Shehena ya mafuta ya Taa na dawa za kulevya yakamatwa mpakani mwa Kenya na Tanzania

Donatila

JF-Expert Member
Oct 23, 2014
7,735
22,433
Shehena ya bidhaa aina ya mafuta ya Taa na dawa za kulevya kilo 98 zilizokuwa zikiingizwa nchini kwa njia za panya kutoka nchini Kenya zimekamatwa katika mapori yanayounganisha mpaka wa nchi jirani, katika operesheni maalum inayofanywa katika vijiji tofauti vilivyopo mpakani ikiwa ni sehemu ya kukabiliana na mtandao wa kihalifu unaojihusiosha na uingizaji wa dawa za kulevya, wahamiaji haramu na ukwepeji wa kodi kwa serikali.

Wakizungumza katika eneo la Horohoro mpakani mwa Kenya na Tanzania timu ya watendaji wa mamlaka ya mapato nchini (TRA), maafisa uhamiaji na wakaguzi wa mamlaka ya chakula na dawa nchini tawi la Horohoro, wamesema lengo la operesheni hiyo ni kuhakikisha kuwa mipaka ya nchi inakuwa salama kufuatia kubainika kuwepo kwa mtandao wa ukwepaji kodi, kupitisha wahamiaji haramu na vikundi vya uhalifu.

Kuhusu kukamatwa kwa dawa za kulevya mratibu mwandamizi msaidizi wa idara ya uhamiaji nchini tawi la Horohoro Mwesiga Lubalila amesema katika zoezi la kukabiliana na uingizaji wa bidhaa haramu, kundi la watu waliokuwa na pikipiki zilizokuwa zimebeba maboksi walipobaini mtego wa kukamatwa walilazimika kuzitupa pikipiki hizo na kisha kukimbia ndipo walipopekua na kukuta dawa za kulevya aina ya Mirungi kilo zenye uzito wa kilo 98 iliyokuwa imefungwa katika vifurushi vyenye uzito wa kilo mojamoja kila kimoja.

Kufuatia hatua hiyo mkaguzi mkuu wa mamlaka ya chakula na dawa Bwana Thomas Nkondola amesema bidhaa zote zinazoingizwa kutoka nchini Kenya hazitaruhusiwa kuingia endapo kama hazijafanyiwa ukaguzi kufuatia baadhi ya wafanyabiashara kuingiza bidhaa zilizopitwa muda wake na hivyo kuhatarisha afya za watumiaji
 
na kukuta dawa za kulevya aina ya Mirungi kilo zenye uzito wa kilo 98 iliyokuwa imefungwa katika vifurushi vyenye uzito wa kilo mojamoja kila kimoja.

i

Acha hizo! Shehena iko wapi ya kubebwa na pikipiki?
Kumbe ni mafuta ya KOROBOI na misokoto ya mirungi ambayo imeHALALISHWA nchini UGANDA.

MOD utazame uzi huu
 
Acha hizo! Shehena iko wapi ya kubebwa na pikipiki?
Kumbe ni mafuta ya KOROBOI na misokoto ya mirungi ambayo imeHALALISHWA nchini UGANDA.

MOD utazame uzi huu
Mafuta ya Taa Kenya nibei rahisi kuliko Tanzania sababu tu EWURA wali-declare kua walishindwa kuwakamata wale wanaochakachua (changanya) Mafuta ya Taa na Petrol. Hapo mwanzo serikali kwa kujua kua mafuta ya taa yanatumika na watu wa kipato cha chini vijijini pamoja na ku-discourage matumizi ya kuni na Mkaa waliamua kutoza kodi ndogo tu ya Tshs 54/= kwa kila lita huku Diesel na Petrol zikitozwa Tshs 500/= kila moja.

Sasa basi, mafuta ya Taa yalikua yakiuzwa kwa bei pungufu ya Tshs 450/= mpaka Tshs 500/= kwa lita 1 compare to Diesel au Petrol. Wachakachuaji waliyanunua haya mafuta ya Taa kwa wingi yakiwa na bei ndogo wakawa wanayachaganya na petrol na kuuza kwa bei ya Petrol.

Sasa basi EWURA kwa kuona kua hawawezi kuwakamata hawa wachakachuaji wakaamua na Mafuta ya taa nayo kuyapandisha kodi from Tshs 54/= mpaka Tshs 450/= karibu na Petrol au Diesel. Wakati hili likifanyika huku kwetu, Kenya wao waliamua kubaki na kodi ileile ndogo kwa Mafuta ya Taa, sababu zikiwa ni zilezile kua haya yanatumiwa na wanachi wa vijijini wenye vipato vidogo.

Mwisho wasiku ndio hivyo, Kenya Bei ya mafuta ya taa iko chini kuliko huku kwetu, na kwa lita moja unaweza kupata mpaka faida ya tshs 500/= ambayo TRA na EWURA wameamua kuiweka kwa huku kwetu.
 
Madawa ya kulevya yanapita Dar es salaam airport tena kwa escort kubwa mkuu hayo mpaka wa hololo yatakua yale majani tuu...
 
Fateni wanaoingiza madawa kupitia mpaka wenu na sisi Kenya lakini tafadhali wacheni majani kitu cha malawi,vijana wanaitaka kwa sana huku Kenya.
 
Back
Top Bottom