Shehena ya mafuta ya Taa kutoka nchini Kenya yakamatwa wilayani Mkinga


Ghazwat

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Messages
17,668
Likes
51,824
Points
280
Ghazwat

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2015
17,668 51,824 280
78eed44233ad67720a9f8616294c6bd1.jpg
Kamati ya ulinzi na usalama wilayani Mkinga imekamata shehena ya mafuta ya Taa kutoka nchi jirani ya Kenya yaliyoingizwa nchini bila kulipiwa ushuru kwa madai kuwa baadhi ya wafanyabiashara hulazimika kupitisha bidhaa hiyo kwa njia za panya kisha kuingizwa nchini kinyume cha sheria madai kuwa mafuta hayo huuzwa kwa bei rahisi nchini Kenya baada ya Serikali ya Tanzania kupandisha bei

Wakizungumza wakati kamati hiyo hiyo iliyoongozwa na mwenyekiti wa Kamati ya ulinzi na usalama wilayani Mkinga Mark Yona kufanya operesheni katika kijiji cha Jesini kilichopo jirani na Kenya. Afisa Uhamiaji wa wilaya pamoja na mkuu wa kikosi maalumu cha kuzuia magendo katika eneo la Moa lililopo mpakani mwa nchi hizo mbili, wamesema mafuta ya Taa yamekuwa yakiingizwa kwa wingi hasa baada ya Serikali ya Tanzania kupandisha bei ya bidhaa hiyo.

Katika zoezi hilo la kuhakikisha sheria za nchi zinaimarishwa, Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilayani Mkinga Mark Yona amesema katika kipindi cha miezi mitatu wamekamata magunia ya mkaa 325 huku miti aina ya mikoko 1500 iliyokuwa ikisafirishwa nchini Kenya baada ya baadhi ya wafanyabiashara kumaliza miti hiyo katika fukwe za bahari ya hindi nchini Kenya na kuanza kuingilia ya hapa nchini.

Kufuatia hatua hiyo meneja wa Wakala wa misitu wilayani Mkinga Frank Chambo ameshukuru kwa operesheni inayoendeshwa na vyombo vya ulinzi na usalama wilayani Mkinga katika kukabiliana na uharibifu wa mazingira unaofanywa na baadhi ya raia wa Kenya kwa kuvuna mikarambati na mikoko na kusafirishwa nchi jirani ya Kenya kwa sababu wao wanakabiliwa na changamoto ya kukosekana kwa usafiri wa majini ili kudhibiti tatizo hilo.
 
kisu cha ngariba

kisu cha ngariba

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2016
Messages
22,204
Likes
47,989
Points
280
kisu cha ngariba

kisu cha ngariba

JF-Expert Member
Joined Jun 21, 2016
22,204 47,989 280
Nashauri serikali wayachome moto.
 
chaliifrancisco

chaliifrancisco

JF-Expert Member
Joined
Jan 17, 2015
Messages
7,707
Likes
13,923
Points
280
Age
25
chaliifrancisco

chaliifrancisco

JF-Expert Member
Joined Jan 17, 2015
7,707 13,923 280
Tuendeleze ujinga.. Na kujenga uadui
 
Sosthenes Maendeleo

Sosthenes Maendeleo

Verified Member
Joined
Oct 24, 2012
Messages
2,264
Likes
855
Points
280
Sosthenes Maendeleo

Sosthenes Maendeleo

Verified Member
Joined Oct 24, 2012
2,264 855 280
Wapige mnada
 
Bilionea Asigwa

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2011
Messages
15,995
Likes
22,575
Points
280
Bilionea Asigwa

Bilionea Asigwa

JF-Expert Member
Joined Sep 21, 2011
15,995 22,575 280
Wawapelekee wanafunzi wa Iliboru pale wakaweke kwenye maharage ya skuli....
Badala ya kuyapiga kiberiti
 
K

kindikwili

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2016
Messages
1,698
Likes
2,477
Points
280
K

kindikwili

JF-Expert Member
Joined Oct 5, 2016
1,698 2,477 280
Wawapelekee wanafunzi wa Iliboru pale wakaweke kwenye maharage ya skuli....
Badala ya kuyapiga kiberiti
Dah! Aisee umenikumbusha mbali sana, wakati Kitemango akiwa mkuu wa shule maharage yalikuwa yanamwagiwa mafuta nadhani pipa nzima. Hivi yale mafuta hayajawa na madhara kwa wengine? Maana kwangu nahisi yameniathiri sana.
 
W

Wajad

JF-Expert Member
Joined
Jul 20, 2012
Messages
1,327
Likes
419
Points
180
W

Wajad

JF-Expert Member
Joined Jul 20, 2012
1,327 419 180
Nimesoma sijaelewa hata kidogo, wamekamata mafuta yakiwa kwenye baiskeli, bodaboda, gari au kwenye trekta?
Eti wanayaita shehena, nilidhani ni meli nzima kumbe picha hapo inaonyesha madumu kama 10 ya lita20 ambayo yanabebwa na pikipiki 2 tu!
 
Ghazwat

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2015
Messages
17,668
Likes
51,824
Points
280
Ghazwat

Ghazwat

JF-Expert Member
Joined Oct 4, 2015
17,668 51,824 280
Eti wanayaita shehena, nilidhani ni meli nzima kumbe picha hapo inaonyesha madumu kama 10 ya lita20 ambayo yanabebwa na pikipiki 2 tu!
Acha sifa wewe. Pikipiki gani ya kubeba madumu hayo, halafu unasema kama 10 kwani unahesabu namna gani?
 

Forum statistics

Threads 1,237,921
Members 475,774
Posts 29,306,478