Sheikh yahya bado anatabiri;mbona aliaga amengatuka??

Pdidy

JF-Expert Member
Nov 22, 2007
50,956
22,153
Wanandugu wa utabiri hivi mh huyu bado anaendelea kutabri nakumbuka alisema kwenye tv amecha na kumwachia mwanae aendelee kutabiri..mmh hizi tabiri zinaanza kuntisha sasa!!!ndio yale watu wanakula pension ppf wanarudi tena kazini??

Shekhe Yahya awatabiria mikosi wanasiasa


Monday, 11 April 2011 21:00
0diggsdigg
Mwandishi Wetu
MTABIRI maarufu Afrika Mashariki na Kati, Shekhe Yahya Hussein, amesema baadhi ya viongozi na wafanyabiashara maarufu nchini kuwa wengi wao watatekwa na kuporwa mali zao na kwamba matukio hayo yatafanyika kati ya mwezi huu na Julai mwaka huu.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Shekhe Hussein aliwataka viongozi na wafanyabiashara hao, kuchukua tahadhari katika shughuli zao na hasa katika kipindi hicho.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, viongozi hao wanapaswa kujichunga ili wasitekwe, wasiibiwe mali zao na kufanywa bidhaa."Kuanzia April 19 na kuendelea hadi Julai viongozi wa vyama vya siasa na wafanyabiashara maarufu, wajichunge ili kuepuka kutekwa nyara na kuibiwa na hata wao wenyewe kufanywa kama bidhaa," alisema Shehe Yahaya.

Alisema kwa kipindi hicho viongozi hao wanapaswa kuchukua tahadhari kubwa hasa katika matembezi yao ya kila siku.Alisema utekaji nyara huo dhidi ya watu waliotajwa, utafanyika wakiwa safarini au kwenye mikutano na kwamba ni vizuri wasiwe peke yao.
 
Na mimi natabiri kuwa kuanzia mwezi wa sita kutakua na watu wangi sana mitaani wanaomba kazi.
 
Qwi qwi qwi qwi

m naogopa kutabiri kuanzia jana nimeamua saa mbili nalala mapema nioteshwe kikombe utabiri unatisha sheikh!!wacha tuombe tuoteshwe
 
Sasa mnatarajia afanye kazi gani wakati kunawatu wanamuamini na hawawezi kuendesha maisha yao bila kumuuliza huyo mganga wao mpaka siku wataisha watu wenye imani naye ndiyo itakuwa mwisho wa kazi yake.
 
Utabiri gani unaambatana na ushauri ................yaani kwa mfano alitabiri kuwa kikwete atakufa kabla ya uchaguzi halafu akampa ushuri wa jinsi ya kukwepa kifo...................ila jamani hizi dini......kwa kweli waislamu wanadanganywa sana na imani..................inakuwaje mtu anatabiri na kutoa suluhisho/ushauri wa kukwepa kitakahotokea?..............kweli wajinga ndio waliwao.
Binafsi sipendi kusikia uchafu huu wa sheikh yahaya.....natabiri sheikh yahaya atakufa kabla ya june 2011
 
Yahaya njaa tu inamsumbua. Inteligensia inamwambia mambo fulani ili kuprempty starategy yao isishtukiwe. Kama wana mpango wa kufanya maovu, safari hii imekula kwao.
 
Back
Top Bottom