Nimeambiwa mishipa midogo katika moyo wangu haipati damu ya kutosha hivyo imenisababishia maumivu upande wa kushoto

malembeka18

JF-Expert Member
Jan 26, 2018
2,780
2,716
Habari wakuu,

Nimekua nikisumbuliwa na maumivu ya upande wakushoto ktk bega na nyuma ya bega usawa wa moyo nimefanya ecg na echo nimebiwa echo Iko sawa. Ila ecg inaonyesha shida kidgo nkaambiwa haya maumivu yanasabishwa na mishipa midogo midogo iliyoko katika moyo haipati damu yakutosha. Nikauliza inatokana na nin akasema inatokea tu. So Ina nkapewa aspirin.

Wakuu nakuja kwenu kuuliza vip huwa kunautatuzi wamoja kwa moja kuifanya mishipa midogo midogo ipate damu yakutosha nakumaliza kabisa tatizo la maumivu
 
Pole,

Daktari aliyefanya ECG ndo ana uwezo wa kusema lolote juu ya hili ua mabadiliko ya mwenendo wa umeme yaliyoonekana na kama yana hatari yoyote au la. Au yanahitaji tiba zaidi.

Jibu lingine unaweza kulipata kwa Invasive Cardiologist ambaye huweza kufanya vipimo zaidi vya kuangalia kiasi cha tatizo kwenye mishipa ya damu ya moyo na kama kwa kiasi husika unahitaji kufanyiwa chochote au la. Hii utaipata kwenye vituo mahsusi kwa magonjwa ya moyo kama Jakaya Kikwete/MNH VS Aga Khan nk.
 
Tatizo hili huwa linatokana na nin
Kuna sababu 21 na zaidi zilitajwa kwenye uzi uliouliza kama siku 2-3 zilizopita(Tatizo la umeme kwenye moyo).

Ili kupata sababu halisi hutegemea historia halisi ya mgonjwa husika, dalili, wakati gani, nini huongeza shida au kupunguza, aina ya mabadiliko ya umeme kwenye ECG nk.
 
Kaka nimepitia baadhi ya juzi zako unasumbuliwa na matatizo mengi kiasi lakn naomba nikushauri kama utafata ushauri wangu utapona kabisa tatizo lako

Tumia kitunguu saumu chukua punje za kitunguu saumu asubuhi meza punje 5 au 4 kwa Kutafuna then unatumia na maji kusukumizia
Mchana tumia mchana kiwango hiko hiko baada ya kula na tumia usiku baada ya kula


Kitunguu hutanua mishipa ya Damu na kitunguu pia hutibu matatizo ya Figo na ukawa sawa kabisa, kitunguu hutibu pia vidonda vya tumbo,husaidia pia kuondoa msongo wa mawazo, kitunguu huondoa cholesterol,mafuta yaliyopo kwenye mishipa ya Damu huondoka yote,hutibu pia UTI, hutibu pia Malaria sugu , matatizo ya moyo,bawasili

Kingine jitahidi Ufanye Mazoezi ya Mwili utoe jasho lakutosha mwilini,punguza Uzito , jitahidi Sana uwe unakuwa karibu na mungu wako usihambuliwe na mapepo mabaya,uchawi,majini na magonjwa nenda msikitini au kanisani hata kwa watumishi


Yote hayo bila kusahau kuacha kutumia mafuta ya korie, achana kabisa kula chips,acha kula vyakula vya wanga, asubuhi usile ukashiba kula kidogo tu,acha Matumizi ya sukari ni hatari ,acha Matumizi ya vyakula vya Ngano ni hatari si salama , Usitumie vinywaji vya viwandani kama soda na pombe nk.


Badili mfumo wako wa Maisha, maradhi hayatokwisha ukikaidi

Ukiuthamini ukale,Usasa hautokumaliza
View attachment 2739880View attachment 2739881
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom