Sheikh Fareed wa Uamsho apatikana akiwa yu hai na mwenye afya tele

salmar

JF-Expert Member
Oct 13, 2012
799
362
Khabari za uhakika nilizozipata sasa hivi ni kuwa Sheikh Fareed asharudi na yu mzima wa afya.

Nitazidi kukujuzeni
560577_456861214364390_1116322220_n.jpg

Ni kweli huyu hapa akiingia nyumbani kwake usiku huu.
attachment.php

208144_298347866931976_467880593_n.jpg

564096_10151057774871176_462766337_n.jpg

Hapa ameingia ndani akifurahia na wanae baada ya kuonekana usiku huu.
MKASA MZIMA WA KUTEKWA KWA SHEIKH FARIDI HUU HAPA

Amesema kuwa waliomchukuwa walijitambulisha kwake kuwa ni askari polisi na kumonesha vitambulisho huku wengine wawili wakiwa na silaha za mshingani hapo hapo wakamfunga macho yake kwa kutum...ia kitambaa ili asijue wapi anapelekwa walimchukua kwa gari na baadae kumuingiza katika nyumba asioijua kwa mahojiano bila ya kumfungua kitambaa hicho kwa muda ...
wa siku tatu mfululizo.

Amesema kuwa watu hao waliomuhoji maswala mengi sana kuhusu tangu kuuanzishwa kwa jumuia ya uamsho na safari zake za kwenda omani na mpaka kumchukulia simu yake bila ya kumrejeshea pia wametaka kujua kuwa anauhusiano gani na rais shein na makamo wakwanza wa raisi maalim seif, wakati wanamuhoji walifika mpaka kupiga risasi chini ya miguu nyake ili kumtisha na kuweza kufikia lengo lao walilojipangia.

Amesema pia watu waliomchukuwa na baadhi ya waliokuwa wanamlinda hawezi kuwajua kutokana na kuwa walikuwa wamevaa soksi ndani ya nyuso zao nakubakisha macho tu,amsema kutokana tu na lafdhi zao ambazo walikuwa wanaongea inaonekana wazi kuwa wengi ni kutoka bara na wazanzibari ni kama wawili tu kutokana na sauti zao.

kuhusu suala lakupigiwa simu na mtu asiemjua amesena kuwa wao kama viongozi huwa mara nyingi wamekuwa wakipigiwa simu na watu wasiowajua na wamekuwa wakionanan nao bila ya matatizo hivyo basi kitendo cha kupigiwa simu siku hio na mtu asiemjua hakikumshituwwa kwani nikawaida kwao hususani aliemnigia alijitambulisha kama ni mwanafunzi wake wa mahad lmahfudh

Aidha amesema kuwa muda wote huo wa siku tatu hakuweza kula chochote katika chumba hicho kwani alikuwa hawaamini na badala yake alikuwa anakunywa maji kutoka bomba la mfereji lililokuwa chooni katika chumba hicho pia amesema wakati yupo ndani hakujua lolote linaloendelea huku nje isipokuwa amejua baada ya kutoka nje kwa kuambiwa na kila manaemkuta.

Aidha sheikh farid ameiomba serikali ya mapinduzi ya zanzibar kutumuia sheria na uadilifu kwa rai wake kinyume cha hivo watakuwa wanaimba tu katika nchi amani na utulivu usiokuwepo pia amewataka wazanzibar kuendelea kutetea maslahi ya nchi yao kama kawaida kwani kufanya hivo ni haki yao na yeye amewahakikishi ataendelea kuitetea zanzibar mpaka tone la mwisho la damu yae.

SOURE' UAMSHO FACEBOOK
 

Attachments

  • f1.jpg
    f1.jpg
    22.5 KB · Views: 11,485
  • f2.jpg
    f2.jpg
    21.4 KB · Views: 5,692
Kuna post ililetwa hapa dk 20 zilizopita ikisema kakutwa kadanja. Tumuamini nani sasa????
 
Hapana yupo hai na hivi sasa watu wajazana kwao malindi znzibar mji umeripuka kwa furaha na nderemo
 
yakhe shekhe Farid nakwenda kula bata nyumba ndogo; natuharibia siku yetu buree! nani nateka yeye kwa lipi haswa? Hii uamsho fitna tupu, mara gari napigwa risasi mara natekwa; wallwah subiri jumaa wazua baalaa nyingine
 
Hao UAMSHO walimficha ili wapate kisingizio cha kufanya ghasia, na baadae wakaipa serikali masaa 26 sheikh apatikane, wakati ukweli walipanga (UAMSHO) kumuachia sheikh ndani ya hayo masaa 26 waliyoipa serikali na hivyo kuonesha kama serikali imesalimu amri!

Usanii mtupu!
 
Back
Top Bottom