tonicimmobility
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 493
- 1,038
Sheikh wa Mkoa wa Dodoma, Sheikh Mustafa Rajab, amesisitiza kwamba maandamano yanayokubalika ni yale ya wananchi kwenda kwenye vituo vya kupiga kura na kurudi nyumbani, akiwahimiza Watanzania kushiriki kikamilifu katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 29, 2025.
Soma pia: Sheikh Alhad Mussa: Tusiingizane mkenge, hakuna maandamano Oktoba 29, piga Kura rudi nyumbani
Akizungumza leo Oktoba 25, 2025 jijini Dodoma, katika kongamano la viongozi wa dini wa Kanda ya Kati (Dodoma na Singida) kuliombea taifa amani na utulivu kuelekea uchaguzi, Sheikh Rajab amesema wanapaswa kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu, kusisitiza Watanzania wajitokeze kupiga kura.
“Hakuna maandamano mengine isipokuwa yale ya wananchi kuandamana kwenda kwenye vituo vya kupiga kura na kurudi nyumbani. Kama viongozi wa dini, tunaendelea kuyahamasisha maandamano haya halali. Maandamano mengine hayapaswi kuungwa mkono na tuna wajibu wa kuyakemea,” amesema Sheikh Rajab.