Shamba la Sumaye kufutiwa hati

Tatizo la kufanya mambo kwa ushabiki. Tz kuendelea bado sana. Tuna umaskini wa fikra.
 
Hivi serikali imeliona Shamba la Sumaye tu kule Mabwepande? Mbona kuna watu wana maeneo makubwa wamepima viwanja havijaendelezwa ni mapori wanasubiri kuviuza lakini hawanyang'anywi Kwa kuwa wako CCM?
Yes. Hilo umeuliza kama swali lakini ndio jibu sahihi. N hata Sumaye mwenyewe anajua kwani wakati akiwa CCM aliwahi kusema ''ukitaka mambo yako yakunyookee jiunge na CCM''. Maskini hakujua kama anajikaanga mwenyewe
 
Kumbe madkteta wote hufanana tabia, jpm kama m7 kwa dr kiiza
 

Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi inakusudia kufuta umiliki wa shamba la Waziri Mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye lenye ukubwa wa heka 33 lililopo Mabwepande mkoa wa Dar es Salaam.


Hatua ya kufutiwa umiliki wa shamba hilo imetokana na agizo la Rais Dk.John Magufuli la kutaka maeneo yote ambayo hajaendelezwa na wamiliki kunyang’anywa na kugawiwa kwa wananchi.


Kauli hiyo ya Rais Magufuli iliwachochea wananchi zaidi ya 100, wakiwamo waliobomolewa nyumba maeneo ya mabondeni jijini Dar es Salaam, kulivamia shamba Sumaye na kujikatia viwanja.


Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya makazi, William Lukuvi alisema tayari wametoa notisi ya siku tisini ya kulifutia hati shamba hilo kutokana kukaa muda mrefu bila kuendelezwa.
chanzo:mtanzania
 
Wanampiga mikwara tu,hawawezi,ni vitisho,vya panya,na kwa paka
 
Tunakushukuru Mhe Rais kwa uzalendo unaonyesha kwenu walla hoi dhidi ya makabaila na mabwanyenye wachache walikuwa wanatudanganya eti wanamabadiliko na watetezi wetu wanyonge kumbe matapeli.

Tunakuomba kwa mungu baba utufungulie zaidi na sisi tupate maendeleo. Tumenyonywa sana inatoka sasa.
 
Una mshukuru huyu rais aliesema analipwa million 9 kumbe million 442 kwa mwaka.
 
Hakika Magufuli ni Taisi wa wanyonge. maana inchi walikuwa wameigawana kihuni kabisa. inawezekaneje mtu mumoja kuwa na eneo hilo lote?? kama sio wizi? Big up Magufuli.
Wanyonge wepi?[emoji15] Unaongelea huyu huyu aliempa mdogo wake nyumba ya serikali. Wacha kumfananisha shetani na malaika
 
Naunga mkono hoja Tuendelee mpaka kwa Ben Yale mashamba ya miwa mtibwa na kagera
Tatizo ni tafsiri. La Ben ni shamba kwa kuwa lina miwa, hivyo limeendelezwa, haliwezi kufutwa. La Sumaye, hati inasomeka shamba lakini eneo ni pori. Hajapaendeleza. Hivyo anafutiwa ili wapewe wananchi wenye uwezo wa kupaendeleza
 
wajiandae na wao kuwa wapinzani na kurudisha nyumba zetu za oysterbay na masaki zilizotupwa
 
Mr. Zero. The most corrupt and useless PM ever. Halafu naye anakimbilia CHADEMA akidhani kuwa atapata uraisi au kurudia uwaziri mkuu wake. Utafikiri CHADEMA ni chaka la kuficha na hatimaye kutakatisha mafisadi waliokubuhu. Sad!
Haha [emoji23] haha [emoji23] haha [emoji23] haha [emoji23] kweli kabisa mkuu. Kama sio msafi ukikimbilia Chadema imekula kwako. Na ndio maana wale wafanyabiashara walivyoona kama akuna matumaini ya Ukawa kuchukua Dola wamerudi tena CCM.
 
Viongozi wengi sana walijitwalia Mashamba, au wanaanza kwanza na Sumaye kama alivyosema wanaanza kwanza na Mbowe japo wapo wengi, lakini mpaka leo sijasikia yoyote mkubwa akitolewa vitu vyake National Housing. We need to think big.
Chuki inajengwa taratibu na serikali. Ukiwa chama tofauti unanyanyaswa
 
Naunga mkono hoja Tuendelee mpaka kwa Ben Yale mashamba ya miwa mtibwa na kagera

Muwage na akili hapa yanazungumziwa mashamba pori ambayo hayaendelezwi ndio mana rais alisema kama wanayataka wayalime usiku na mchana sasa hayo ya Ben ya miwa sasa huon kama yanaendelezwa


TATIZO LENU MNAPENDA KU COMMENT NA KU LIKE HAMPENDI KUTAFAKALI
 

ndo nini hapa tena.
 
Asilielie...hata mwaka jana akiwa bado CCM mkewe Ester alifutiwa umiliki wa maelfu ya ekari mkoa wa pwani ambayo hakuwahi kuyaendeleza...huyu mtu ni mlafi wa ardhi pasipo kuiendeleza,hana tofauti nayule muhindi/muingereza aliyefutiwa jana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…