Shambulizi la moyo (heart attack)

Dr, asante sana kwa ujumbe wako huu. binafsi nina maswali mawili

je watoto wadogo wanaweza kupata matatizo haya ya moyo?

je haya matatizo yanahusiana vipi na moyo kuwa na tundu?
ni mara chache watoto wadogo kupatwa na ugonjwa huu. wataupata tu iwapo mishipa yao ya moyo (coronary arteies) zina hitilafu ya kuzaliwa (prinzmetal angina) ambayo husababisha mishipa hiyo kuwa ina inasinyaa (spasm). kuhusu tundu katika moyo, inategemea ni tundu gani, kuna mfano ASD,VSD, na patent ductus arterious n.k. hayo ni baadhi ya common matobo katika moyo, lakini kwa kweli hayasababishi heart attack!!
 
  • Dawa ya kuyeyusha mafuta katika mishipa ya damu kama vile clopidogrel

ningependa kuwashaulu watz wenzangu kuwa mtu anapata heart attack jaribuni sana kitu cha kwanza kumpa aspirin, inazibua hiyo mifupa. fungueni pia madirisha ili apate hewa ya kutosha. ni huduma ya kwanza na ya muhimu katika kuokoa maisha ya mgonjwa




 
Asante mzizi mkavu, kwa elimu unayotupa,
binafsi nafaidika sana nayo.
Ubarikiwe zaid, na uishi miaka mingi yenye afya njema,
ili tuendelee kuipata elimu yako.
 
dr asante sana kwa elim sasa hapa napo nina maswali
je watu hawa wenye unyongevu, huwa wanakuwa kwenye hatari wanapowaza tu kutaka kujiua au hatar ni mapaka waanze kutenda kitendo hicho?

je tabia na mwenendo wa maisha hasa stress unachangiaje hili tatizo kwa vijana?
@​gfsonwin Dawa ya Stress bila ya kula Vidonge

1. Jaribu kuwa kimya nyumbani au chumbani,


2. Koga maji ya umoto moto au vuguvugu kadri upendavyo au kama una mke/mume mwambie akukande kande na maji mgongoni.


3.Ukimaliza oga jifute mwili kisha paka lotion ya lavender au aroma therapy lotion au aveeno lotion.


4. Panda kitandani lala panda kitandani ulale huku umejifunika shuka soft au blanket soft au comforter safi.


5. soma duaa yako ya kulali geuka mkono wa kulia vuta pumzi ndani nje mara tatu huku ukifikiria neema za Mola wako na mambo mazuri yaliokutoke kisha lala.


Utaamka stress au mawazo yote yameondoka guarantee.

Zingatia haya yote yanafanyika baada ya swala zako na dua zako kumuomba Mola kwani hiyo ni bora zaidi. Jaribu kufanya hivyo kisha unipe Feedback. P.h.D. MziziMkavu.
 
mkuu gfsonwin , vipi hali ya mama yako? naomba utupe mrejesho please.

Nina ndugu yangu (aged 28) ananyemelewa/amepata stroke likely. Wanasema huwa ana historia ya presha ya kupanda. Juzi usiku alianguka chini (kuanguka kwa kawaida baada ya kuhisi kizungu zungu). Wakampeleka hospital, akachomwa sindano na kulazwa kwa night moja kuamkia jana, asubuhi akawa discharged akaendelee kunywa dawa nyumbani. Alipata matibabu yafuatayo:

1. Lasix - Sindao
2. Junior asprin - Vidonge
3. Olmesar H - Vidonge
4. Nifedipine - Vidonge
5. Neuroton - Vidonge
6. To attend Physiotherapy - hii bado hawajafanya.

Tangu alipodondoka ile usiku, akawa anahisi upande mmoja wa mwili (kuanzia mdomo, mkono, na mguu) una ngazi, yaani viungo hivyo upande mmoja wa mwili vimeganda! Hata kuongea hatamki maneno vizuri.

Alianza kutumia dawa hizo za vidonge jana asubuhi baada ya kuwa discharged, alikuwa hana nguvu kabisa hawezi kusimama wala kunyanyuka pekeake. Leo kaamka ana nguvu kidogo (japo bado hawezi kuinuka pekeake) na ule mguu uliokuwa umeganda/umepooza ameanza kuusense kwa mbaaali akikanyagia. Ila mkono bado kabisa umeganda (hausense kabisa) na mdomo pia bado (hatamki maneno vizuri).

Kama una chochote cha ku-share regarding kutibia mgonjwa wa stroke, nitashukuru sana.

-Kaveli-
 
Back
Top Bottom