Chakaza
JF-Expert Member
- Mar 10, 2007
- 40,948
- 74,431
Taarifa ya TBC1 kuhusu kukatwa mapanga na mashoka kwa Mbunge wa Ilemela na yule wa Ukerewe imetuacha na maswali mengi. Tukio hilo ni kubwa na la aina yake kutokea katika nchi hii tokea tupate uhuru. Inakuwaje TV ya taifa waripoti swala hili kama tukio la kawaida lisilo na uzito wowote katika jamii? Au kwa vile ni wabunge waupinzani? Nchi inayojitapa kuwa ya amani na utulivu na wabunge wanapigwa mapanga na mashoka tunaenda wapi? Hoja jee kituo cha TV cha taifa kinapo dharau jambo kama hili maana yake nini katika mustakabali wa Taifa?