Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 74,901
- 155,970
Shehe Yahya anaangaliaga sana mwenendo wa mambo, ni kama vile anabip, sasa ikatokea akapigiwa kwake ni ujiko.atatoka kwasababu hana kosa au kwasababu ya nguvu za giza?
Babu Seya (kulia) akiwaaga watu waliofurika mahakamani kusikiliza kesi yao. Kushoto ni mwanaye Papii Kocha (Mtoto wa Mfalme).
MTABIRI maarufu Afrika Mashariki, Sheikh Yahya Hussein, amesema mwanamuziki maarufu, Nguza Vicking (Baby Seya) atatoka gerezani, kitu ambacho ni habari njema kwa wapenzi wa muziki nchini....
Akizungumza na gazeti hili ofisini kwake Magomeni jijini Dar es Salaam, Sheikh Yahya alisema alituma ujumbe ulioongozwa na Bw. Hassani Yahya siku ya Jumamosi iliyopita kwenda kumuona Babu Seya gerezani Ukonga na amemuambia mwanamuziki huyo kuwa avute subira kwani elimu ya nambari (Numerology) inaonesha kuwa atatoka gerezani.
Miaka ya nyuma nilitabiri kuwa Nguza atatoka gerezani Februari lakini kumbe kuna Nguza wawili sasa mmoja ametoka pamoja na mdogo wake, sasa bado nasema waliobaki watatoka, alisema Sheikh Yahya.
Alisema alipotabiri kwa waandishi wa habari na kupitia kituo cha televisheni cha Channel Ten kuwa Nguza atatoka Februari wakati ule watu wengi walipuuza lakini sasa imekuwa hivyo.
Mi nashindwa kuelewa sisi waTZ tuna matatizo gani. Yaani eti ni 'habari njema kwa wapenzi wa muziki"
mahakama ya juu kabisa imemwona ana hatia.....sasa hili la kwamba watu wanammiss mtu aliyekuhukiwa kwa kosa la ubakaji linatoka wapi?
Mbona watu hawawazungumzii wale watoto 11 waliotendewa unyama na huyu bwana?
Au ndo biashara?
Mkuu uko right kwamba kuna watu walifungwa kimakosa... na kesi hii ina utata sana, lakini nadhani pia tuwe makini kidogo, kama babu seya akitoka, basi iwe ni kwasababu ya haki yake na siyo eti kwasababu wapenzi wa muziki watafurahi..Kumbuka kuna watoto 2 walifungwa miaka 6 KIMAKOSA
MWALIMU/dalali hakufungwa na mapaka leo haijuliani ............
Hii kesi imekaa kiutata sana na ndio maana imevuta hisia za watu.
Huyu mtabiri ni wa CCM achaneni naye.
na ndio maana Jana Wakili Mabere Marando akihojiwa TBS Tv alisema kuwa, amewaomba mawakili wenzake wasome hukumu yote , kisha wamsaidie kuona kama kuna hoja ya kuomba usikilizwaji upya wa kesi hiyo pale mahakama ya rufaa, ambapo kisheria majaji saba wanaweza kukaa na kuipitia upya kwa mujibu wa sheria za JMT.Kumbuka kuna watoto 2 walifungwa miaka 6 KIMAKOSA
MWALIMU/dalali hakufungwa na mapaka leo haijuliani ............
Hii kesi imekaa kiutata sana na ndio maana imevuta hisia za watu.
Mkuu uko right kwamba kuna watu walifungwa kimakosa... na kesi hii ina utata sana, lakini nadhani pia tuwe makini kidogo, kama babu seya akitoka, basi iwe ni kwasababu ya haki yake na siyo eti kwasababu wapenzi wa muziki watafurahi..
tukumbuke kwamba kuna sheria na wasifu wa nguza, ambavyo ni vitu viwili tofauti
kwakweli mimi shikh yahya ananisikitisha sana, na wanaonisikitisha zaidi ni wale wanaopromote hayo mambo kwenye media
Sawa mkuu kama watu wanafungwa kimakosa ina maana kesi ilisikilizwa kimakosa inatakiwa irudiwe upya kusikilizwa kisahihi kwenye mahakama ya rufaa. Imagine wewe ungefungwa kwa miaka 6 kimakosa na umri wa miaka 18 au hata zaidi.
Francis tu ndio alikuwa mtoto..huyo mwingine sijui Mbangu ana utoto gani ilhali sasa ana zaidi ya miaka 30?Kumbuka kuna watoto 2 walifungwa miaka 6 KIMAKOSA
MWALIMU/dalali hakufungwa na mapaka leo haijuliani ............
Hii kesi imekaa kiutata sana na ndio maana imevuta hisia za watu.
Huyu mtabiri ni wa CCM achaneni naye.