Elections 2010 Shein bila viatu Ofisini, ipoje?

Indume Yene

Platinum Member
Mar 17, 2008
2,950
711
Nilijaribu kuangalia hii picha kwa makini sikuweza kupata jibu mapema. Nilifikiri jamaa yuko msikitini lakini hapa anasaini fomu za kugomea Urais Zenji mbele ya Jaji mkuu wa Zanzibar (Mh. Hamid Mahamoud). Angalia picha sehemu yenye mzunguko mwekundu.
Mwenye maoni tofauti....
SHENI1.JPG
 
SHENI.jpg
Kuna vitu vingine vinahusu tamaduni ya sehem husika. Hiyo ndiyo zanzibar wao wamejitahidi saana kuwa wanavyoona inafaa kwao kuliko kuiga.
 
Mh... Zanzibar wanakaa ofisi pekupeku kama bata?
Hebu angalia hapo pahala panafanana na kitu ofisi?

Hiyo picha ukiangalia utakuta Jaji Mkuu Hamid Mahmoud (Kati kati) na Jaji wa Mahakama Kuu Mh. Mshibe Ali Bakar (kushoto) wote wamevua viatu, ikiashiria kuwa eneo walipo ni safi na haliruhusiwi kuingia na viatu kwa mtu yeyote.
 
Asijeanguka jukwaani na viatu vikadondoka;

Basi avae soksi
 
Nilijaribu kuangalia hii picha kwa makini sikuweza kupata jibu mapema. Nilifikiri jamaa yuko msikitini lakini hapa anasaini fomu za kugomea Urais Zenji mbele ya Jaji mkuu wa Zanzibar (Mh. Hamid Mahamoud). Angalia picha sehemu yenye mzunguko mwekundu.
Mwenye maoni tofauti....

Angalia wenziwe(jaji Mkuu na Mrajisi Mkuu) wao pia hawana viatu. Shein kwa siku hiyo hakuvaa viatu vya buti vinavyomfanya avae soksi. As simple as that!
 
Jamani hata soksi hana ama kweli huyu mzee wa mikasi ufisadi haujui Kribu upande wetu! Hii kali kabisa shemeji zangu wazenji wakiwa ofisini ni peku peku
 
Hebu angalia hapo pahala panafanana na kitu ofisi?

Mkuu Junius,

Ina maana walikuwa nyumbani kwa mtu? Ninapata mashaka kwamba Dr. Shein alikuwa nyumbani kwake na hao jamaa walienda kumfuata ili kumsainisha fomu zake. Maana huo mkao wake sioni kama una ashiria kwamba Mzee alikuwa kiofisi ofisi. Ofisi za serikali huwa zina dress code?

Hiyo picha ukiangalia utakuta Jaji Mkuu Hamid Mahmoud (Kati kati) na Jaji wa Mahakama Kuu Mh. Mshibe Ali Bakar (kushoto) wote wamevua viatu, ikiashiria kuwa eneo walipo ni safi na haliruhusiwi kuingia na viatu kwa mtu yeyote.

Mkuu wewe ni mwenyeji huko Zenji, naomba niambie kuna ofisi yoyote ya serikali (SMZ) au taasisi ya umma ama idara/kitengo cha SMZ ambayo watu wakiwa ofisini wanatakiwa kuvua viatu?
 
Dr. Shein alikuwa nyumbani kwake na hao jamaa walienda kumfuata ili kumsainisha fomu zake?

Bila ya shaka.

Mkuu wewe ni mwenyeji huko Zenji, naomba niambie kuna ofisi yoyote ya serikali (SMZ) au taasisi ya umma ama idara/kitengo cha SMZ ambayo watu wakiwa ofisini wanatakiwa kuvua viatu?

Ni kweli zipo ofisi za umma Zanzibar ambazo kuna maeneo maalum, kwa sababu maalum, watu hawaruhusiwi kuingia na viatu.
 
..hata mimi naanza kuwa na wasiwasi kwamba hapo ni nyumbani kwa Dr.Shein.
 
..hata mimi naanza kuwa na wasiwasi kwamba hapo ni nyumbani kwa Dr.Shein.
Hapo bila shaka ni nyumbani siyo ofisini. Kwani kuna tatizo gani? Huyo bwana ameishaanza kupewa heshima ya Urais hata kabla ya kupigiwa kura. Ni ishara ya awali kwa mavu (Maalim) kuwa hana lake kwenye urais. Kwa hiyo ajitayarishe kwa nafasi mojawapo ya umakamu.
 
Tatizo ni kwamba sheria inaruhusu Jaji Mkuu na Msaidizi wake kwenda nyumbani kwa Mgombea kupata signature?

Nadhani hio itakuwa kwamba Jaji Mkuu na Msaidizi wake wamevunja Sheria... It means walikwenda nyumbani kwa Mgombea wa chama cha Asilia Jahazi?
 
Tumeambiwa ni utamaduni kwa hiyo hakuna tatizo, isitoshe carpet la uhakika.
 
Back
Top Bottom