NI JUKUMU LA UVCCM KUWALINDA VIONGOZI WETU WA CHAMA - SHAMIRA
Mjumbe wa Baraza Kuu (UVCCM) Taifa Ndg Shamira Mshangama amesema vijana wa CCM wana jukumu la kulinda viongozi wanaotokana na Chama cha Mapinduzi kwa kuhakikisha wanaendelea kushika nafasi ambapo kama Mbunge au diwani alikuwa ni kutoka CCM ataendela kubaki wa Chama hicho katika uchaguzi unaofuata
Shamira Mshangama ameyasema hayo wakati akizungumza na wajumbe wa Kamati ya Utekelezaji mkoa wa Songwe ikiwa ni muendelezo wa Ziara yake ya kuimarisha uhai wa Jumuiya ya Vijana wa CCM katika Mikoa, wilaya, Matawi na Shina kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka huu 2025 ambapo amesema vijana wana jukumu la kuhakikisha kazi za Viongozi ikiwemo miradi mbalimbali inayotekelezwa inafahamika kwa wananchi
Amesema kupitia Kutangaza miradi inayotekelezwa kutasaidia kupata kura za Kishindo ambapo ametoa rai kwa vijana wote nchini kuendelea kuyasema yanayofanywa na Rais Dkt Samia katika kuwaletea wananchi Maendeleo