Mkuu
sensor, kuhusu Ponda sikuupandisha Uzi bali nilichangia mada tu.
Ilionekana bayana kuwa Serikali ya CCM isingemuachia huru Ponda kabla ya Uchaguzi Mkuu, maana walijua angeweza kuwahamasisha Waislam wasiichague CCM kwa kuwa ilishindwa kuitekeleza ahadi yake ya kuwapa Waislam Mahakama ya Kadhi.
Ikumbukwe Ponda pamoja na wenzake walifanya zoezi la Sensor ya Taifa kuingia dasari kwa kuwaamasisha Waislam wasikubali kuhesabiwa na kweli baadhi yao hawakuhesabiwa, hivyo Serikali iliona wakimuachia kabla ya Uchaguzi anaweza kukumbusha mambo ya Mahakama ya Kadhi.