Habari wana mmu, Nina rafiki yangu mpendwa ktk Bwana,alikuwa na mpenzi wake aliempenda sana kuliko maelezo na kwa bahati mbaya hivi sasa wameachana,na kisa cha kuachana ni shem kudai kwamba Mungu ameongea nae kwenye ndoto kwamba huyo sio mkewe.
EPORA ni kweli Mungu husema na watu kwa maono au ndoto kumjua mmewe au mkewe mtarajiwa,lakini hii inahitaji watu waliokiroho sana wenye uwezo wa kupambanua mambo kulingana na neno la Mungu.
Maana ndoto wakati mwingine huja kwa sababu ya mawazo unakuta kijana amempenda binti anamfikiri sana matokeo yake ni kumuota na kujifanya ameoteshwa na Mungu kumbe ni akili yake.Lakini wengine hutumia njia hii kuwapata wasichana wenye imani sana kwa Mungu kuwa watamuogopa Mungu na kukubali kirahisi kwa vile ni Mungu amesema.
Hutokeaje mtu anamchumbia mtu baadaye anamuacha kuwa Mungu kasema siyo mkeo/mmeo?
...Mara nyingi watu huanza mahusiano au mazoea kabla ya kumuomba Mungu labda mtu anaona dada fulani anavyomheshimu alivyomkarimu anaaona kuwa huyu anaweza kuwa mkewe,na anamweleza nia yake hiyo ya kutaka awe mkewe.Sasa kwa vile mtu huyu anamtegemea Mungu wengi hihitaji kuthibisha kama kweli huyo ni mkewe kama siyo mwenyewe, Mungu anamwambia siyo huyo,na yeye inabidi amuache huyo na kuanza kuuliza kwa Mungu mkewe ni yupi hapo huweza kuonyeshwa mkewe/mmewe halisi.
Ila kwa watu walio makini zaidi hawawezi kumtamkia msichana kuwa ni mke mtarajiwa bila kuthibisha kwa Mungu,wakishathibitisha kwa Mungu ndiyo humjulisha na binti nia yake ya kuwa naye hata mimi nilitumia hii nimeona inalipa.
Kwa mwanaume mwenye hekima siyo vyema sana kumfuata binti na kumwambia unataka kumuoa vile Mungu kasema badala yake ni kumweleza jinsi amempenda na Kama Mungu ikimpendeza atamuoa.
"Mkwe mwenye busara mtu hupewa na Bwana"