Jamani hii ni nini? Mke wa jamaa mmoja ambaye sina ukaribu naye na wala sio jirani yangu kivileeee....lakini namfahamu mumewe ambaye anauwezo wa kimaisha .... gari mbili za kutembele ajira serikalini.. mkewe amemfungulia mradi wa kuku wa nyama na mayai..kifupi hela ya kubalilisha mboga haipigi chenga... lakini ananiambia shemeji nikopeshe 100,000/= lakini chonde chonde....mume wangu asijue.. iwe siri yetu... jamani ushauri...

Asipolipwa jee? Vitu vingine si vya kufanyia majaribio..! Eti unywe sumu halafu uangalia kama utaharisha, utakufa badala ya kuharisha.! Hilo jimama ni la kupigwa chini tu, mambo ya siri na mke wa mtu ya nini?Si kila anayekuomba msaada anataka mahusiano kwa nini mnakuwa na positive answers?Inawezekana huyo shemeji yako kweli ana shida na hiyo pesa pengine ana tatizo labda kwa upande wa familia yake na mumewe hayupo katika nafasi ya kumsaidia though kuna magari na anafanya kazi serikalini pamoja na hayo yote siku hazifanani,Kama upo katika nafasi ya kumsaidia tenda wema uende zako usigeuke nyuma na kama kweli una nia ya kumsaidia kwa dhati bile kuexpect return kwanini umshirikishe mumewe,wewe mpe km vigezo na masharti aliyokupa then angalia ustaarabu wako.
sometimes sisi viumbe huwa tunafikiria visivyo! huenda mama wa watu ana shida iliyomfika shingoni na haoni mtu mwingine wa kumkopa ila huyo shemeji wa kivileee! tuondokane na mentality za kihivyooo!
hakuna jambo ambalo ni jema utafanya na mke wa mtu alafu eti tufanye iwe siti mme wangu asijue,jamani aya mambo si yakufanyia majaribio ,mke wa mtu si mchezo
Alichosema chenye ujumbe hapo ni 'nataka iwe siri yetu'...