Sheikh Farid: Kwanini nishitakiwe kwenye mahakama ya Tanganyika?

GEBA2013

JF-Expert Member
Feb 22, 2014
4,325
4,734
wakuu nimesikia hi habari kwenye gazeti la Mtanzania la leo,Sheikh Farid aliyekuwa anashatkiwa kwa tuhuma za ugaidi na wenzake,alimwuliza hakimu wa mahakama ya Kisutu,kwamba kwanini ashtakiwe Tanganyika nawakati yeye sio mtanganyika?

Kwanini nisishtakiwe Zanzibar na wakati ni nchi na ina mamlaka yake kamili kama mahakama?

MY TAKE: Wazanzimbar sasa hivi wanajitambua wanahitaji nchi yao.Wanataka mamlaka yao kama dola huru isiyoingiliwa kimamlaka na upande mwingne wa utawala.
====================================

KIONGOZI wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI), Sheikh Farid Hadi Ahmed (43), jana amezua tafrani mahakamani baada ya kuhoji kwanini anashitakiwa Tanzania Bara kwa ugaidi wakati Zanzibar ni nchi ambayo ina Mahakama Kuu.

Sheikh Farid alidai hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam mbele ya Hakimu Mkazi, Hellen Riwa baada ya kuunganishwa na watuhumiwa wengine 19 wa ugaidi na kufanya idadi yao kufikia 20.
Sheikh-Farid-Hadi-Ahmed.jpg

Kiongozi wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar (JUMIKI), Sheikh Farid Hadi Ahmed

"Mheshimiwa hakimu, sisi wote hapa tunatoka Zanzibar, hatuna ndugu hapa, gerezani wanazuia watu wasije kutuona.

"Tumetolewa Zanzibar tumekuja kushitakiwa huku Tanganyika, kwani Zanzibar hakuna Mahakama Kuu? kwanini tusishitakiwe kwenye nchi yetu?

"Zanzibar ina kila kitu, yupo Mwanasheria Mkuu wa Serikali, nchi yetu inafanywa kama si nchi, tunashangaa kushitakiwa hapa, tumeletwa kuonewa tu, sisi watuhumiwa tu, tumeshaonewa sana, hasa mimi nimechoka kuonewa," alisema Sheikh Faridi.

Alisema kama hakimu atataka kujua kila mshitakiwa ana jambo gani, wataeleza kwani kila mmoja ana jambo lake la kulalamikia.

Hata hivyo, Jamhuri ikiongozwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Benard Kongola, ilidai hakuna maelekezo yoyote ya kuwakataza ndugu wa washitakiwa kufika gerezani kuwaona.

Hakimu Riwa, alisema ataangalia sheria inasemaje, na kwamba alikuwa anahisi labda wanafanya hivyo kutokana na uzito wa mashitaka yanayowakabili, na upelelezi haujakamilika.

"Mashitaka ya ugaidi hapa nchini ni mapya, nitaenda kusoma zaidi kuangalia inakuwaje," alisema Hakimu Riwa.

Kwa mujibu wa Wakili wa Serikali Mwandamizi, Kongola, Sheikh Faridi na wenzake, inadaiwa kati ya Januari 2013 na Juni 2014 katika maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, walikula njama ya kutenda kosa la kuingiza watu nchini kufanya ugaidi.

Katika shitaka la pili, wanadaiwa katika kipindi hicho walikubaliana kumuingiza Sadick Absaloum na Farah Omary nchini ili kushiriki kutenda makosa ya ugaidi.

Kongola alisema Shitaka la tatu, linamkabili Sheikh Faridi peke yake, ambaye anadaiwa kuwa kati ya Januari 2013 na Juni 2014 maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, huku akijua ni kosa, alimuingiza nchini Sadick na Farah kufanya ugaidi.

"Sheikh Faridi pia anadaiwa kuwahifadhi Sadick na Farah huku akijua watu hao walitenda vitendo vya kigaidi," alisema Kongola.

Washitakiwa hawakutakiwa kujibu lolote, kwa kuwa upelelezi haujakamilika na mahakama iliahirisha kesi hadi Agosti 21, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Washitakiwa wengine katika kesi hiyo, ni Jamal Swalehe, Nassoro Abdallah, Hassan Suleiman, Anthari Ahmed, Mohammed Yusuph, Abdallah Hassani, Hussein Ally na Juma Juma.

Wengine ni Saidi Ally, Hamisi Salum, Saidi Amour Salum, Abubakar Mngodo, Salum Ali Salum, Salum Amour Salum, Alawi Amir, Rashid Nyange, Amir Hamis Juma, Kassim Nassoro na Said Sharifu.


Chanzo:
Mtanzania


 
Asubiri katiba ya CCM itamapa jibu kamili wapo wanaiandaa kwa huko Dodoma
 
Mkuu siyo hivyo. Wazanzibari wanajaribu kwenda kwa mujibu wa sheria. Nadhani wamegundua kwamba Mahakama za chini siyo swala la Muungano hivyo kama Mzanzibari akashitakiwe Zanzibar anakotokea.

Naomba nipewe elimu juu ya mashitaka haya ya kigaidi!! Je? Unaweza kushtakiwa nvhi yeyote tu? Au vipi?
 
Ni kwa sababu anajua kule Zanzibar watamwachia huru licha ya kuingiza watu wa kufanya Ugaidi Zanzibar
 
Gaidi ni gaidi tu, kwani wakati anaua watu aliwauliza kama wanatokea Tanganyika au Zanzibar?. Asurubiwe kabisa huyu gaidi mwenye asili ya kiarabu. Aende kwao uarabuni aue waarabu wenzake na siyo huku
Nakubaliana na wewe moja na sifuri mbili
 
Nakumbuka mtu aliyerioua ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, Mohamed Gailani alihukumiwa Marekani na anatumikia kifungo huko ama Gwantanamo Bay. Makosa ya kigaidi hayana mipaka
Exactly, Gaidi hana haki
 
Ni kweli zanzibar ina mahakama kuu na swala la mahakama sio la muungano,sema huyu ni kati ya wale wanaotaka serikali3 na kule zanzibar sio mtu mdogo anawafuasi wengi na pia ni mtu wa msimamo kama shekhe ponda

Swala la kuunganishwa kwenye kesi ya ugaidi hilo naiachia mahakama ya Tanganyika,kama inamamlaka ya kumshitaki mzanzibar bs kila la kheri
 
Nakumbuka mtu aliyerioua ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, Mohamed Gailani alihukumiwa Marekani na anatumikia kifungo huko ama Gwantanamo Bay. Makosa ya kigaidi hayana mipaka

Umewahi kutafakari kwanini afungiwe Gwantanamo Bay na siyo jela ndani ya Marekani?
 
Mkuu huyu ni Mtanzania aliyezaliwa Zanzbar i.e ni Mzanzibari.
Gaidi ni gaidi tu, kwani wakati anaua watu aliwauliza kama wanatokea Tanganyika au Zanzibar?. Asurubiwe kabisa huyu gaidi mwenye asili ya kiarabu. Aende kwao uarabuni aue waarabu wenzake na siyo huku
 
Gaidi ni gaidi tu, kwani wakati anaua watu aliwauliza kama wanatokea Tanganyika au Zanzibar?. Asurubiwe kabisa huyu gaidi mwenye asili ya kiarabu. Aende kwao uarabuni aue waarabu wenzake na siyo huku
Wewe ni mbaguzi.kwani wewe kama unaijua asili yako,twambie unatokea katika misitu ya congo au zaire. Usije na jawabu kuwa unatokea Tangayika! Eneo lijulikanalo kama Tanganyika lilikuwa ni pori la wanyama mwitu watupu kama mlikuja kuwindaa afu wazee wenu wengine wakarejea na wengine wakaingia mitini.
 
Nakumbuka mtu aliyerioua ubalozi wa Marekani nchini Tanzania, Mohamed Gailani alihukumiwa Marekani na anatumikia kifungo huko ama Gwantanamo Bay. Makosa ya kigaidi hayana mipaka
Ni kweli mkuu kama ambavyo na ugaidi haunaga mipaka wanalipua angani baharini na nchi kavu na wahanga wa vitendo vya kigaidi ni watu wa mataifa yote.
 
Back
Top Bottom