Shangwe kwa wadau wa horticulture kwa kupatikana kwa ndege ya mizigo

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,810
11,980
Asasi kilele ya kukuza na kuendneleza kilimo cha matunda, mboga, maua na mbegu Tanzania (TAHA) kwa kushirikiana na kampuni ya kuendeleza kiwanja cha ndege cha Kilimanjaro (KADCO) wamefanikiwa kuleta ndege ya mizigo kwa ajili ya kutatua changamoto ya usafirishaji wa mazao ya horticulture kwenda nje ya nchi.

Ujio wa ndege hiyo ya 787-dreamliner mali ya shirika la ndege la Ethiopia imekuja kama jitihada ya TAHA kutafuta namna ya kutatua changamoto ya kuokoa hasara inayotokea kwa wakulima kwa madhara ya ugonjwa wa COVID-19 iliyosababisha makampuni mengi ya ndege duniani kusimamisha safari za ndege hivyo kusababisha madhara makubwa kwa wakulima na wafanya biashara wa mazao ya horticulture

Akizungumza mara baada ya kutua kwa ndege hiyo katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Kilimanjaro, Afisa Mtendaji Mkuu wa TAHA Dkt.Jacqueline Mkindi amesema TAHA ilijisikia vibaya kusikia uharibifu uliotokana na kukosekana kwa usafiri wa ndege, huku akielezea adha waliyokutana nayo wakati wa kutafuta nafasi katika kiwanja cha ndege cha Nairobi jambo ambalo iliwaongezea nguvu katika kufanya jitahda za kupata ndege.

Vile vile amesema anashukuru sana serikali kwa kuunga mkono jitihada hizo na wadau wengine katika tasnia kwani hawakujali kuwa kuna tishio la ugonjwa wa COVID-19 lakini waliamini katika kutafuta suluhisho la changamoto zainazowakabili

Akielezea matumaini yao makubwa katika kukabiliana na changamoto ya usafiri wa mazao ya horticulture (perishable goods) Meneja Mkuu wa kampuni ya usafirishaji (TAHAFRESH) Amani Temu amesema wamejipanga si kwa COVID-19 pekee ila kuhakikisha changamoto inamalizika.

Ndege hiyo ya mizigo itakuwa ikitua mara tatu kwa wiki kwa ajili ya kupakua mizigo kwa ajili ya kusafirisha, jambo litakalopunguza adha kubwa kwa wakulima waliokuwa wakiteseka na kutafuta nafasi katika nchi jirani. Kutua kwa ndege hiyo jana iliondoka na tani 27 za mizigo ya horticulture na kg 308 za mizigo ya kawaida.

Kwa upande wa KADCO, Mkurugenzi mtendaji Eng. Christophr Mkoma amesema wanaishukuru sana TAHA na wadau wengine kwa ushirikiano mwema huku akiahidi kutoa ushirikiano kikamilifu katika kutekeleza na kukuza tasnia ya horticulture kwa ajili ya manufaa ya Taifa

Aidha mkurugenzi wa TAHA Dr.Mkindi amewataka watanzania kuendelea kuchukua hatua stahiki ya kujikinga dhidi ya COVID-19 huku wakizidi kuchapa kazi na kuacha kubweteka kwa sababu ya hofu ya ugonjwa huo.
 
Hii ni habari njema sana kwa watanzania na hasa Kilimanjaro na Arusha changamkieni fursa hiyo kama kawaida yenu.
 
Back
Top Bottom