msg usiifute unaweza geuziwa kibao wewe ndio ulikuwa nae itakusaidia kama evidence
   
 4. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #4
  Aug 21, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Mr Rocky kwa kweli sikuona chochote na kiukweli baada ya kuwasalimia niliconcentrate kusoma magazeti yangu niliyokuwa nayo mzee..Nimeshangaa kupigwa biti asubuhi yake...
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 5. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #5
  Aug 21, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Lokissa well said man
  You mean i should keep silent?
  Message sijaifuta kwa kweli!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 6. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #6
  Aug 21, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  unajua rshps ziko za aina nyingi..kuna zingine unakuta jamaa hataki kabisa kusikia mwanamke wake yuko bar hata kama yuko na rafikie..kwa hiyo unaweza ukute jamaa kadanganywa kua bibie anaenda kwa ndg yake kumsalimia kumbe yuko bar au pengine hata hajamuambia chochote ila jamaa anajua bibie yuko tu nyumbani so inawezekana sana alikua pale hajafanya kosa lolote lakini kumbe jamaa wengine hawataki kabisa kusikia partners wao wako bar coz wengi hua wanaamini kua mwanamke mwenye heshima haruhusiwi kukaa bar tena mwenyewe bila ya jamaa yake
   
 7. Mwali

  Mwali JF-Expert Member

  #7
  Aug 21, 2012
  Joined: Nov 9, 2011
  Messages: 7,032
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Wala usiseme lolote. Hata ukihojiwa, umeona nini hapo?
  Huna ushahidi wowote kwamba alikua akifanya makosa.
  She just did not want you to disclose that to her man.
  Ukisema utakua mbea. maybe atamwambia mwenyewe.

  Anasubiri the right moment, ndio amwambie, au maybe
  ana sababu zake za kumficha mumewe kuhusu mtoko huo.
  We chuna, kaa pembeni. Ukiulizwa na rafiki yako maybe...
  ila usijaribu kukurupuka na kumwambia rafiki yako. DON'T!
   
 8. CORAL

  CORAL JF-Expert Member

  #8
  Aug 21, 2012
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 2,477
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Kwanza usimfikirie vibaya shemeji yako. Amini kuwa yale aliyokwambia ni ukweli. Kuhusu ni kwa nini awe ma wasiwasi je, mkeo kama unamruhusu kwenda baa na pengine unaenda naye nyakati fulani, ukiambiwa na mtu kuwa alimwona baa wakati wewe umesafiri je utakuwa na amani? Je si utafikiri kuwa labda huyu anayeniambia kuna mambo mengine anaficha? Hata kama atakuhakikishia kuwa hakukuwa na jambo lisilo la kawaida, bado utajiuliza , kwa nini anisimulie? Lazima kuna kitu kinafichwa. Kwa hiyo shemeji yako anataka v kuepusha wasiwasi kwa mumewe usio wa lazima. Kwa hiyo wewe mjulishe tu kuwa hayo ni mambo ya kawaida ni hayatoshi kuwa ajenda ya kuwambia mumewe. Ukimuhakikishia, hata kama mumewe ataambiwa na mtu mwingine wewe unapaswa kuwa mtetezi wa shem wako. Usipuuze mambo madogo, yanaweza kuwa chanzo cha mzozo mkubwa katika ndoa.
   
 9. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #9
  Aug 21, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,176
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  she was guilty ndo mana kakuwahi!mapenzi bwana kitu ya ajabu kabisa unajua unaweza kumueleza rafiki yako halafu kibao kikakugeukia zaid,manake na siye tukiamua kuwaweka pabaya huwa tunawalisha na kuwatapisha vingi i see,we nyamaza tu atakuja kujikamatisha mwenyewe,na usithubutu kumwambia rafiki yako kuwa uliwahi kumuona maeneo fulani shem wako hata kama kuna siku atakuja kukushtakia,we uchune tu!manake atakuona na we sio.kifua kaka kifua !NGUMU KUMEZA TAMU KUTEMA.pole kakangu!
   
 10. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #10
  Aug 21, 2012
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,676
  Trophy Points: 280
  Hebu tujifanye wajinga.Kisha tufikiri hivi;huyo shemejio hapendi jamaa yake ajue alienda bar ndo maana amekuambia usimwambie,sio kwamba alikua analijamaa.Vipi hiyo,inalipa?
   
 11. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #11
  Aug 21, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,176
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280
  yaah sms usiifute in case of anything!
   
 12. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #12
  Aug 21, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  What if kama hakuwepo pale kwa nia nzuri mtotowamjini?
  Nini nafasi yangu kama broo akijua kuwa i was there and i didn't disclose the issue to him??
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #13
  Aug 21, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  well said Mwali
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #14
  Aug 21, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  snowhite i really feel the same way!
  I even thought of the same hypotheses!!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. Blaki Womani

  Blaki Womani JF-Expert Member

  #15
  Aug 21, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 8,467
  Likes Received: 3,738
  Trophy Points: 280
  labda alishakatazwa kwenda mahala kama hapo akiwa pekee au pamoja na marafiki so anaogopa mwenzie kujua hilo piga kimya kama kuna lolote litatokea hapo baadae utajua nini cha kufanya
   
 16. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #16
  Aug 21, 2012
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,933
  Likes Received: 2,085
  Trophy Points: 280
  Huo kwa kweli ni mtego! Hudhani pia kuwa inawezekana anataka kuona kiwango cha mapenzi (au loyalty) ulichonacho kwa huyo rafiki yako (mumewe)?

  Kama ningekuwa ni mimi, ningem press huyo shemeji aniambie ukweli wote ni kwa nini anataka nimtunzie hiyo siri. Pengine Mungu anataka "kumwokoa" rafiki yako kupitia kwako...kuwa makini usimwache rafiki yako aangamie.
   
 17. Watu8

  Watu8 JF-Expert Member

  #17
  Aug 21, 2012
  Joined: Feb 19, 2010
  Messages: 47,347
  Likes Received: 2,685
  Trophy Points: 280
  muhimu uchuna tu, unaweza zua balaa bure
   
 18. SnowBall

  SnowBall JF-Expert Member

  #18
  Aug 21, 2012
  Joined: Sep 13, 2011
  Messages: 3,067
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Eiyer na mimi hili nimelifikiria pia..
  Thats why mpaka sasaivi sijafanya lolote..
  But nimeshindwa kusimama sana kwenye hili baada ya kujiuliza kwa nini anizuie kusema lolote?
  What is behind the scene!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. snowhite

  snowhite JF-Expert Member

  #19
  Aug 21, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 14,176
  Likes Received: 2,136
  Trophy Points: 280

  na kweli we jilie zako kobis,ataingia tu kwenye 18 za mumewe watakamatana wenyewe!
   
 20. hovyohovyo

  hovyohovyo JF-Expert Member

  #20
  Aug 21, 2012
  Joined: Jul 8, 2012
  Messages: 540
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Tuseme hata kama ungependa kumwambia rafiki yako, ungeanzaje na ungemalizaje?. Bila shaka ungeishia kuwa ulimwona shemejio bar, akinywa. SO WHAT??. Njia bora ni kutulia. Kuna wakati niliwahi kumshitua rafiki yangu juu ya jambo kama hili (Nilishuhudia demu wake akigombana na mke wa mtu kwa kutuhumiwa kuwa ameingilia ndoa). Nilipomwambia jamaa, hakuniamini kabisa. In fact aliside na demu wake kuonesha kwamba anamwamini). So huwezi jua mume naye atareact namna gani. Achana naye!!
   
Loading...