Sheikh Ponda: Tamko lililotolewa na Sheikh Ramadhani si la jumuiya, ni lake mwenyewe

saidi kindole

JF-Expert Member
Sep 21, 2012
310
792
MKUTANO ulioitishwa na Sheikh Juma Ramadhan, Naibu Amiri wa Shura ya Vijana na Maimamu wa Mkoa wa Dar es Salaam, umeratibiwa na uongozi wa Chama cha Wananchi (CUF). Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Mtoa taarifa ndani ya CUF amesema, mkakati wa kuitisha mkutano huo na kupachikwa jina ‘Mkutano wa Masheikh kuhusu neno Takbiri’ linalolalamikiwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa dhidi ya Chama cha ACT-Wazalendo, umefanywa kunufaisha CUF.
“Baada ya msajili kuiandikia barua ACT-Wazalendo na baadaye Zitto (Zitto Kabwe, Kiongozi wa ACT-Wazalendo) kufafanua huku akitaka viongozi wa dini watoe ufafanuzi wa neno takbiri.

“Hii ilionekana kuwa karata ya kisiasa, ndipo akatafutwa mtu ambaye atasimama na kutoa tafsiri hiyo kwa malengo maalum. Mkakati ukapangwa,” amesema mtoa taarifa bila kutaja jina la aliyeandaa mkakati huo ndani ya CUF.

Leo tarehe 27 Machi 2019 Sheikh Juma Ramadhan ambaye pia ni Naibu Amiri wa Shura ya Vijana na Maimamua Mkoa wa Dar es Salaam amewaeleza waandishi wa habari kuwa, kitendo cha kutamka neno hilo wakati wa kupandishwa bendera ya ACT-Wazalendo visiwani Zanzibar ni kinyume na Maadili ya Dini ya Kiislam.

Kwenye mazungumzo yake na waandishi Sheikh Ramadhan ambaye pia ni Imamu wa Masjidi Taqwa Mwananyamala amedai kitendo hicho kinaidhalilisha Dini ya Kiiislamu.

Amesema, takbira ambayo ni maneno ya kumtukuza Mwenyezi Mungu hutamkwa mahala patakatifu na kwamba, wanaodaiwa kuwa wafuasi wa ACT-Wazalendo hawakulitamka katika mahala sahihi.

“Kitendo kilichofanywa na ACT-Wazalendo kikiwa kinaongozwa na Zitto cha kupandisha bendera ya chama chake katika nchi ya Zanzibar kwa maneno matukufu, maneno ya kuashiria takbira kisijirudie tena,” amesema.

Sheikh Ramadhani amewataka Zitto na chama chake kuomba radhi Waislamu kutokana na kauli hiyo la sivyo, yeye kama kiongozi wa vijana wa Kiislamu mkoani Dar es Salaam ataagiza vijana hao wakabiliane na chama chake ikiwemo kuomba dua kwa MwenyeMungu ili chama hicho kifutwe.

“La sivyo vijana wa Dar es Salaam watasubiri maamuzi tutakayotoa kwa chama chao ili wakabiliane na ACT-Wazalendo na hili hatushindwi,” amesema.

Hata hivyo, Jumuiya na Taasisi za Kiislam nchini inayosimamia Jumuiya ya Shura ya Vijana na Maimamu imeeleza kuwa, kilichofanywa na Sheikh Ramadhan na wale alioongozana nao ni cha kwake peke yake.

Sheikh Ponda Issa Ponda, Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam alipoulizwa na MwanaHALISI ONLINE kama jumuiya yao inatambua tamko hilo, amekana.

“Kwanza umefanya vizuri kuniuliza. Niseme tu kwamba, kilichozungumzwa na Sheikh Ramdhani ni cha kwake mwenyewe na si cha jumuiya.

“Kila jambo kwenye jumuiya zetu kuna utaratibu tumejiwekea hasa kwa suala kubwa kama hilo. Sheikh Ramadhan anajua mwenyewe alichokieleza na sio msimamo wa jumuiya ambayo yeye ni Naibu wa Shura ya Vijana,” amesema Sheikh Ponda.

Amesema, ameshangaa kuona tamko lile na kwamba, baada ya kupata taarifa hizo aliwasiliana na vijana kwenye jumuiya hiyo kujua msingi wa tamko hilo.

“Nilipouliza walisema hawajui lolote. Nashangaa kuona tamko linatolewa halafu vijana wenyewe hawajui chochote. Nasisitiza tamko ni lake na lichukuliwe kama lake na sio taasisi,” amesema Sheikh Ponda.
 
jamani hili ni neno tu,sema hawa act walifanya vibaya kutumia neno la kiarabu,wangelisema kwa kingereza ingependeza zaidi,lakini kitendo cha kutumia kiarabu,huu ni udini mkubwa,nashauri hatua kali sanya zichukuliwe,hawawezi kutumia kiarabu wakati wakijua kabisa waarabu ni magaidi wakubwa na hatuwapendi kabisa na ni maadui
 
Akili za hawa masheikh wengine wanazijua wenyewe. Yaani unaitisha kikao kujadili matumizi ya neno la kiarabu la kumuenzi mungu wenu halafu unatoa tamko kwa waandishi wa habari kuwatishia waliomuenzi huyo mungu!
 
Waislamu wanao ishi jijini dar es slam wamuijia juu mh zitto kutokana na wanachama
wa ACT wazalendo wanaoishi zanzibar kupandisha bendara huku wakitumia kulaani

Habari nzima iko hapa

 
Waislamu wanao ishi jijini dar es slam wamuijia juu mh zitto kutokana na wanachama
wa ACT wazalendo wanaoishi zanzibar kupandisha bendara huku wakitumia kulaani

Habari nzima iko hapa


Kwani Takbir maana yake nini?

Mbona waislamu hutumia salamu ya Bwana Yesu Asifiwe kwenye dhifa mbalimbali za kitaifa!.......mnalisemeaje hilo?!
 
Back
Top Bottom