Sheikh yahya anusurika kuuawa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sheikh yahya anusurika kuuawa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Sumbalawinyo, Mar 17, 2010.

 1. Sumbalawinyo

  Sumbalawinyo JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2010
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 1,286
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  SHEIKH YAHYA ANUSURIKA KUUAWA

  [​IMG]Habari zisizo na shaka zinasema kuwa mashabiki hao, wengi wao wakiwa wa Klabu ya Simba, walivamia nyumbani kwa mnajimu huyo kwa lengo la ‘kumrudi’ kutokana na kile kilichodaiwa kuwa ni kutoa utabiri feki dhidi ya klabu yao.

  Siku hiyo (usiku), mashabiki wa Simba wakiwa na kiwewe cha timu yao kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2010 baada ya kuifunga Azam FC na kufikisha pointi 56 ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote, waliandama hadi kwa Sheikh Yahya.
  Wakiwa nyumbani kwa mtabiri huyo, mashabiki hao walikuwa wakiimba nyimbo za kumdhihaki mtabiri huyo, huku wengine wakipoteza uungwana ‘kabisa kabisa’ na kutoa matusi.

  Kama hiyo haitoshi, mashabiki hao waliendelea kuporomosha maneno makali na kusisitiza kwamba ni lazima wamuone Sheikh Yahya.
  Kutokana na hali hiyo, majirani wa Sheikh Yahya walitoa taarifa polisi ambapo ‘vijana wa Mwema’ walitinga eneo la tukio na kurusha risasi ambazo ziliwatawanya mashabiki hao.

  Awali, ilidaiwa kuwa Sheikh Yahya alitabiri kuwa Simba ingepoteza mchezo dhidi ya Azam, hivyo isingeweza kutangaza ubingwa siku hiyo.
  Hata hivyo, kabla ya timu hizo kuingia uwanjani, Sheikh Yahya alijitokeza na kukanusha habari hizo na kutoa msisitizo kwamba katika maisha yake ya utabiri hajawahi kutabiri mechi ndogo, isipokuwa hufanya hivyo kwa Simba na Yanga, tena kwa malipo.

  “Ieleweke pia kuwa utabiri wa mpira niliacha tangu mwaka 1977, na nilikuwa natabiri mechi za Simba na Yanga, mimi huwa sitabiri timu ndogo. Na huwa sitabiri bure.
  “Kwa sasa utabiri wa mpira wanafanya wanafunzi wangu, mimi siwezi kutabiri Simba na Azam, hata mjinga kiasi gani alikuwa akijua kuwa Simba lazima iishinde Azam, naushangaa uvumi huu,” alisema Sheikh Yahya kabla ya mechi hiyo, iliyochezwa Jumapili, Uwanja wa Uhuru, Dar.

  Aliongeza: “Sijapendezwa na usumbufu kwa mashabiki wa Simba na kwa kumpakazia kitu kama hicho, inavyoonekana kuna watu wanataka kazi hii ya utabiri, lakini wanakosea sana wanaponitumia kwa kupotosha umma.

  [​IMG]
   
Loading...