Sharon Otieno, uhai uliochukuliwa kuficha aibu ya Gavana

kwa-muda

JF-Expert Member
Sep 5, 2018
1,163
2,223
sharon-otieno-2.jpg

Sharon Otieno mwanafunzi wa chuo kikuu alikuwa ni kimada wa Gavana wa Migori -Kenya, Bwana Okoth Obado. Sharon alitekwa na mwili wake ukaja okotwa ukiwa una jeraha la kuchomwa kisu.
kutokana na uchunguzi wa polisi, imegundulika kwamba Sharon alikuwa mjamzito na mimba ikiwa ya gavana ambaye alitaka itolewe lakini Sharon aligoma kuitoa. Na alipoona gavana anasisitiza hiyo mimba itoke na asipoitoa wasijuane, Sharon aliuamua kuuza habari hiyo kwa mwandishi wa habari ambaye wakati walikutana na kutekwa pamoja ila mwandishi wa habari alifanikiwa kuruka kutoka kwenye gari na kutoroka.
Kutokana na upelelezi wa makachero haya ndiyo matukio yaliyojiri mpaka kutekwa na kuawa kwa Sharon:

Tarehe 3 Sept
Sharon na mwandishi wa habari wa gazeti la Nation, Baraka Odur wanatekwa wakiwa kwenye harakati za kukutana na mtu aliyedai ana habari anayotaka kumpatia huyo mwandishi huko Homa bay Kisumu. Mtoa habari huyo anakuja kufahamika kuwa ni msaidizi binafsi wa Gavana Okoth na anaitwa Michael Oyamo.
Odour anafanikiwa kutoroka kwa kuruka kutoka kwenye gari ikiwa kwenye mwendo katika eneo la soko la Nyangweso huko Homa Bay kwenye Barabara ya kuelekea Kisumu.

Tarehe 4 Sept
Ikiwa ni siku ya Jumatatu, makachero wanamkamata msaidizi wa gavana Okoth ajulikanaye kama Michael kwa tuhuma za kuwateka Sharon na Odour.
Mwili wa Sharon unaokotwa ukiwa umetupwa katika msitu wa Odori huko katika kitongoji cha Homa Bay. Wakati huo Sharon alikuwa na ujauzito wa miezi saba na mwili ulikuwa na majeraha ya kuchomwa chomwa kwa kisu. Mwili unachukuliwa na kuhifadhiwa kwenye hospitali ya Oyugis Level Four iliyo katika mji wa Oyug.

Tarehe 5 Sept
Wanafunzi wa chuo kikuu cha Rongo wanafanya maandamano wakitaka haki itendeke juu ya mauaji ya Sharon. Maandamano yanafanyika katika barabara yenye jina la gavana ijulikanayo kama Rongo-Migori High way.

Tarehe 7 Sept
Uchunguzi juu ya mwili wa marehemu Sharon unagundua kuwa alibakwa, akakabwa, na kuchomwa mara kadhaa kwa kisu, pia hata kiumbe alichokuwa kabeba tumboni mwake nacho kilichomwa kisu.

Tarehe 8-9 Sept
Polisi wanazidi kukamata washukiwa zaidi baada ya upelelezi kuzidi kupanuka.

Tarehe 10 Sept
Msaidizi wa gavana, Michael anafikishwa kwenye mahakama ya Homa Bay na kusomewa mashitaka yake juu ya kuhusika na mauji ya Sharon. Mahakama inamnyima dhamana. Michael anashitakiwa akiwa pamoja na wahusika wengine nane na wote wanabaki mahabusu.

Tarehe 11 Sept
Gavana Okoth anafanyiwa mahojiano na kitengo cha DCI huko Kisumu. Mahojiano hayo yanachukua saa nane.
Kunakuwa na sintofahamu baada ya Michael kuachiliwa na kukamatwa tena na makachero wa DCI kisha kumpeleka Kisumu.

Tarehe 13 Sept
Gavana Okoth anaitishamdaharo na waandishi wa habari kisha anakiri kuwa alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na marehemu Sharon aliyekuwa na umri wa miaka 26. Pia natambulisha familia yake kwa hadhira kwa mara ya kwanza na kudai kwamba familia yake ilikuwa inafahamu juu ya uhusiano huo. Okoth nadai kwamba hakuhusika kabisa na mauaji ya kinyama ya mwanadada huyo.

Tarehe 15 Sept
Kitoto cha Sharon kinazikwa nyumbani kwa babu yake SHharon huku jamii ikitaka uchunguzi ufanyike na haki itendeke.

oko.jpg


Tarehe 16 Sept
Makachero wanakamata gari lenye rangi ya kijivu aina ya Toyota Fielder lenye usajili wa namba KCL 481, gari hilo ndilo linadaiwa kutumika katika utekaji nyara wa marehemu na mwandishi wa habari. Dereva wa gari hilo natambulika kwa jina la Jackson Otieno Gombe, ambapo naye anashikiliwa na jeshi la polis.

Tarehe 18 Sept
Casper Otieno,ambaye ni mmoja kati ya wapambe wa gavana Okoth anajisalimisha mwenyewe katika kituo cha polisi baada ya kugundulika kwamba lile gari ni mali ya mke wake.

Tarehe 20 Sept
Kipimo cha DNA kinagundua kuwa ni kweli kwamba ile mimba aliyokuwa kabeba marehemu Sharon ilikuwa ya gavana Okoth. gari ile Toyota Fielder iliyotumika katika utekaji inapelekwa kwenye kitengo cha uchunguzi (forensic analysis) huko Nairobi. Gari hilo inashikiliwa katika makao makuu ya kitengo cha DCI.

Tarehe 21 Sept
Makachero wanamkamata gavana Okoth baada ya kuweza kupata ushahidi wa kutisha unaomhusisha moja kwa moja na mauaji ya Sharon. Anahifadhiwa katika kituo cha polisi cha Girigiri kwa maelekezo kutoka kwa mkuu wa kitengo cha DCI George Kinoti. Okoth anamaliza wikiendi akiwa mahabusu.

Tarehe 24 Sept
Gavana Okoth anapelekwa mahakama ya Milimani kwa mashitaka ya mauaji. Anakana mashitaka. Mahakama ina amuru aendelee kushikiliwa katika gereza huku ombi la kupatiwa dhamana likiamuliwa kuwa litasikilizwa tarehe 25 Sept.
Migori anakuwa mtuhumiwa namba tano, pamoja na msaidizi wake Michae, pia mlinzi wake Elvis Omondi na mweka mpambe wake ambaye pia ni mweka hazina wa jimbo Caspal Obiero ambaye ndiye mmiliki wa lile gari.
oko2.jpg
 
Hawana akili,kitendo cha Mwandishi kuwatoka ama wangesitisha huo unyama kwa huyo Dada ama wangemtafuta Mwandishi mpaka apatikane. Yote juu ya yote huu ni unyama uliozidi kipimo.
 
  • Thanks
Reactions: rr3
Kosa kubwa la marehemu ni kujaribu kuuza habari.
Ilikuwa kama tamaa flani na alitaka kujinufaisha na mimba.

Mwanasiasa aliehusika ni katili kupita maelezo bila kujali tamaa au makosa ya marehemu.
 
Back
Top Bottom