Babu Seya na wanae waibukia Mapinduzi ya Zanzibar

Babu Seya na wanae waibukia Mapinduzi ya Zanzibar

Benjamini Netanyahu

JF-Expert Member
Joined
Aug 7, 2014
Posts
102,675
Reaction score
126,914
babu.jpg

Familia ya mwanamuziki Nguza Vicking 'Babu Seya' imeungana na Wazanzibari kwa ajili ya kusherehekea maadhimisho ya miaka 54 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Maadhimisho hayo yaliyafanyika jana Ijumaa katika Uwanja wa Amaan Zanzibar yakihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa kitaifa akiwamo Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein.

Tayari Serikali imewatafutia studio ya kurekodi muziki familia familia hiyo baada ya kuonana na Rais John Magufuli Ikulu waliopokwenda kutoa shukurani.

Mmoja mtoto wa Babu Seya, Michael Nguza maarufu kama Nabii Nguza aliliambia Mwananchi kuwa lengo la kwenda Zanzibar ni kusherekea maadhimisho ya mapinduzi hayo.

“Tumekuja kusherehekea sikukuu ya Mapinduzi ya Zanzibar,” amesema Nabii Nguza.

Babu Seya na wanawe Johnson Nguza ‘ Papii Kocha na Nabii Nguza wameanza kuonekana hadharani mfululizo ikiwa ni baada ya kuonana na Rais Magufuli walikokwenda kutoa shukurani baada ya kuachiwa huru Desemba 9 mwaka jana.

Baada ya kuonana na Rais Magufuli siku zilizofuata wakiwa na , Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Juliana Shonza walikwenda katika Studio za Wanene zilizopo Mwenge kwa ajili ya mchakato wa kuanza kufanya kazi zao.

Chanzo: Malunde blogs
 
Hivi hawa si ni WACONGOMAN au ndo washakuwa WATZ Automatic
 
Jamii ya waathriwa wa vitendo vyao vile wanasikiaje?
Au walisingiziwa?
 
Back
Top Bottom