Hashpower7113
JF-Expert Member
- Sep 26, 2011
- 1,353
- 2,144
Kutoka kwa Sheikh Ahmed Kandauma
Kila sifa njema anastahili Mola wa ulimwengu huu ambaye ni Allah Subhannahu Wataalah, na rehema na amani ziwe juu yake Mtume Muhammad (S.A.W).
Tunamshukuru Allah kwa kutuwezesha kukutana tena katika ukurasa huu ambapo tutajadili mambo mbalimbali yanayotusaidia kuijua dini yetu ya Kiislamu.
Leo tunazungumzia kuhusu ndoa na umuhimu wa kuoneshana mapenzi na huruma katika ndoa.
Kwanza kabisa yatupasa kujua kuwa ndoa ni ibada tukufu sana ambayo huambatana na mapenzi ya dhati kati ya mume na mke. Tukumbuke kuwa ndoa ni muungano wa watu wawili, mwanaume na mwanamke.
Lazima pia ufahamu kwamba ndoa ina masharti yake na kanuni zake lakini mapenzi ndiyo kitovu cha ndoa. Alama kubwa ya ushamiri na umahiri wa ndoa ni mapenzi ya dhati kutoka kwa mume na mke.
Mapenzi ya dhati kwa mume huleta furaha na amani ndani ya ndoa pamoja na uvumilivu. Hakika huwezi kumvumilia mtu ambaye huna mapenzi naye ya dhati.
Subira na msamaha hupatikana kwa wapenzi wa kweli ambao wanapendana kwa dhati kutoka ndani ya mioyo yao. Ifahamike kwamba mapenzi ya dhati siku zote hujificha ndani ya moyo wa mume na mke lakini katika ndoa, mapenzi haya yanapaswa kuonekana waziwazi kwa wanandoa wawili.
Ili upate heshima ya ndoa basi ni lazima kuwe na mapenzi ya dhati kwa mume na mke. Niwarekebishe kidogo wale ambao wanafikiri mapenzi ni kulala kitandani au kujamiiana pekee, laa hasha, kule ni kutekeleza kitendo lakini kwanza mapenzi yanaanza moyoni ili hata mkikutana sehemu ya faragha inakuwa raha mustarehe.
Mwenyezi Mungu anatufafanulia katika kitabu kitukufu cha Quraan kwamba ndoa ni alama au ishara ya uwezo wake Allah na uwepo wake Allah.
Lakini pia anatueleza kuwa ndoa ni mapenzi kati ya mume na mke.
Katika Surat Ruum, aya ya 21, Quraan inasema:
“Na akatia mapenzi na huruma kati ya mume na mke...”
Natumaini tumepata ushahidi juu ya kuwa ndoa ni mapenzi na huruma kupitia aya hii.
Ni kwa vipi utaweza kuipata huruma kwa mume au mke?
Kwanza ili huruma iweze kupatikana ni lazima mume ajue nafasi yake kwa mke na mke ajue nafasi yake kwa mume ndiyo huruma itajengeka kwa wawili hao.
Mume amhurumie mke kipindi amechoka na yale mapungufu yake ya kibinadamu. Mke naye amhurumie mume kipindi ana msongo wa mawazo na yale mapungufu yake ya kibinadamu.
Tambua ewe mume au mke ndoa ni mapenzi ya dhati na huruma kutoka moyoni.
Niwatakie mafanikio mazuri ya ndoa zenu na baraka tele.
Tunamuomba Allah atuongoze katika haki.