UVCCM jifunzeni kuwa na akiba ya maneno, tujikumbushe hapa

666 chata

JF-Expert Member
Mar 14, 2013
1,474
2,000
TAARIFA YA UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM) KWA VYOMBO VYA HABARI.
_______________
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jana Agosti 29 kimezindua kampeni zake katika viwanja vya Jangwani Jijini Dar es Salaam. Katika uzinduzi huo viongozi kadhaa wa Chama hicho walihudhuria, wakiwemo Waziri Mkuu mstaafu Fredrick Sumaye, Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Ufisadi, Edward Lowassa pamoja na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Lawrance Masha ambao walihutubia mkutano huo wa ufunguzi.

Ni jambo la kushangaza kumsikia mgombea wa nafasi ya Urais kupitia CHADEMA, Edward Lowassa akihemewa na Kujikuta akishindwa kuikabili hadhira ya Watanzania wanaofikia milioni 45 kuwaelezea ana malengo gani ya urais, Chama chake kina dira na sera zipi za msingi, pia akizungumza bila kuonyesha mtiririko wa sera kupitia ilani ya Uchaguzi ya chama hicho.

Mgombea wa CHADEMA Lowassa ni dhahiri ameshindwa uchaguzi mkuu mapema, amebakia akilalama, kupiga soga na kujenga matumaini hewa kwa Watanzania huku akishindwa kujua ni changamoto zipi za msingi zinazowakabili wananchi katika maisha ya kila siku.

Lowassa akiwa anatetemeka jukwaani na kuongea kwa taabu amelizungumzia suala ambalo tayari mahakama ya rufaa imekwisha litolea hukumu. Suala hilo ni kesi ya Mwanamuziki Nguza Vicking na mwanawe Johnson Nguza waliohukumiwa kifungo cha maisha jela kwa makosa ya ubakaji.

Mahakama imedhibitisha kuwa Nguza Vicking maarufu kama "Babu Seya" na mwanaye Johnson Nguza maarufu kama "Papii Kocha" ni WABAKAJI, WANAJISI na WALAWITI. Na hivyo wamehukumiwa kifungo cha maisha gerezani kutokana na tabia hizo chafu katika jamii.

Lowassa anakuja na hadithi ya kuwaachia huru, kana kwamba anaona vyombo vya sheria vimewaonea na kuwakandamiza. Ifahamike kati ya makosa ambayo yameainishwa katika sheria za Tanzania, kosa la ubakaji halina msamaha. Mbakaji hawezi kupewa msamaha wa Rais. Msaidieni Lowassa maana anaonekana haijui sheria.

Tangu nchi imepata uhuru, hakuna Rais aliyewahi kutoa msamaha kwa wabakaji, wala walawiti. Lowassa anaonekana kuchanganyikiwa. Ni dhahiri kwamba CHADEMA na mgombea wao Lowassa hawajajipanga kuongoza nchi. Hawana hoja za kuwasaidia watanzania, badala yake wanategemea siasa za matukio ili kujipatia kura. Tunaomba watanzania muwapuuze.

Imetolewa na:

Shaka Hamdu Shaka,
Kaimu Katibu Mkuu - UVCCM Taifa na Mjumbe wa NEC.
30 August 2015.
 
Twamo

JF-Expert Member
May 27, 2017
2,182
2,000
Daaa! Huenda kesho wakaitisha mkutano na waandishi wa habari kulaani msamaha wa rais kwa babu Seya na mwanae! Ila wasivyo na aibu utakuta na wao wanampongeza Mh. Rais kwa msamaha huo! Tanzania bila unafiki haiendi
 
666 chata

JF-Expert Member
Mar 14, 2013
1,474
2,000
Daaa! Huenda kesho wakaitisha mkutano na waandishi wa habari kulaani msamaha wa rais kwa babu Seya na mwanae! Ila wasivyo na aibu utakuta na wao wanampongeza Mh. Rais kwa msamaha huo! Tanzania bla unafiki haiendi
Wee hakuna wa kulaani hapo tena watapongeza vikubwa sanaa na kudai rais kawaskiliza kwa kuwatoa wakina seya.
 
TLE

JF-Expert Member
Oct 14, 2016
222
250
Mtoa post hongera sana kwa kutunza kumbukumbu lkn nakulamu kitu kimoja umewahi sana kuitoa hii post ungesubiria kidogo watoe tamko lao lingine juu ya hii kadhia ya Babu sea na mwanae ili tuone undumila kuwili wao,sasa hv wakiona hawawezi kutoa tamko la kumpongeza Mkulu
 
The Bourne

JF-Expert Member
Aug 24, 2017
1,077

Hahahaahhaahahaha mkuu nlikua na usongo nao, wahuni wale.
 
SULEIMAN ABEID

JF-Expert Member
Feb 26, 2013
297
250
WANASEMAGA HIYO NDIYO SIASA YA TZ. HUONI MPAKA SASA WABUNGE WA CCM HAWAJAMUUNGA MKONO JPM KWA KAZI NZURI ANAZOFANYA!? NI WAPINZANI PEKEE NDO WAMEANZA KUMUUNGA MKONO NA SASA WANAJIUZULU UDIWANI NA UBUNGE WAKIMKUBALI MAGUFULI, CCM WAO KIMYAAA! TUNAOMBA WATHAMINI MCHANGO WA RAIS WETU, WAANZE KUJIUZULU SASA.
 
Kapilipoint

JF-Expert Member
Nov 30, 2017
381
500
Wana akili ndogo Mkuu hawawezi kuwa na akiba ya maneno huoni Polepole eti anajua Siasa kuliko mzee Lowassa?
 
Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
26,565
2,000
TAARIFA YA UMOJA WA VIJANA WA CCM (UVCCM) KWA VYOMBO VYA HABARI.
_______________
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) jana Agosti 29 kimezindua kampeni zake katika viwanja vya Jangwani Jijini Dar es Salaam. Katika uzinduzi huo viongozi kadhaa wa Chama hicho walihudhuria, wakiwemo Waziri Mkuu mstaafu Fredrick Sumaye, Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Ufisadi, Edward Lowassa pamoja na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Lawrance Masha ambao walihutubia mkutano huo wa ufunguzi.

Ni jambo la kushangaza kumsikia mgombea wa nafasi ya Urais kupitia CHADEMA, Edward Lowassa akihemewa na Kujikuta akishindwa kuikabili hadhira ya Watanzania wanaofikia milioni 45 kuwaelezea ana malengo gani ya urais, Chama chake kina dira na sera zipi za msingi, pia akizungumza bila kuonyesha mtiririko wa sera kupitia ilani ya Uchaguzi ya chama hicho.

Mgombea wa CHADEMA Lowassa ni dhahiri ameshindwa uchaguzi mkuu mapema, amebakia akilalama, kupiga soga na kujenga matumaini hewa kwa Watanzania huku akishindwa kujua ni changamoto zipi za msingi zinazowakabili wananchi katika maisha ya kila siku.

Lowassa akiwa anatetemeka jukwaani na kuongea kwa taabu amelizungumzia suala ambalo tayari mahakama ya rufaa imekwisha litolea hukumu. Suala hilo ni kesi ya Mwanamuziki Nguza Vicking na mwanawe Johnson Nguza waliohukumiwa kifungo cha maisha jela kwa makosa ya ubakaji.

Mahakama imedhibitisha kuwa Nguza Vicking maarufu kama "Babu Seya" na mwanaye Johnson Nguza maarufu kama "Papii Kocha" ni WABAKAJI, WANAJISI na WALAWITI. Na hivyo wamehukumiwa kifungo cha maisha gerezani kutokana na tabia hizo chafu katika jamii.

Lowassa anakuja na hadithi ya kuwaachia huru, kana kwamba anaona vyombo vya sheria vimewaonea na kuwakandamiza. Ifahamike kati ya makosa ambayo yameainishwa katika sheria za Tanzania, kosa la ubakaji halina msamaha. Mbakaji hawezi kupewa msamaha wa Rais. Msaidieni Lowassa maana anaonekana haijui sheria.

Tangu nchi imepata uhuru, hakuna Rais aliyewahi kutoa msamaha kwa wabakaji, wala walawiti. Lowassa anaonekana kuchanganyikiwa. Ni dhahiri kwamba CHADEMA na mgombea wao Lowassa hawajajipanga kuongoza nchi. Hawana hoja za kuwasaidia watanzania, badala yake wanategemea siasa za matukio ili kujipatia kura. Tunaomba watanzania muwapuuze.

Imetolewa na:

Shaka Hamdu Shaka,
Kaimu Katibu Mkuu - UVCCM Taifa na Mjumbe wa NEC.
30 August 2015.
WhatsApp Image 2017-12-09 at 09.12.30.jpeg
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom