shamba linauzwa

Vkindu ni kubwa au sio.....whereabout in vikindu mkuuu???Lazima tukubali wabongo tuna kauvivu fulani vile.Tangazo gani hili la biashara???Au ndo shule zetu!!!
 
Shamba la eka moja linauzwa maeneo ya vikindu.

je, liko karibu na barabara kuu (main road)?
lina mimea yo yote ya kudumu (minazi, mikorosho, n.k.)
jirani pande 4 zote hawana kero za mipaka?
linauzwa bei gani?
 
Mbona hujaweka Bei? Lina Barua ya kijiji au Hati ya Ardhi? Na huko vikindu ndo wapi tena? Mbagala au?????
 
nafikri kweli hiyo sio tangazo la biashara ulitakiwa kutoa maelezo yote yanayoweza kumshawishi mtu kama eneo lilipo, mimea, nk
 
Ngoja nitoe maelezo vizuri.
Hili shamba lipo vikindu maeneo ya mbagala, lipo off kilwa road like 15 mins by feet from the main road. Halina tatizo lolote kuhusu mipaka. Lilinunuliwa kipindi serikali ilipogawa viwanja maeneo hayo.Hivyo swala la hati halina tatizo.
Mazao yaliyomo humo ni migomba, mihogo, na minazi. hiyo sehemu ina rutuba poa kabisa.
Bei ni 2,000,000Tshs.(2 milioni)
 
Vkindu ni kubwa au sio.....whereabout in vikindu mkuuu???Lazima tukubali wabongo tuna kauvivu fulani vile.Tangazo gani hili la biashara???Au ndo shule zetu!!!
sikufundishwa kuandika tangazo la biashara skul. si unajua tena skul za chini ya mwembe
 
mmmmh!!!!! haya umetoa maelezo BUT how about your contacts??????yaani na hivi vitu ni lazima ufundishwe shule???Au ni uvivu tu wa kufikiri???kweli tuna kazi ngumu kuelimishana na ndio maana Dar es salaam wabunge wengi ni CCM.......bcos mambumbumbu ni wengi hapo.
 
Contacts mbona hujaweka??unatoa maelezo nusu nusu???Kweli wabongo ni wavivu wa kufikiri alijisemea BWM.....au napo unataka kusema lazima ufundishwe darasani???Ndio maana Dar wabunge wengi ni CCM kwani mambumbumbu nao ni wengi kuliko hata Tarime.
..........ndio hiyo.
 
Correct English should be "approximately 15 mins on foot" - JF tunaelimishana sio kukosoana.


Wewe ndio mwenye shamba, nokoa au middle person? Kwa ye yote anayehusika, tupatie contact yake - simu au barua pepe.
mimi sio mwenye shamba, mwenye shamba ni my sibling, anatafuta mteja hivyo nikaona bora niweke hapa JF tangazo. kama unahitaji kweli nitumie PM.
 
Extra care is needed, u stand for your sibling na hutaki kutoa contact details, kwa nini umeweka tangazo?, nachelea kusema labda ni kautapeli fulani. Be open by disclosing everything that will make easy communication. Wajua migogoro ya mashamba/viwanja kwa bongo ni mingi sana!
 
Jamani nielewesheni, eka moja ni shamba au ni kiwanja?? Nashauri sema kiwanja chenye square metre 4,900 kinauzwa shilingi 2,000,000/=. Pretty kama kuna la kuanzia eka 5 na kuendelea nitumie kwenye pm kabisa.
 
Jamani nielewesheni, eka moja ni shamba au ni kiwanja?? Nashauri sema kiwanja chenye square metre 4,900 kinauzwa shilingi 2,000,000/=. Pretty kama kuna la kuanzia eka 5 na kuendelea nitumie kwenye pm kabisa.
mimi ninalo la ekari 18 lipo vikindu (vianzi)manyani bei ni 35,000,000/ ni pm tuongee
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom