Donatila
JF-Expert Member
- Oct 23, 2014
- 8,274
- 25,322
SHEKHE Mkuu wa Baraza la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Mufti Abubakari Zuberi.Pamoja na kuwashukuru madaktari na wauguzi kwa juhudi kubwa wanazofanya kunusuru maisha ya watu.
Mufti aliwatembelea wagonjwa hao jana mchana, baada ya kumalizika kwa Swala na Baraza la Idd El Fitri kitaifa iliyofanyika Msikiti wa Riadha, Moshi mjini.
Alisema BAKWATA na Waislamu kwa ujumla wana utaratibu wa kutimiza misingi ya uislamu kwa kutembelea wagonjwa na kuwafariji, kutoa sadaka, misaada na kula chakula na yatima.
Akiwa hospitalini hapo, Mufti alimshukuru pia Rais John Magufuli na serikali yake kwa kuona umuhimu wa kuisaidia hospitali ya Mawenzi kukabiliana na changamoto ya wagonjwa kwa kuipatia kiasi cha Sh. milioni 800 za kuendelea na ujenzi wa jengo la ghorofa tatu la wodi ya mama na mtoto.
Kazi ya ujenzi wa jengo hilo kwa sasa inatekelezwa na Wakala wa Majengo nchini (TBA), ili kupunguza mzigo wa msongamano wa wagonjwa na Hospitali ya Rufani ya KCMC.
Mkoa wa Kilimanjaro una hospitali kubwa tatu za rufani ambazo ni hospitali ya rufani ya KCMC,hospitali ya taifa ya magonjwa ya kifua kikuu ya Kibong’oto na hospitali ya rufani ya mkoa wa Kilimanjaro Mawenzi.
Baada ya kumaliza ziara yake hospitalini hapo alikwenda kula chakula na yatima zaidi ya 80 kutoka vituo mbalimbali vinavyolea watoto hao katika mji wa Moshi katika Shule Kuu ya Polisi Moshi (MPS).
Chanzo: Nipashe