Shamsa Ford aungana na Ney wa Mitego kwenye 'Wapo Tour'

Johnny Sack

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
8,942
19,130
Nani amekuambia wapenzi waliotengana au kuachana ni maadui? Sahau kabisa kuhusu hilo kwani Rapa Nay wa Mitego ameudhihirishia umma kwa kutangaza kuwa kwenye Tour yake ya muziki ‘Wapo Tour’ atasindikizwa na ex wake Shamsa Ford kwenye Special Appearance na pia atakuwa MC siku hiyo.
upload_2017-5-7_14-0-32.jpeg


Nay wa Mitego amesema watu wengi huwa wanaamini mkiachana basi ndiyo mwisho wa urafiki lakini kumbe sio hivyo na ndiyo maana hata yeye ameamua kumleta Shamsa Ford kwenye Tour yake ya Wapo.

Wapo Tour itakuwa ni ya Kipekee sana kwani itakuwa na list ya wasanii wawili watatu hivi wa kunisindikiza, lakini pia atakuwepo Shamsa Ford kwenye Special Appearance pia atakuwa kama MC kwa siku hiyo jukwaani,watu watarajie kuona burudani ya kipekee kabisa“Amesema Nay wa Mitego kwenye mahojiano yake na Bongo Five.

Nay wa Mitego na Shamsa Ford walishawahi kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi miaka ya nyuma na baadae kuachana.

‘Wapo Tour’ itaanzia jijini Dar es Salaam tarehe 20 May Mwaka huu pale Dar Live,Mbagala na baadae kuelekea mikoani.

By Godfrey Mgallah

Chanzo: Bongo5
 
Si mbaya maana bongo movie kila kitu kwao maigizo ili mradi pesa iingie mfukoni.

Huyu ney kila siku anawatukana bongo movie ila akitaka kuwatumia wanamshobokea sana,ndio hivyo tena watu wenyewe wamebakiza akili za kuvukia bara bara,movie zenyewe zimebakiza audience za mabasi ya masafa marefu.
 
Bila shaka watalala room Moja huko kwenye hiyo tour.
Dawa ya Ex wako ni kumchunia Moja kwa Moja kinyume na hapo ni sawa na kutembelea muwa kama mkongojo ukifika njiani utakula tu.
 
Wakapashe tu kiporo hakuna namna, japo ni mapema mno tangu mwanadada kufunga ndoa- kiporo hata hakijachacha baaana tyr kinaenda kupashwa!
 
Back
Top Bottom