Shehe Yahya Husein awatabaria kina Nguza kuachiliwa

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,706
155,198

Babu Seya (kulia) akiwaaga watu waliofurika mahakamani kusikiliza kesi yao. Kushoto ni mwanaye Papii Kocha (Mtoto wa Mfalme).

MTABIRI maarufu Afrika Mashariki, Sheikh Yahya Hussein, amesema mwanamuziki maarufu, Nguza Vicking (Baby Seya) atatoka gerezani, kitu ambacho ni habari njema kwa wapenzi wa muziki nchini....
Akizungumza na gazeti hili ofisini kwake Magomeni jijini Dar es Salaam, Sheikh Yahya alisema alituma ujumbe ulioongozwa na Bw. Hassani Yahya siku ya Jumamosi iliyopita kwenda kumuona Babu Seya gerezani Ukonga na amemuambia mwanamuziki huyo kuwa avute subira kwani elimu ya nambari (Numerology) inaonesha kuwa atatoka gerezani.

“Miaka ya nyuma nilitabiri kuwa Nguza atatoka gerezani Februari lakini kumbe kuna Nguza wawili sasa mmoja ametoka pamoja na mdogo wake, sasa bado nasema waliobaki watatoka,” alisema Sheikh Yahya.
Alisema alipotabiri kwa waandishi wa habari na kupitia kituo cha televisheni cha Channel Ten kuwa Nguza atatoka Februari wakati ule watu wengi walipuuza lakini sasa imekuwa hivyo.
 
atatoka kwasababu hana kosa au kwasababu ya nguvu za giza?
 
Shehe Yahya anaangaliaga sana mwenendo wa mambo, ni kama vile anabip, sasa ikatokea akapigiwa kwake ni ujiko.
kifupi ni msanii, anaekula kwa gharama za ujinga ...shehe Video bana, unatuboa tu,
 
Mi nashindwa kuelewa sisi waTZ tuna matatizo gani. Yaani eti ni 'habari njema kwa wapenzi wa muziki"

mahakama ya juu kabisa imemwona ana hatia.....sasa hili la kwamba watu wanammiss mtu aliyehukukiwa kwa kosa la ubakaji linatoka wapi?

Mbona watu hawawazungumzii wale watoto 11 waliotendewa unyama na huyu bwana?

Au ndo biashara?
 
Babu Seya (kulia) akiwaaga watu waliofurika mahakamani kusikiliza kesi yao. Kushoto ni mwanaye Papii Kocha (Mtoto wa Mfalme).

MTABIRI maarufu Afrika Mashariki, Sheikh Yahya Hussein, amesema mwanamuziki maarufu, Nguza Vicking (Baby Seya) atatoka gerezani, kitu ambacho ni habari njema kwa wapenzi wa muziki nchini....
Akizungumza na gazeti hili ofisini kwake Magomeni jijini Dar es Salaam, Sheikh Yahya alisema alituma ujumbe ulioongozwa na Bw. Hassani Yahya siku ya Jumamosi iliyopita kwenda kumuona Babu Seya gerezani Ukonga na amemuambia mwanamuziki huyo kuwa avute subira kwani elimu ya nambari (Numerology) inaonesha kuwa atatoka gerezani.

“Miaka ya nyuma nilitabiri kuwa Nguza atatoka gerezani Februari lakini kumbe kuna Nguza wawili sasa mmoja ametoka pamoja na mdogo wake, sasa bado nasema waliobaki watatoka,” alisema Sheikh Yahya.
Alisema alipotabiri kwa waandishi wa habari na kupitia kituo cha televisheni cha Channel Ten kuwa Nguza atatoka Februari wakati ule watu wengi walipuuza lakini sasa imekuwa hivyo.

Asitake kutwambia kuwa 'hakujua kuna nguza wawili.,..mtabiri gani anakuwa na 'kumbe kumbe' hizi?
 
Mi nashindwa kuelewa sisi waTZ tuna matatizo gani. Yaani eti ni 'habari njema kwa wapenzi wa muziki"

mahakama ya juu kabisa imemwona ana hatia.....sasa hili la kwamba watu wanammiss mtu aliyekuhukiwa kwa kosa la ubakaji linatoka wapi?

Mbona watu hawawazungumzii wale watoto 11 waliotendewa unyama na huyu bwana?

Au ndo biashara?

Kumbuka kuna watoto 2 walifungwa miaka 6 KIMAKOSA
icon5.gif
icon5.gif
icon5.gif
icon5.gif

MWALIMU/dalali hakufungwa na mapaka leo haijuliani ............
Hii kesi imekaa kiutata sana na ndio maana imevuta hisia za watu.

Huyu mtabiri ni wa CCM achaneni naye.
 
Mkuu uko right kwamba kuna watu walifungwa kimakosa... na kesi hii ina utata sana, lakini nadhani pia tuwe makini kidogo, kama babu seya akitoka, basi iwe ni kwasababu ya haki yake na siyo eti kwasababu wapenzi wa muziki watafurahi..

tukumbuke kwamba kuna sheria na wasifu wa nguza, ambavyo ni vitu viwili tofauti

kwakweli mimi shikh yahya ananisikitisha sana, na wanaonisikitisha zaidi ni wale wanaopromote hayo mambo kwenye media
 
na ndio maana Jana Wakili Mabere Marando akihojiwa TBS Tv alisema kuwa, amewaomba mawakili wenzake wasome hukumu yote , kisha wamsaidie kuona kama kuna hoja ya kuomba usikilizwaji upya wa kesi hiyo pale mahakama ya rufaa, ambapo kisheria majaji saba wanaweza kukaa na kuipitia upya kwa mujibu wa sheria za JMT.
KIMSINGI mARANDU ANAINYESHA MASHAKA MAKUBWA, ILA ANASITA KUINGIA KICHWA KICHWA, NDO MAANA KAOMBA wenzake wamsaidie jambo hilo....maana ndani ya siku 60 unaruhusiwa kisheria kuomba hearing.
Bado swala la Nguza na watoto wake litawaumiza watu wengi kichwa , kwa muda mrefu.
 
Mkuu uko right kwamba kuna watu walifungwa kimakosa... na kesi hii ina utata sana, lakini nadhani pia tuwe makini kidogo, kama babu seya akitoka, basi iwe ni kwasababu ya haki yake na siyo eti kwasababu wapenzi wa muziki watafurahi..

tukumbuke kwamba kuna sheria na wasifu wa nguza, ambavyo ni vitu viwili tofauti

kwakweli mimi shikh yahya ananisikitisha sana, na wanaonisikitisha zaidi ni wale wanaopromote hayo mambo kwenye media

Sawa mkuu kama watu wanafungwa kimakosa ina maana kesi ilisikilizwa kimakosa inatakiwa irudiwe upya kusikilizwa kisahihi kwenye mahakama ya rufaa. Imagine wewe ungefungwa kwa miaka 6 kimakosa na umri wa miaka 18 au hata zaidi.
 
Ha ha ha!:rolleyes: "Lakini kumbe kuna Nguza wawili" kazi kubwa! We-weeeeeee ndio utabiri huo! ndio kashtuka leo kuna Nguza wawili! Biashara matangazo...
 
Kama atatoka, aseme atatoka lini, sio mambo ya blah blah hapa! Huyu Sheikh ni wa kupiga bakora sasa, maana anatishia hata watu vifo kama watagombea dhidi ya JK!
 
Sawa mkuu kama watu wanafungwa kimakosa ina maana kesi ilisikilizwa kimakosa inatakiwa irudiwe upya kusikilizwa kisahihi kwenye mahakama ya rufaa. Imagine wewe ungefungwa kwa miaka 6 kimakosa na umri wa miaka 18 au hata zaidi.

mkuu,, mbona nimemsikia Marando akiwa amekaririwa na vyombo vya habari akiwaaasa wale walioachiwa huru 'wasithubutu kudai fidia' serikalini kwa hofu kuwa 'wakipoteza' hiyo rufaa itakuwa mbaya sana kwao? kuna kitu gani alichokiona wakili Maarufu Marando?

nadhani tuzipe benefit of doubt mahakama zetu pamoja na majaji. Si nasikia walikaa majaji saba au? na kwamba ndio mwisho? kama na hawa walimwona babu seya na manaye wana makosa, inakuwaje bado tunakuwa na wasi wasi hivi? na labda tuwe na namna yetu ya kushughulikia kesi I mean tuachane na mfumo wetu wa sheria iwe ni 'mob justice' tu au vipi
 
Kumbuka kuna watoto 2 walifungwa miaka 6 KIMAKOSA
icon5.gif
icon5.gif
icon5.gif
icon5.gif

MWALIMU/dalali hakufungwa na mapaka leo haijuliani ............
Hii kesi imekaa kiutata sana na ndio maana imevuta hisia za watu.

Huyu mtabiri ni wa CCM achaneni naye.
Francis tu ndio alikuwa mtoto..huyo mwingine sijui Mbangu ana utoto gani ilhali sasa ana zaidi ya miaka 30?
 
si wameishaachiliwa?????????????????/ kwani wale wawili walioachiliwa siku ile si akina nguza????????????????/////
 
bwana Kaizer, kumbuka kuna yule mwalimu a.k.a dalali ambaye ndio alikuwa anawapeleka wale watoto kwa babu seya kwenda kubakwa;swali je,unahisi yupo jela? au unahisi kuwa yule mwalimu hana hatia ndio maana hajafungwa au kusikia kesi yake mahala popote pale? huoni hii kesi ina utata kwa mwalimu kutokufungwa maisha naye pia? acha ushabiki..hii kesi ina walakini! kuna mtu ana interest yake hapo! either bifu au mambo ya kunyang'anyana mademu (vimada na waheshimiwa)
 
Back
Top Bottom