Shambulizi la moyo (heart attack) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Shambulizi la moyo (heart attack)

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Apr 21, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Apr 21, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Moja ya magonjwa hatari sana ambayo yanaweza kumpata mtu yoyote ni ugonjwa wa shambulizi la moyo. Huu ni miongoni mwa magonjwa yanayoongoza kwa kusababisha vifo vya wanaume na wanawake.

  Kwa kawaida, ugonjwa huu hutokea pale ambapo sehemu ya nyama ya moyo inapoharibika au kufa kutokana na kukosa damu ya kutosha.

  Je tatizo hili husababishwa na nini?
  Husababishwa na kuziba kwa mishipa ya damu inayosambaza damu katika moyo (coronary artery blockage) kutokana na mafuta mabaya mwilini (atherosclerotic plaque).

  Watu gani wapo katika hatari ya tatizo hili?
  Watu walio katika hatari ya kukumbwa na ugonjwa huu ni pamoja na


  • Wenye umri mkubwa miaka 45 kwa wanaume na 55 kwa wanawake
  • Wavutaji wa sigara
  • Watu wenye mafuta ya lijamu katika damu au wale wenye mafuta mabaya aina ya triglycerides na low density lipoprotein kwa kiwango kikubwa katika damu zao
  • Wenye kisukari
  • Wenye matatizo ya shinikizo la damu
  • Walio na unene kupita kiasi (obesity)
  • Wenye matatizo sugu ya kushindwa kufanya kazi kwa figo zao (chronic renal failure)
  • Moyo kushindwa kufanya kazi (heart failure)
  • Wanywaji wa pombe kupindukia
  • Watumiaji wa madawa ya kulevya hasa cocaine na methamphetamine
  • Watu wenye msongo wa mawazo (Chronic high stress levels)
  • Upungufu wa vitamin B2, B6, B12 na folic acid
  Dalili za shambulizi la moyo

  • Maumivu makali ya ghafla kifuani ambayo husambaa kwenye taya, shingo, bega na mkono wa kushoto
  • Kupumua kwa shida
  • Kutoka jasho kwa wingi sana (diaphoresis)
  • Kuhisi mapigo ya moyo yanapiga haraka (palpitations)
  • Kichefuchefu
  • Kutapika
  • Kuchoka haraka sana
  • Kupoteza fahamu
  Shambulizi la moyo limehusishwa na nini?
  Tafiti mbalimbali zimeusisha mambo yafuatayo na shambulizi la moyo


  • Msongo wa mawazo
  • Maambukizi hasa vichomi vinavyosababishwa na vimelea vya chlamydophila pneumonia.
  • Hutokea zaidi asubuhi hasa saa tatu (saa 3 asubuhi)

  Vipimo na uchunguzi

  • ECG - Kipimo hiki huonyesha ni sehemu gani ya moyo iliyoathirika
  • Coronary angiography - Kinasaidia kwa kuangalia wapi ambapo mishipa ya damu imekuwa membamba sana kupita kiasi (narrowing of vessels) au imeziba.
  • Cardiac markers levels
  • X-ray ya kifua (chest X-ray)
  • MPI (Myocardial Perfusion Imaging) - Kipimo hiki hufanywa kwa kutumia mashine maalum ya PET Scan ambapo kinauwezo wa kugundua tatizo la shambulizi la moyo, huchunguza kikamilifu maumivu ya kifua, huangalia mwelekeo wa tiba ya kuzuia damu kuganda, hutoa mwelekeo wa ugonjwa wa shambulizi la moyo kama ni mzuri au mbaya, hutathmini ubora wa tiba ya shambulizi la moyo kabla na baada ya mgonjwa kupata tiba, huweza kutambua hata shambulizi la moyo ambalo si rahisi kugundulika kwa kutumia vipimo vyengine na pia hutathmini ukubwa wa tatizo la shambulizi la moyo. Hata hivyo kwa sasa kipimo hiki hakipatikani nchini kwetu.
  Ili kuweza kutambua uwepo wa tatizo hili, mwaka 1979, shirika la Afya Duniani (WHO) liliweka vigezo vya kutambua shambulizi la moyo. Vigezo hivyo ni

  • Historia ya kuwa na maumivu ya kifua zaidi ya dakika 20
  • Mabadiliko katika kipimo cha ECG, na
  • Kupanda na kushuka kwa kipimo kiitwacho kitaalamu cardiac biomarkers hasa creatine kinase - MB na troponin
  Matibabu
  Shambulio la moyo ni tatizo linalohitaji matibabu ya dharua. Lisipotibiwa kwa haraka husababisha kifo katika muda mfupi sana tangu mgonjwa apatwe na tatizo. Matibabu ya tatizo hili hujumuisha


  • Kumpa mgonjwa hewa ya oksijeni
  • Mgonjwa hupewa vidonge vya Aspirini ndogo kuzuia damu kuganda (thrombolytic) kwa ajili ya kuyeyusha damu iliyaganda na hivyo kuzibua mirija midogo ya damu katika moyo iliyozibwa na kuganda huku kwa damu.
  • Vile vile mgonjwa hupewa dawa za kuweka chini ya ulimi kiitwacho nitrogylycerin (glyceryl trinitrate) ambazo husaidia kutanua mishipa ya damu (vasodilation)
  • Dawa ya kutuliza maumivu kwa mfano morphine
  • Dawa ya kuyeyusha mafuta katika mishipa ya damu kama vile clopidogrel
  • Kuzibua mishipa ya damu inayosambaza damu katika moyo kwa kutumia - Percutaneous coronary intervention (PCI)
  • Upasuaji (CABG)
  Njia za kuzuia shambulizi la moyo

  • Kuacha kuvuta sigara
  • Kufanya mazoezi ya mara kwa mara
  • Kupunguza unywaji wa pombe
  • Kubadilisha aina ya mlo. Kupunguza mafuta katika mlo na chumvi.
  • Kutumia mafuta ya samaki (omega-3 fatty acids)
  • Kuna utafiti unaosema kuwa uchangiaji damu hupunguza hatari ya magonjwa ya moyo hasa kwa wanaume.
  Madhara ya shambulizi la moyo

  • Moyo kushindwa kufanya kazi (heart failure)
  • Matatizo katika mfumo wa mapigo ya moyo (Atrial fibrillation) ambayo hatimaye hupelekea kifo
  • Shambulizi la moyo kurudia mara ya pili
  • Kifo cha ghafla (sudden death)
  • ​Dr.Henry Mayala
   
 2. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #2
  Apr 21, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,963
  Likes Received: 1,841
  Trophy Points: 280
  Dr, asante sana kwa ujumbe wako huu. binafsi nina maswali mawili

  je watoto wadogo wanaweza kupata matatizo haya ya moyo?

  je haya matatizo yanahusiana vipi na moyo kuwa na tundu?
   
 3. M

  Ma Tuma Senior Member

  #3
  Apr 21, 2012
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 123
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  hongera dr haya ndio mambo yanayofaa kuelimisha jamii.hongera kwa upendo wako.tutazingaia
   
 4. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #4
  Apr 21, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,963
  Likes Received: 1,841
  Trophy Points: 280
  hhivi dr mbali na pb, ni kitu gani kingine kinachoweza kusababisha stroke au kupooza?
   
 5. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #5
  Apr 21, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  @gfsonwin Unyongovu Waweza Kusababisha Magonjwa ya Moyo kwa Vijana


  Katika tafiti mpya zilizofanywa hivi karibuni zinaonyesha kuwa unyongovu na jaribio la kujiua ni viashiria hatari ambavyo huleteleza vijana kufa kwa magonjwa ya moyo.
  [​IMG]
  Katika utafiti mkubwa uliohusisha washiriki zaidi ya 7000 walio chini ya miaka 40 ulionyesha kuwa kwa wale waliokuwa na historia ya unyongovu au jaribio la kujiua walikuwa na hatari kubwa zaidi ya kufa kutokana na magonjwa ya moyo hasa yale ambayo moyo hukosa oksijeni ya kutosha (ischemic heart disease) ukilinganisha na wale ambao hawakuwa na historia hiyo.
  Ingawa jinsia zote zilikuwa kwenye hatari zaidi ya kufa kutokana na magonjwa ya moyo, lakini wanawake wenye unyongovu au waliofanya jaribio la kujiua walikuwa na hatari mara 14 zaidi ya kufa kwa magonjwa ya moyo yatokanayo na kukosa oksijeni ya kutosha (ischemic heart disease) kulinganisha na wale ambao hawakuwa na unyongovu au jaribio la kujiua.
  Katika utafiti huu uliofanywa na Profesa Viola Vaccarino kutoka chuo kikuu cha Emory, Atlanta, Georgia aligundua jinsi matatizo ya kisaikolojia yanavyopelekea kuongeza hatari ya kufa mapema na magonjwa ya moyo katika idadi ya vijana.
  Taarifa nyingi zilizopo za magonjwa ya moyo ambazo zilizokwisha tolewa huwa za umri wa kati na wazee, maana imekuwa ikizoeleka magonjwa haya huathiri zaidi rika hiyo, ambayo ni kweli kabisa hasa katika magonjwa yanao athiri zaidi mishipa ya damu ya moyo (CHD).
  Kutokana na watatifi mkazo humewekwa zaidi kwa wazee ingawa magonjwa mengi ya moyo huanza katika kipindi cha ujanani.
  Katika utafiti huu taarifa zilichukuliwa kutoka kwa washiriki 7641, wenye umri kati ya 17 hadi 34, kutoka mwaka 1988 hadi 1994.
  Katika ratiba ya uchunguzi, tathmini ilikuwa kuhusu unyongovu na jaribio la kujiua , na matokeo baada ya ufuatiliaji yalikuwa kama ifuatavyo: washiriki 51 walikufa kutokana na magonjwa ya moyo, na kati ya hao 28 walikufa kutokana na moyo hukosa oksijeni ya kutosha (ischemic heart disease).
  [​IMG]
  Wagonjwa 538 walikutwa na historia ya unyongovu na 419 kuwa na jaribio la kujiua. Na 136 walikuwa na historia ya vyote viwili.
  kubadilishwa athari ya uwiano (HR) kwa ajili ya hatari kwa CVD kifo 2.38 kwa ajili ya wagonjwa walio na unyogovu (95% ya muda kujiamini [CI], 0.93-6.08) na 3.21 kwa ajili ya wale walio na majaribio ya kujiua zamani (95% CI, 1.36-7.56)
  Kuna mjadala mkubwa kuhusu madhara ya unyogovu na ugonjwa wa moyo na mishipa katika vifo vya wanawake kama ikilinganishwa na wanaume. Nadhani ushahidi kutoka kwa utafiti huu ni imara lakini masomo ya baadaye ni wazi kuwa ni muhimu.
  Mmoja wa watafiti wengine Dr Scherrer alisema “kwa madaktari, anadhani matokeo ya jumla yanazidi kuongeza wasiwasi ni wakati gani hutambua unyongovu, ambapo ni kawaida kwa watu wenye umri mdogo, kuna uwezekano wa haja ya kuweka mkazo mkubwa katika kufuatilia afya yao ya moyo. Na kwamba sio kitu ambacho madaktari wengi hufanya mara kwa mara kwa wagonjwa wenye umri mdogo sana.
  Na hii huacha swali kubwa la kujiuliza:
  Je inawezekana kuzuia magonjwa ya moyo yahusishwayo na unyongovu, kwa kuimarisha usimamizi na ufuatiliaji wa mambo ya hatari yanayoweza kupelekea magonjwa ya moyo kwa kundi la vijana?
  Unyongovu Waweza Kusababisha Magonjwa ya Moyo kwa Vijana
   
 6. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #6
  Apr 21, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,963
  Likes Received: 1,841
  Trophy Points: 280
  dr asante sana kwa elim sasa hapa napo nina maswali
  je watu hawa wenye unyongevu, huwa wanakuwa kwenye hatari wanapowaza tu kutaka kujiua au hatar ni mapaka waanze kutenda kitendo hicho?

  je tabia na mwenendo wa maisha hasa stress unachangiaje hili tatizo kwa vijana?
   
 7. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #7
  Apr 21, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  @gfsonwin
  A stroke occurs when the blood supply to part of your brain is interrupted or severely reduced, depriving brain tissue of oxygen and food. Within minutes, brain cells begin to die.
  A stroke is a medical emergency. Prompt treatment is crucial. Early action can minimize brain damage and potential complications.
  The good news is that strokes can be treated and prevented, and many fewer Americans now die of stroke than was the case even 15 years ago. Better control of major stroke risk factors — high blood pressure, smoking and high cholesterol — is likely responsible for the decline.

  Symptoms


  Watch for these signs and symptoms if you think you or someone else may be having a stroke. Note when signs and symptoms begin, because the length of time they have been present may guide treatment decisions.

  • Trouble with walking. You may stumble or experience sudden dizziness, loss of balance or loss of coordination.
  • Trouble with speaking and understanding. You may experience confusion. You may slur your words or be unable to find the right words to explain what is happening to you (aphasia). Try to repeat a simple sentence. If you can't, you may be having a stroke.
  • Paralysis or numbness on one side of your body or face. You may develop sudden numbness, weakness or paralysis on one side of your body. Try to raise both your arms over your head at the same time. If one arm begins to fall, you may be having a stroke. Similarly, one side of your mouth may droop when you try to smile.
  • Trouble with seeing in one or both eyes. You may suddenly have blurred or blackened vision, or you may see double.
  • Headache. A sudden, severe "bolt out of the blue" headache, which may be accompanied by vomiting, dizziness or altered consciousness, may indicate you're having a stroke.
  When to see a doctor
  Seek immediate medical attention if you notice any signs or symptoms of a stroke, even if they seem to fluctuate or disappear. Call 911 or your local emergency number right away. Every minute counts. Don't wait to see if symptoms go away. The longer a stroke goes untreated, the greater the potential for brain damage and disability. To maximize the effectiveness of evaluation and treatment, it's best that you get to the emergency room within 60 minutes of your first symptoms.

  If you're with someone you suspect is having a stroke, watch the person carefully while waiting for emergency assistance. You may need to:

  • Begin mouth-to-mouth resuscitation if the person stops breathing
  • Turn the person's head to the side if vomiting occurs, which can prevent choking
  • Keep the person from eating or drinking

  Kiharusi ni ugonjwa unaoleta kupooza unaosababishwa na matatizo kwenye mishipa ya damu inayolisha ubongo.
  Katika tiba kiharusi (stroke) inamaanisha upotevu wa uwezo wa ubongo unaoendelea haraka. Sababu yake ni tatizo katika mishipa ya damu inayopeleka damu kwenda ubongo. Matatizo haya ni ama kuzibwa au kupasuka kwa mishipa ya damu. Seli za ubongo hufa haraka zisipopata oksijeni na lishe ya kawaida na yote haya hufika kwa njia ya damu.
  Kiharusi ni hali ya dharura inaweza kutibiwa kama tatizo latambuliwa na kutibiwa haraka. Lisipotibiwa husababisha viwango mbalimbali vya kipooza mwilini.
  Shinikizo la juu la damu, usukari, chakula chenye mafuta mengi au kuvuta kwa sigara huongeza hatari ya kushikwa na kiharusi.
   
 8. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #8
  Apr 21, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,963
  Likes Received: 1,841
  Trophy Points: 280
  my mom was attacked with stroke 8 months ago. she was examined and they found that she doesnt have neither hypertension nor diabetese and she doesnt smoke. from your urgument i think she might be having high cholestarol. now tell me from medical point of view what shuold we do to help her?
   
 9. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #9
  Apr 21, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  @gfsonwin stress inachangia sana kutokana na hali ya ugumu wa maisha ya Binadamu na Mataizo ya kifamilia . Kwa ushauri wangu watu wenye hali ya hii stress ningeshauri wawe na marafiki zao wapenzi kila wakati na kuwapa maneno mazuri na ushauri mzuri kuliko kuwaacha upweke kunaweza kusababisha hatari ya Mtu kujiuwa kwa kukusudia. mimi Watu wenye matatizo kama haya ya stress ninawaita watu wenye matatatizo ya Saikolojia

  Kujifahamu

  Hakuna mtu wa jana, leo au kesho aliye sawasawa na mwingine: kila mmoja ni wa pekee. Mungu ametufanya tofauti ili tutimilizane. Kila mmoja anahitaji wengine, na kila mmoja ni muhimu kwa wenzake. Katika maisha ya jamii kuna sehemu ambayo yeye tu anaweza

  kuijaza. Wazo hilo linaweza kumsaidia kijana ambaye ni mwepesi kukata tamaa na kujitupa. Daima uhai ni zawadi nzuri kwa mhusika na kwa wenzake wote. Kijana ni zawadi yenye nguvu na wema hata kwa [[taifa, kiasi kwamba kujali ustawi wa kijana ni kujenga taifa.

  Tunataka kujifahamu tulivyoumbwa (mwili, nafsi na roho, ambavyo vyote vinafungamana ndani mwetu): 1. ili tuweze kujithamini hasa kwa kuona sisi ni nani mbele ya Mungu; 2. ili tufahamu mipaka yetu na kuikabili inavyofaa; 3. ili tufahamu vipawa tulivyojaliwa tuwashirikishe wenzetu; 4. ili tubadilike kuwa bora zaidi na kuchangia ustawi wa jamii; 5. ili tuhusiane vizuri zaidi na wenzetu; 6. ili tuweze kujieleza kwa watu fulanifulani na kupata mashauri ya kutufaa.

  Kujikubali


  Daima ni muhimu tukubali hali ilivyo, halafu tujitahidi kuifanya bora zaidi. Tusipojikubali kwanza tutahangaika tu hata kukata tamaa. Wajue wasijue vijana wapokua wanashindwa kujikubali walivyo. Pengine wanaficha silika zao wasitambulikane na watu, hata

  wakashindwa kujielewa, wakapatwa na vilema vya ukuaji pia. Ni lazima waache kujifunika uso kwavinyago hivyo; badala yake wakabili ukweli wao, wenye sifa na kasoro. Hivyo tu watapitia vizuri mabadiliko ya ujana upande wa mwili, nafsi, jamii, maadili na roho. Hatimaye

  watakomaa na kushika nafasi yao maishani. Kwa kila mtu ni muhimu kuwa na marafiki; hasa kijana anahitaji kikundi. Lakini hiyo isiwe njia ya kukwepa nafsi yake mwenyewe wala ya kuficha tabia yake kwa kuzungumza, kutembea au kutenda namna fulani wanavyofanya wenzake. Kwa hiyo asijifananishe nao. Kila mtu anakua kwa namna yake, akibadilika kwa kiasi tofauti na muda tofauti. Ni lazima

  ajifunze kuyapokea mabadiliko hayo pia yanayomfanya geugeu sana, hasa msichana katika mzunguko wake wa kila mwezi: mara anaonekana jasiri au korofi, mara amejaa wasiwasi.


  Kujistawisha


  Uhai unasukuma kiumbe chochote kistawi. Mimea inakua namna yake, wanyama namna yao, na binadamu polepole zaidi kwa kuwa ndiye kiumbe bora anayehitaji kukomaa pande zake zote. Kulingana na haja yetu ya kukomaa hivyo, sio tu kufikia umri au kimo fulani,

  ndani mwetu zimo nguvu zinazotuhimiza tujilinde ili tuzidi kuishi wenyewe, tuendeleze uhai tulionao kwa kuzaa, tujitegemee (yaani tumiliki maisha yetu), tutawale vitu na watu ili mambo yaende tunavyotaka, n.k. Haja iliyoota mizizi mirefu ndani mwetu ni ile ya

  kujikamilisha tusiwe watu wanaoishi ili mradi tu. Kadiri tunavyokua tunajisikia kuwajibika. Haja hizo zinafanya tujiwekee pia malengo katika utendaji. Basi, baada ya kujifahamu, kila mmoja wetu achague na kuazimia awe bora vipi, kwa sababu wenyewe tunaamua

  tuweje. Ni wajibu wetu kujipenda na kwa hiyo kujitunza na kujistawisha kimwili, kinafsi, kijamii, kimaadili na kiroho. Kazi hiyo inahitaji nia na bidii za kudumu. Tufuate taratibu za kulinda afya ya mwili, heshima ya mavazi, usafi wa mazingira. Tujiepushe na uvivu

  unaosababisha mawazo na matendo mabaya. Tujihadhari na maandishi, picha na maneno yasiyofaa, yasije yakatupotosha kimawazo au kusisimua ashiki. Tuhusiane vema na wengine (adabu, lugha nzuri n.k.). Hasa tufuate dhamirina kustawisha roho iliyo sehemu bora

  ya utu wetu ambamo tunashirikiana na Mungu. Mbali ya motisha kutoka nje (yaani kupewa tuzo au adhabu), sisi binadamu tuna maarubuyanayotuongoza kwa ndani na kututia nguvu tutende namna fulani na kukwepa mambo mengine. Yanaweza kuwa ya aina

  mbalimbali: 1. tusiyofundishwa kwa kuwa ni haja za mwili(kupumua, kunywa, kula, kujisaidia, kupumzika, kutumia jinsia n.k.) au haja za nafsi (kupendwa, kufungamana, kukubaliwa, kufanikiwa, kujitokeza, kusaidia, kushindana, kushinda, kutawala, kujihami, kuwa salama,

  kuongozwa, kujishusha, kujitawala, kumiliki, kupanga, kubadili, kujua, kuhemka, kujamiiana, kucheza); 2. yaliyorithiwa kwa wazazi na ukoo (silika,maelekeo, vipawa n.k.); 3. ya kujipatia, yaani tusiyozaliwa nayo, ambayo tunayapata maishani mwetu hasa kutoka kwa watu wanaotuzunguka (mazoea, mila, tunu, imani n.k.). Maarubu hayo yanasaidia kukua na kuelekea ukomavu, yaani hali ya kuwa jinsi Muumba alivyokusudia kisha kupitia hatua kadhaa.
   
 10. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #10
  Apr 21, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  @gfsonwin Mama yako ana miaka mingapi?
   
 11. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #11
  Apr 21, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,963
  Likes Received: 1,841
  Trophy Points: 280
  ana miaka 57
   
 12. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #12
  Apr 21, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Kinga na tiba ya ugonjwa wa kiharusi (Stroke)

  --------------------------------------------------------------------------------


  Kiharusi ni ugonjwa mkali wa mishipa ya damu kwenye ubongo unaohatarisha vibaya afya na maisha ya binadamu. Takwimu husika zimeonesha kuwa, kila mwaka watu milioni 1.5 wanapatwa na ugonjwa huo nchini China, na nusu kati yao wanakufa kutokana na ugonjwa huo, na watu wengi wanaopona wanapoteza uwezo wa kufanya kazi kwa viwango tofauti. Hali hiyo imesababisha mzigo mkubwa kwa familia na jamii.

  Mzee Wang Qinmei mwenye umri wa miaka 65 ana afya njema na hakuwahi kupatwa magonjwa makubwa. siku moja asubuhi katika majira ya mchipuko mwaka huu, alienda sokoni kwa baisikeli kununua chakula kama kawaida, ghafla alijisikia kizunguzungu na akapoteza fahamu. Baada ya muda mfupi, alipata fahamu na kuomba msaada kutoka kwa wapita njia na akapelekwa hospitali.

  Katika chumba cha huduma ya kwanza, daktari alithibitisha haraka ugonjwa uliompata mzee Wang. Daktari wa upasuaji wa mishipa ya damu kwenye ubongo katika hospitali ya 301 ya jeshi la ukombozi wa watu wa China Bw. Wang Jun alisema:

  "baada ya kumfanyia upimaji wa CTA, tuligundua sehemu moja nyembamba katika mishipa mikubwa ya damu iliyoko shingoni, na asilimia 90 ya sehemu hiyo ya mishipa ya damu imezibwa. Hali hiyo ni ya hatari sana."

  Tatizo la wembamba wa mishipa ya damu ya shingoni ni chanzo kikubwa cha ugonjwa wa kiharusi wa aina ya kukosa damu kwenye ubongo. Asilimia 60 ya wagonjwa wa ugonjwa huo wanatokana na tatizo la kuzibwa kwa mishipa ya damu ya shingoni. Pamoja na kuzidi kuziba kwa mishipa ya damu, dalili za ugonjwa huo zinaonekana kidhahiri na wazi zaidi, hatimaye zinasababisha kiharusi kibaya. Kwa kuwa asilimia 90 ya mishipa ya damu ya shingoni inakuwa imeziba, hali hiyo inaufanya ubongo ukose damu na oksijen, na dalili mbalimbali za ugonjwa huo zote zinasababishwa na tatizo hilo.

  Mbali na kiharusi cha kukosa damu kwenye ubongo, aina nyingine ni kiharusi cha kutokwa damu kwenye ubongo. Chanzo kikubwa ni shinikizo kubwa la damu linalosababisha mishipa midogo ya damu kwenye ubongo ivimbe na kupasuka.

  Kwanza, ugonjwa wa kiharusi unahusiana na umri na jinsia. Kwa kawaida, watu wenye umri wa zaidi ya miaka 55 wana hatari kubwa zaidi ya kupatwa na kiharusi, na hatari ya kupatwa ugonjwa huo kwa wanaume ni asilimia 50 zaidi kuliko wanawake. Ya pili, ugonjwa huo ni wa kurithi. Aidha, magonjwa ya shinikizo kubwa la damu, kisukari, tatizo la moyo, tatizo la kuwa na uzito kupita kiasi, kuvuta sigara na kunywa pombe zote zinaweza kusababisha kiharusi.

  Kwa kawaida, kuna dalili kadhaa zinaonekana kabla ya kutokea kwa kiharusi. Mkurugenzi wa idara ya upasuaji wa mishipa ya damu katika hospitali ya 301 ya jeshi la China Bw. Li Baomin alisema:

  "kabla ya kutokea kwa kiharusi, mgonjwa hujisikia kizunguzungu, mwasho kwenye mikono na miguu, na kutoona vizuri. Baada ya muda, hisia hiyo itaisha au itarejea tena. Kama una dalili hizo, ni lazima uchukue tahadhari."

  Bw. Li alisema, kama dalili hizo zinatokea mara kwa mara katika siku moja au mbili, na pia una shinikizo kubwa la damu au ugonjwa wa kisukari au ugonjwa wa kurithi, unapaswa kwenda hospitali mara moja kufanyiwa uchuguzi. Hivi sasa, ugonjwa wa kiharisi unaweza kuthibitishwa mapema na kwa usahihi.

  Basi kama wagonjwa wakipatwa na kiharusi nyumbani au kwenye sehemu za hadhara tutafanyaje? Watalaamu wanaeleza kuwa, kiharusi kinatokea ghafla, wagonjwa wanaweza kupoteza fahamu, kuanguka, kutikisika au kushindwa kuongea. Watu huchanganyikiwa wakati hali hiyo ikitokea, na hata wanakuwa hawajui la kufanya. kwa kawaida, watawaamsha hata kuwatingisha wagonjwa. Vitendo hivyo vinaweza kuwadhuru wagonjwa hao, hata vinafanya hali yao iwe mbaya zaidi.

  Kama mtu akipatwa kiharusi, kwanza jamaa zake wasihangaike, bali wanatakiwa kumtuliza mgonjwa, na ni afadhali wasimwamshe alipo, lakini wanatakiwa kumwita daktari mara moja. na ni bora walegeze nguo za ndani za mgonjwa, hatua hiyo inamsaidia mgonjwa kupumua bila tatizo. Kama mgonjwa akitikisika, hali hiyo ni mbaya, ni lazima wamshtue. Kwa kuwa wakati huo, mgonjwa anaweza kujiuma ulimi, hivyo ni afadhari wazibe mdomo wa mgonjwa kwa nguo. Wagonjwa wengi wa kiharusi wanatapika, ili kuzuia wagonjwa kama hao wasijizibie koo, ni bora kuwalaza shingo upande. Kama matapishi yakibaki mdomoni, ni lazima yatolewe mdomoni kwa vijiti, na kama mgonjwa huyo ana meno bandia, inapaswa kuyatoa ili yasije yakaingia kooni.

  Zamani ugonjwa wa kiharusi ulikuwa unatibiwa kwa upasuaji, hivi sasa unatibiwa kwa matibabu yenye usalama, ufanisi na rahisi zaidi. Matibabu hayo ni kuingiza mrija mdogo kwenye mshipa mkubwa wa damu wa pajani na kuifikisha kwenye sehemu yenye tatizo mwilini na kutibu. Kwa kuwa kipenyo cha mshipa mkubwa wa damu ni milimita 15 hivi, na kipenyo cha mirija ni milimita 2 tu, hivyo mrija huo unaweza kupita kwenye mishipa ya damu bila tatizo. Mbali na hayo, kutokana na kuwa hakuna nevu za hisia ndani ya mishipa ya damu, basi wagonjwa hawasikii maumivu.

  Mzee Wang Qinmei alitibiwa kwa matibabu hayo. Daktari aliweka chombo maalum cha kupanua mshipa wa damu ndani ya sehemu ya mshipa mkubwa wa damu wa shingoni kwake iliyozibwa kwa kutumia mirija. Mzee Wang alisema:

  "Baada ya kuwekewa chombo cha kupanua mshipa wa damu, nilisikia damu inapita vizuri, ghafla hisia ya kizunguzungu iliondoka mara moja."

  Matibabu hayo hayahitaji kuwapa wagonjwa nusukaputi ya mwili mzima. Wagonjwa wanaweza kutibiwa wakiwa na fahamu vizuri. Pia kwa kuwa matibabu hayo yanaleta majaraha madogo tu, basi wagonjwa wanaweza kutembea saa 24 tu baada ya matibabu. Hivi sasa, wagonjwa wengi zaidi wa kiharusi wanachagua matibabu hayo.
   
 13. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #13
  Apr 21, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  @gfsonwin nikikufundisha Dawa zangu za Tiba Mbadala yaani Dawa za Kienyeji utaweza kumfanyia Mama yako ili aweze kupona ?
   
 14. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #14
  Apr 21, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,963
  Likes Received: 1,841
  Trophy Points: 280
  Dr, umeeleza vizuri sana juu ya stree mimi naomba kuchangia kidogo hapo.

  Vijana wengi wamekuwa wahanga wa strees hasa kwa miaka hii. Sababu yake kubwa ni kwamba msukumo rika umekuwa ukiwatawala kuliko utashi wa mtu binafsi. Mathalani, kama ulivyosema ni rahsi sana kumkuta kijana analinganisha maisha yake na ya mwenzie wa umri kama wake na akatamani vitu fulani kutoka kwake ama akatamani vitu alivyo navyo mwenzie. sasa maisha yasipo mruhusu kuwa navyo kijana huyu lazima ataangukia kwenye lindi la mawazo ambalo yamkini halina majibu kwa wakati huo. kitu ambacho huamsha maswali mengi kichwani mwake yanayokosa majibu ya moja kwa moja. Hali hii humfanya kijana anyong'onyee na kuona hta wale wa karibu yake hawampendi au hawamsaidii.

  kwa jambo kama hili nafikiri suluhu yake ipo ndani ya kijana mwenyewe,kwamba aone kila siku huwa tunajifunza kupitia wenzetu, lakini huwa kamwe hatuigi maisha yao. usilinganishe maisha bali jifunze kutokana na maisha. kijana anapaswa amwone mwenzie kama ubao tu lakini kamwe siyo kama kanuni fulani kwenye maisha.

  Jambo jingine ninaloliona ni mwenendo mzima wa maisha. Mara nyingine maisha hayampi mtu yale anayoyataka, na hii ni kawaida wala huwezi kulazimisha. Hali hii inapomkuta mtoto mdogo huwa haimuumizi sana kwani anaweza asiielewe, au asijali au hata akiumia ikawa ni kwa muda tu kisha akasahau. Vilevile hali hii inapomtokea mtu ambaye ni mzee wala hatojali atasema ni kawaida, tofauti huwa ni kwa kijana ambaye huwa inamuumiza. Hii ni kwasababu kijana huwa vitu vingi anavyovitaka ni vya kumuendeleza kimaisha. sasa hapa anapokosa anaona kabisa siwezi kuendelea kwa staili fulani kwasababu kitu fulani muhimu hapa nimekikosa.

  mwenye suluhu ya jambo hili siyo kijana, ila ni mwenendo mzima wa maisha au niite system of life. hii hutengenezwa na sera nzuri zinazokubalika na zinzolenga kumuendeleza kijana. pia sera zisizo mbagua kijana iwe kwa rangi, au elimu au dini.n.k

  ushauri wangu kwa vijana maisha yanapotupa machungu, tuyapokee lakini tusiyaweke nafsini mwetu kamwe, tuyaone kuwa nayo haya yatapita. na tunapopewa mazuri basi tuyapokee na kuyahifahi vizuri kwa kizazi chetu na hata cha baadae. ila tukumbuke kumshukuru mungu kwa kila jambo.
   
 15. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #15
  Apr 21, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,963
  Likes Received: 1,841
  Trophy Points: 280
  \ndiyo nitaweza.
   
 16. Habdavi

  Habdavi JF-Expert Member

  #16
  Apr 21, 2012
  Joined: Mar 5, 2011
  Messages: 393
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 45
  ahsante sana, huu ujumbe unahusu watu wengi
   
 17. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #17
  Apr 21, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,963
  Likes Received: 1,841
  Trophy Points: 280
  asnte sana wewe kwa kuusoma. ila pia na wewe weka nyama hapo ili mwisho wa siku tupate elimu kamili.
   
 18. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #18
  Apr 21, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  @gfsonwin Dawa ya kutibu Ugonjwa wa kiharusi,Baridi, Mirihi


  Huduma ya kwanza tumia, udil karaha kwa wingi,Habbat soda unga vijiko vitano,Asali vijiko vitano, Hii ni kwa ajili ya kula, Ama kwa ajili ya kupakaa ni mafuta ya zaituni vijiko viwili 1x2 wiki moja.

  b.Tiba kwa ukamilifu kwa idhni ya Mwenyeezi Mungu:
  1.Bakalhad Gramu 50
  2.manimani Gramu 50
  3.Ubani dhukra Gramu 50
  4.mustaki Gramu 25
  5.kungu Manga Gramu 25
  6.habbati soda Gramu 50
  7.sufa Gramu 50
  8.kakila Gramu50
  9.makal arzak(buma) Gramu 25
  10.basbas jauza Gramu 25
  11.halilinji Gramu 25
  12.balinji Gramu 25
  13.albinji Gramu 25
  14.tangawizi Gramu 50
  15.daarfilfil Gramu 50
  16.hiliki Gramu 50
  17.haltiti ya unga Gramu25
  18. udi karaha Gramu 50
  19.Dawa zote hizo Twanga uchekeche upate unga wake Uugawe sehemu 2 ya kwanza Utiye ndani ya Mafuta ya zaituni au mafuta ya Ufuta awe anajipakaa mwilini kila usiku anapotaka kulala na Dawa ingine uweke kwenye Asali ya nyuki mbichi kipimo cha chupa moja ya Orange. Matumizi awe anakunywa hiyo Dawa uliyo changanya na asali kwa kipimo cha nusu kikombe cha kahawa kutwa mara 1x3 atumie dawa hiyo mpaka atakapo maliza Inshaallah atapona.

  Dawa ya kumchuwa Mgonjwa wakati wa asubuhi atachuliwa kwa dawa zifuatazo: Menthol,tymol(arak zamda) juice ya kitunguu thaumu nusu kikombe cha kahawa, mafuta ya zaituni kikombe cha kahawa koroga sawa sawa Mchuwe kila siku kutwa mara 1x2 kwa muda wa mwezi mmoja. Dawa zinapatikana sokoni kariakoo kwa wauza Madawa za kiarabu wapemba wa mtaa pemba au ulizia watu watakuonyesha wapi hizi dawa zinapatikana hapo Dar Tumia Dawa zangu kisha unipe feedback.
   
 19. Michael Amon

  Michael Amon Verified User

  #19
  Apr 21, 2012
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 8,741
  Likes Received: 707
  Trophy Points: 280
  Ngoja kwanza nikapate breaksfast halafu nitarudi tena kuisoma hii mada.
   
 20. vicent tibaijuka

  vicent tibaijuka JF-Expert Member

  #20
  Apr 21, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 276
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  stroke can be caused by hemorrhage or thrombus in the brain. Hemorrhage is due to hypertansion, but trombus can be caused by cancer, arteroscelerosis etc. let her undergo more medical exam.
   
Loading...