Shehena ya tumbaku hatarini kukosa wanunuzi Tabora

Shehena ya tumbaku hatarini kukosa wanunuzi Tabora

FikraPevu

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2010
Posts
304
Reaction score
236
Ili kuwanusuru wakulima wa tumbaku na hasara wanayoweza kuipata ya kukosa soko, serikali imeanzisha majadiliano na nchi nne za India, Misri, China na Iran ambazo zimeonyesha nia ya kununua shehena hiyo ya tumbaku.

Akizungumza katika kikao cha tisa cha Bunge la Tanzania, Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa amesema katika msimu 2016/2017 wakulima wamelima tumbaku nyingi kinyume na makubaliano na wanunuzi. Amewata wakulima kuwa wavumilivu wakati serikali inaendelea na jitihada za kuwatafutia wakulima hao soko la uhakika katika nchi mbalimbali duniani.

“Kwa kawaida wakulima huingia kwenye makubaliano na wanunuzi kulingana na kiwango cha tambuku kinachotakiwa kuuzwa lakini mwaka huu inaelekea kuna mavuno mengi matokeo yake bado shehena kubwa iko ghalani”, amesema Waziri Mkuu.

Kulingana na maelezo ya Waziri Mkuu, mpaka sasa nchi ya India imeonyesha muitikio mzuri na timu ya wataalamu wa Tanzania inafanya mazungumzo na wanunuzi juu ya bei. Serikali inataka wakulima wafaidike na bei nzuri ili kuboresha maisha yao na kuongeza Pato la Taifa.

Bei elekezi ya tambaku kwa msimu huu 2016/2017 ni kati ya shilingi 4,400 na 4,500 kwa kilo ambapo serikali imeziagiza kampuni za ndani kununua tambuku kwa shilingi ya Tanzania ili kuwawezesha wakulima kufaidika na zao hilo.

Wadau na wanaharakati wameitaka serikali kutafuta suluhisho la kudumu la tumbaku nchini. Njia mojawapo ni kukaa na wakulima hao ili kuwatafutia zao mbadala ili kuwaepusha na madhara ya tumbaku kwa afya zao na kuzuia uharibifu wa mazingira.

Kwa upande wao, Chama Cha Wakulima wa Tumbaku Duniani (ITGA) kimeitaka serikali ya Tanzania kufungua milango ya majadiliano ili kuwawezesha wakulima kulima mazao mbadala ikizingatiwa kuwa tumbaku inakabiliwa na changamoto mbalimbali.

Rais wa wa chama hicho cha ITGA, Daniel Green amesema tumbaku ina mchango mkubwa katika uchumi wa nchi kwasababu inazalisha ajira na kutengeneza kipato. Amezitaka serikali za nchi zinazolima zao hilo kuwatafutia wakulima zao mbadala kabla ya kuwazuia kuzalisha tumbaku.

“Hatupingani na sera zinazolinda afya ya jamii, jambo moja ni kuwa tumekuwa tukiomba tuwe sehemu ya mchakato ambao utawasaidia wakulima wa tumbaku kuwa na mstakabali mzuri”, amesema Green.

Zaidi, soma hapa => Wakulima wa tumbaku hatarini kukosa soko, mahitaji ya zao hilo yapungua duniani | FikraPevu
 
Mkuu hii habari n ya lini? Nasikia masoko yameanza leo tarehe 23 October 2017....
Na bei za kununua tumbaku iliyo baki zimeshatangazwa tayari.
Mm n mkulima wa tumbaku toka nimezaliwa nimekuta home wanalima tumbaku, nimesomeshwa na hela za tumbaku na nimebahatika kupata kazi japo kilimo cha tumbaku sijakiacha bado...
Kiukweli wakulima wa tumbaku wamesahaulika sana, japo tumbaku n zao linalo ingizia fedha za kigeni nyingi sana kwa Tanzania na kodi kubwa sana.
Swala la kuuza tumbaku kwa Tsh badala ya dola, sidhan kama wanawasaidia wakulima, apo naona serikali inawanyima hela CRDB ambao ndo walikua wanajipangia Exchange rate na kupata faida ya ile difference (spread).
IMG-20171122-WA0013.jpg
 
Mimi nadhani aliyetoa taarifa amejikita mahitaji ya dunia ndio maana serikali imewatafutia soko la nje wakulima kwa sababu wanunuzi was ndani wamenunua lkn bado tumbaku IPO.

Wakulima wamezalisha sana msimu huu.
 
Bora wabadili zao tu jamani..hivi hili zao halilipi kweli??????

when-and-how-to-harvest-marijuana-plants-35639-w800.jpg
 
Back
Top Bottom