Shekhe Suleiman Takadil

huyu ndio akimfunza nyerere Kiswahili ili aongee na waswahili pia namna ya kuongea nao. alifaulu kwani Julius aliweza japokuwa neno moja tu ndio lilimshinga kulitamka vizuri nalo ni TANGA-NYIKA
cc mohamed said
 
acha ujinga kama baba, mama wala babu yako hakushiriki ktk uhuru wa nchi basi usidhalilishe wana mapinduzi. kama muda huo akicheza bao je babu yako wewe akifanya nin kama sio kucheza na nyani tu porini na magovi yake.

Acha upuuzi Babu yangu alimchangia Nyerere nauli ya kwenda UN,wakati huo wazee wa Kariakoo walikuwa wakicheza bao.
 
Hivi ilikuwaje habari ya mzee Shekhe Suleiman Takadil alikuwa na nafasi gani katika kupambania uhuru wa Tanganyika
Sheikh Suleiman Takadir alikuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU kuanzia 1954 - 1958 alipofukuzwa TANU baada ya kutokea ugomvi baina yake na Mwalimu Julius Nyerere.

Si rahisi kumweleza Sheikh Suleiman Takadir kwa mistari miwili mitatu kwani historia yake ni ndefu sana katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Historia ya Sheikh Suleiman Takadir inaogopwa kutajwa kwa kuwa yeye alitoa tahadhari kuhusu hali ya baadae ya Waislam katika Tanganyika huru utabiri ambao nusu karne baada ya uhuru bado unawatia hofu viongozi walioshika madaraka.

In Shaa Allah natayarisha darsa kuhusu Sheikh Takadir na nitarejea tena hapa Majlis.

Sent using Jamii Forums mobile app

Hapo chini ni maisha ya siasa ya Sheikh Suleiman Takadir:

Mohamed Said: JINAMIZI LA UDINI TANZANIA: UTABIRI WA SHEIKH SULEIMAN TAKADIR
 
Sheikh Suleiman Takadir alikuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wazee wa TANU kuanzia 1954 - 1958 alipofukuzwa TANU baada ya kutokea ugomvi baina yake na Mwalimu Julius Nyerere. Si rahisi kumweleza Sheikh Suleiman Takadir kwa mistari miwili mitatu kwani historia yake ni ndefu sana katika kupigania uhuru wa Tanganyika. Historia ya Sheikh Suleiman Takadir inaogopwa kutajwa kwa kuwa yeye alitoa tahadhari kuhusu hali ya baadae ya Waislam katika Tanganyika huru utabiri ambao nusu karne baada ya uhuru bado unawatia hofu viongozi walioshika madaraka. In Shaa Allah natayarisha darsa kuhusu Sheikh Takadir na nitarejea tena hapa Majlis.

Sent using Jamii Forums mobile app

Hapo chini ni maisha ya siasa ya Sheikh Suleiman Takadir:

Mohamed Said: JINAMIZI LA UDINI TANZANIA: UTABIRI WA SHEIKH SULEIMAN TAKADIR

Mkuu nasubria kwa hamu saana hio Darsa yaSheikh Suleiman hapa majlis‍♂️
 
Bingwa wa mchezo wa bao mitaa ya Kariakoo.
Ngongo,
Sheikh Suleiman Takadir hakuwa bingwa wa bao.

Sheikh Takadir ubingwa wake ulikuwa katika ilm ya dini ya Kiislam.

Ubingwa wa Sheikh Suleiman Takadir ulikuwa katika fasaha alikuwa bingwa wa kuzungumza.

Mikutano yote ya TANU yeye ndiye alikuwa anatangulia kupanda jukwaa kufungua mkutano kwa dua kisha kumtambulisha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere.

Sheikh Suleiman Takadir alikuwa bingwa wa siasa za uhuru kiasi wana TANU wakampachika jina wakamwita, "Makarios," wakimfananisha na Padri Makarios wa Ugiriki ambae yeye pia alikuwa akiongoza mapambano dhidi ya Waingereza nchini kwake.

,
1552560300566.png

Kulia: Bi. Titi Mohamed, Clement Mtamila, Sheikh Suleiman
Takadir, Julius Nyerere na nyuma ni John Rupia, Rajab Diwani
na Mama Maria Nyerere.

Soma hapo chini historia ya Sheikh Suleiman Takadir:
Mohamed Said: JINAMIZI LA UDINI TANZANIA: UTABIRI WA SHEIKH SULEIMAN TAKADIR

Sent using Jamii Forums mobile app
 
acha ujinga kama baba, mama wala babu yako hakushiriki ktk uhuru wa nchi basi usidhalilishe wana mapinduzi. kama muda huo akicheza bao je babu yako wewe akifanya nin kama sio kucheza na nyani tu porini na magovi yake[/b][/u]
.

Kwani MTU anakuwa na magovi mangapi? Minimum na maximum
 
Kujua historia kunasaidia kujitafakari. Hii nayo wengine tunapata tafakari jadidu.
KUTOKA FB: SHEIKH SULEIMAN TAKADIR ALIVYOPOTEA KATIKA HISTORIA YA UHURU WA TANGANYIKA
Mohamed Said July 11, 2017 0
Mohamed Said Salum Ugomvi kati ya Sheikh Suleiman Takadir na Mwalimu Nyerere ndani ya ofisi ya TANU pale New Street ni katika matokeo ya historia ya TANU ambayo wana TANU wenyewe walipenda labda yafutike yasijulikane. Nadhani hata Mwalimu Nyerere hakupenda ugomvi ule uingie katika historia yake. Hakika ni kisa cha kusikitisha. Ugomvi huu alinihadithia marehemu Mzee Haidar Mwinyimvuababa yake Sheikh Ahmed Haidar ambae alikuwapo katika mkutano ule 1958 mara tu baada ya TANU kuamua kuingia katika Kura Tatu. Dr. Tamim ndiye aliyenipeleka kwa Mzee Haidar nyumbani kwake Magomeni. Alinieleza historia nzima ya Sheikh Takadir na ya Nyerere katika siku zile za mwanzo hadi Sheikh Takadir alipofukuzwa TANU. Kisa kizima nimekieleza katika kitabu cha Abdul Sykes.

scan0026.jpg

Kushoto ni Sheikh Suleiman Takadir, John Rupia na Julius Nyerere

Mohamed Said Salum Wakati wa utafiti wa kitabu cha Abdul Sykes sikuweza kupata picha ya Sheikh Takadir popote ikawa kama vile huyu mtu hakuwa katika TANU tena kiongozi wa juu kabisa. Picha yake ya kwanza nilikuja kuipata miaka hii ya 2000 na alinipa rafiki yangu marehemu Abdallah Kihombo nyumbani kwake Ilala. Baadae nikapata nyingine kutoka kwa Jim Bailey African Archive, Johannesburg...
 
Acha upuuzi Babu yangu alimchangia Nyerere nauli ya kwenda UN,wakati huo wazee wa Kariakoo walikuwa wakicheza bao.
inaonekana umeamua kuthibitisha kuwa wewe ni kichaa kama mjombako. hao wacheza bao ndio waliomvua Mwl kaptura wakampa suruali, wakamzuia asitembee na baiskeli baada ya kumpa gari. wakamktia tiketi za UN then we unaleta uzuzu hapo tenaa mkoa wenu hata mmoja aliedai uhuru
 
inaonekana umeamua kuthibitisha kuwa wewe ni kichaa kama mjombako. hao wacheza bao ndio waliomvua Mwl kaptura wakampa suruali, wakamzuia asitembee na baiskeli baada ya kumpa gari. wakamktia tiketi za UN then we unaleta uzuzu hapo tenaa mkoa wenu hata mmoja aliedai uhuru

Mtamvua Nyerere kaptula wakati alishatangulia siku nyingi UK wakati wazee wa kariakoo ujanja wao haukuwa zaidi ya Gerezani na Tandamti.
 
Mtamvua Nyerere kaptula wakati alishatangulia siku nyingi UK wakati wazee wa kariakoo ujanja wao haukuwa zaidi ya Gerezani na Tandamti.
Kabla ya kutumwa mwl UN kumbuka wazee haohao wa Kariakoo walishaenda huko kudai uhuru baada ya Malkia kukataa ndipo wakamtafuta Mwl kwani alikuwa na sifa alizotaka Queen.
 
Back
Top Bottom