Plot4Sale Shamba linauzwa Kibaha Mnemela Kibaoni

Gily Gru

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
7,812
20,872
Habari wadau,

Kuna mama mmoja anauza eneo kibaha mnemela umbali kilometer saba kutoka hospital ya tumbi. Eneo nimeenda kuliangalia leo huko, maeneo ya kibaoni, mbele ya Boko Mnemela. Eneo ni tambarare na lina ekari mbili kasoro kidogo kutokana na kuweka njia kidogo pembeni ukingoni mwa eneo.

Eneo hili lina miembe miwili, mikorosho miwili bahati mbaya leo mmoja tumekuta umeanguka, kuna pia mpera na mti mwingine ambao nimeshindwa kuutambua. Hili eneo lina maandikishano kutoka serikali ya kijiji, ila jirani wa karibu kapima nimesahau tu kupiga picha ya mawe yake ila yamepakana na eneo lake.

Huyu mama anauza hili shamba kwa sababu mumewe anaumwa na yuko ocean road anahitaji hela kwa ajili ya operation. Pia unaweza kumtembelea nyumbani kwake kumuona Yombo, pamoja na mumewe aliyerudishwa nyumbani baada ya kupungukiwa na hela. Hata hivyo anapokea malipo nusu ili aendelee na operation kwanza na mnunuzi atakubaliana nae malipo in installments mpaka atakapomaliza kulipia. Mama yuko teyari kabisa kwenda mahakamani au kwa mwanasheria.

Nisiwachoshe, kwa bei anayouza ni million 12. Karibu na hapo alipo kuna wafugaji in fence ya ukuta. Pia kuna viwanda viwili kimoja cha maziwa cha mwarabu, kingine kimenitoka kichwani kidogo sorry.

Mimi sio dalali wala sihitaji mtu anifate PM mambo yawe wazi. Ila number za bi mkubwa ni 0715875810 na 0754875810. Anaitwa mama Kimasiko (mtu mzima kidogo), kama uko interested mchekini kwa mawasiliano niliyoorodhesha hapa.

Shukrani na Usiku Mwema.

PIA MWEZI WA HERI HUU KAMA KUNA MTU ANATAKA KUMTEMBELEA NA MUMSAIDIA MZEE ANAYEUMWA AMTAFUTE HUYU MAMA ANAKAA YOMBO. PIA UKIHITAJI KUMTUMIA MSAADA MPIGIE AU KAMTEMBELEE NYUMBANI. SINA UNDUGU NAE KABISA SIO UTAPELI NA SIJAWEKA NUMBER ZANGU HAPA NIMEWEKA NUMBER ZAKE.





 
Karibuni wateja wanaotaka kununua shamba mkoa wa pwani. .

LAKINI HATA KUMPIGIA KUMJULIA MGONJWA HALI PIA NI SAWA, HATA KAMA HUTAKI KUNUNUA. .
 
Mungu amsaidie apate pesa ya matibabu afya yake itengamae.
 
Hicho kiwanja shamba limepimwa na ana hati?
 
Hicho kiwanja shamba limepimwa na ana hati?
Please do ask her
Ila kwa maelekezo yake anapokea hela kwa awamu na wenzake walipima yeye hakupima. Ila ana maandikishiano na mashaidi wako pia, pamoja na majirani
 
Karibu na mitoboto??

Na hauzi heka 1??
Ndugu mie nimemsaidia kumpostia tu online ndo mana nikaweka number zake, muulizeni yeye zaidi

Ila kwa shida ni kupata hela ya kumfanyia ume wake operation, natumai atauza
mcheki kwa number zake 0715875810 na 0754875810
 
Mungu amsaidie apate pesa ya matibabu afya yake itengamae.
Kwa maelekezo ya huyu mama huyu mzee kaumwa mda mrefu sana, sasa anahitaji hela ya kuanzia million 3.5 ili afanyiwe operation. .

Ndo mana anahitaji kuuza hili shamba liweze kuwawezesha dawa na hospitali na anapokea by installments na yuko teyari kuandikishana kwa mwanasheria au mahakamani. .
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…