Sheikh: Wakristo wana haki kuchinja

Sheikh: Wakristo wana haki kuchinja

Status
Not open for further replies.

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,803


IJUMAA, APRILI 12, 2013 06:22 NA ASIFIWE GEORGE, DAR ES SALAAM

SHEIKH wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhadi Mussa Salum, amezungumzia mzozo wa kuchinja na kusema kuwa muumini wa dini yoyote anahaki ya kuchinja. Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Sheikh Salumu, alisema suala la kuchinja kila mtu anaweza kuchinja kutokana na imani yake.

Alhad alisema muumini wa dhehebu lolote anaweza kuchinja, huku akitoa angalizo kuwa uchinjaji huo uzingatie imani ya watumiaji wa nyama hiyo.

Sheikh Alhad alisema kwamba Wakristo wana haki ya kuchinja ilimradi nyama hiyo ni kwa ajili ya matumizi yao wenyewe katika familia zao na si vinginevyo.

“Binafsi sina tatizo katika suala la kuchinja kwani kulingana na utamaduni tuliokuwa nao Wakristo wana haki ya kuchinja kwa matumizi yao wenyewe na kama ni kwa ajili ya matumizi ya umma basi Waislamu wafanye hivyo,”alisema.

Aidha alizidi kusisitiza kuwa suala la kuchinja linahitaji mjadala miongoni mwa viongozi wa dini wenywewe na si kuitupia lawama Serikali kwa kuibua mijadala ambayo ni vigumu kwa Serikali kuwa na majibu yake kwa wepesi zaidi.

Alisema Serikali haiwezi kusuluhisha tatizo hilo bali ni kusimamia utatuzi wake, hivyo viongozi wa dini wana wajibu wa kuandaa mijadala yenye lengo la kuweka sawa mambo hayo.

“Kwa kupitia mijadala hii itakayo waunganisha viongozi wa dini zote mbili, wananchi wataweza kupata ukweli wa mambo mbalimbali yanayoonekana kuwa kero na yanayohatarisha ustawi wa amani ya nchi yetu.

“Sote ni wadau wa amani hivyo ni wajibu wetu sisi viongozi wa dini kukaa na kuzungumzia matatizo yaliyopo ili tuweze kurejesha amani ambayo kwa sasa inatetereka ,”alisema Sheikh Salum.

 
Hili liko wazi.Tatizo ni serikali kuendelea kuukuza huu mgogoro.
 
Huyu shekhe anaonekana angalau amegusa form four ndiyo maana kuna traces za points kwenye mawazo yake.
 
Huyu shekhe anaonekana angalau amegusa form four ndiyo maana kuna traces za points kwenye mawazo yake.

Sheikh ametumia hekima na busara katika suala hili. Je kuna shule inafundisha hizi tunu?
 
This is too much! Kila mtu anakurupuka na kuzungumza anavyojisikia yeye. Tutakuwa na wasemaji wangapi na wameruhusiwa na mamlaka ipi kuzumgumzia hili?

Mbona nchi za jirani zetu kama: Kenya, Uganda, Malawi, Rwanda n.k. suala la 'nani achinje' siyo tatizo? Kwanini iwe hapa kwetu Tanzania kwenye 'kisiwa cha Amani'!
 
huyu shehe kaongea kipi kipya? Anyway, kwa kuwa wakristo hatunaa habari za kujikweza tunawaachia wao waendelee kuchinja za umma. Lakini, hawa waislam waache upuuzi na chokochoko zao dhidi ya ukristo! Kila leo mihadhara, kanda za kijinga tu, kauli za kihayawani, chuki dhidi ya mkristo... Kwani mkristo jiwe? Mkristo akasema kwa kuwa unanifuata hadi chumbani na kunighasi basi ngoja nikuonyeshe kuwa naweza kukudhibiti. Sasa mkristo kusema nae anataka kuchinja kwa nini mkereke? Hivi hiyo mihadhara na kejeli na viitisho dhidi ya mkristo ni ibada pia? Turudi tuishi kama zamani kwani masuala ya imani ni kuvumiliana na si kingine, ila kuvumilia hakuwezi kuwa pande moja.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom