Shamba la mifugo la Utegi

Shamba la mifugo la Utegi

Koryo2

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2016
Posts
2,056
Reaction score
2,523
Mhe. Rais, kwanza kabisa sisi wananchi wa Vijiji sita vya UTEGI, MIKA,OMUGA, NYANDUGA na INGRI kwa kifupi (UMONI) tunakushukuru sana kwa kulitolea ufafanuzi na uamuzi kuhusu shamba la mifugo la Utegi katika ziara yako ya kutembelea Mkoa wa Mara.

Pamoja na kutotembelea Wilaya ya Rorya kwa sababu ya kubanwa na ratiba tulitarajia Mhe. Mbunge wa Rorya angetoa taarifa juu ya shamba hili wakati alipopewa nafasi ya kusalimia wananchi na kueleza changamoto zinazokabili Jimbo lake lakini kinyume chake hakufanya hivyo. Kwa ufahamisho wako Mhe. Rais Mbunge wetu ni rafiki mkubwa wa Ndugu Otieno Igogo na katika miaka yote ya Ubunge wake ameshindwa kupata ufumbuzi wa Shamba hili licha ya sisi wananchi kumtuma kufanya hivyo.

Mhe.Rais nina mifano michache tu kuhusu hujuma alizofanya Ndugu Otieno Igogo katika Shamba hili.

(1) Wakati Serikali inawapa Vijiji hivi sita shamba hili kulikuwa na ng'ombe zaidi ya 600 (Mia sita) aina ya chotara. Leo hii shamba lina ng'ombe wapatao 30 (thelathini) tu. Kwa akili ya kawaida hawa ng'ombe kufikia sasa toka 2005 wangekuwa zaidi ya ng'ombe 2000.

(2) Kuna kiwanda cha maziwa katika Shamba hilo. Kiwanda hiki kulikuwa na mashine za kutengeneza maziwa ya unga, samli na mashine kubwa za boiler. Mashine hizi zote ziling'olewa na zingine ziliuzwa Bukoba kwenye kiwanda cha mtu binafsi ya kahawa na zingine ziliuzwa nchini Kenya.

(3) Katika shamba hili kuna mlima uitwao Koryo na ndiyo chimbuko la jina la Kata ya Koryo. Katika mlima huu kulikuwa na miti mingi ya asili mikubwa kwa ajili ya mbao. Miti yote amvuna na kupasua mbao. Mlima huo sasa umebaki kama jangwa.

(4) Amesomba mawe yote yaliyokuwa kwenye mlima Koryo akiwauzia wafanyabiashara wa Tarime kwa tripu moja ya mawe Tshs.70,000 (Elfu sabini) na shughuli hii imefanyika tangu alipochukua shamba hili mpaka leo.

(5) Amediriki kuwauzia wananchi maskini wanauozunguka shamba hili hata majani ya kuezekea nyumba zao za kienyeji ili hali shamba ni la kwao.

Mhe. Rais sisi wananchi wa Vijiji sita hatuna ugomvi na Ndugu Otieno Igogo lakini tunachotaka aturudishie gharama zote za mali alizopora kutoka kwenye shamba hili. Hesabu ifanyike ili kujua gharama halisi ya hasara iliyopatikana.

Mhe. Rais, tumekubali wewe ni Rais wa wanyonge. Tumefuatilia na kupiga kelele sana juu ya shamba hili na hasa katika awamu ya nne bila mafanikio yeyote huku akitamba kuwa hatuwezi kumfanya lolote lakini katika utawala wako Mhe. Rais tumepata ukombozi sisi wanyonge. Mhe. Rais Mungu akutangulie katika uongozi wako na sisi tuko nyuma yako kwa asilimia mia moja.

Mhe. Rais pia tunamshukuru sana Mkuu wa Mkoa Ndugu Malima kuwa karibu na sisi katika kulifuatilia suala hili ili sisi wananchi tupate haki yetu.

Mhe. Rais mwisho nimshukuru Ndugu A.Kuhanda Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Mara. Binafsi namfahamu. Ni mmojawapo Makamanda Mahiri,mwadilifu na mchapa kazi. Ameongoza Mikoa ya Manyara, Kilimanjaro na sasa Mara. Makamanda kama hawa wanatakiwa wafikiriwe. Amefuatlia sana suala la shamba hili na hatimaye sasa tunakaribia kulipatia ufumbuzi.
Mhe. Rais Mungu akubariki sana katika majukumu yako ya kuwakomboa wanyonge kwa asilimia kubwa. Mungu akubariki sana.
 
Ni kweli maeneo haya yangelirudishwa katika vijiji ulivyovitaja. Ni uonevu wa hali ya juu kuvinyang'anya vijiji vyote hivi maeneo ya mashamba na malisho, kwa ajili ya kiwanda kilichokwisha kujifia.

Lakini nilimnukuu mh. Rais ni kuwa bora shamba hili angelikabidhiwa mh. Lakairo (mbunge). Na natumaini kwa Tz yetu hii kauli ya Rais ni amri na sheria.
Sasa tumemruka Otieno Igogo na kuangukia kwa Lakairo [emoji40] [emoji87]. Ukweli wa shamba hili ilitakiwa iundiwe tume ije na majibu, badala ya matamko ya mtu moja. Hii Italeta tena mgogoro mkubwa zaidi.
 
Jana nimesikia hati za umiliki zimekabidhiwa sasa kama kuna hili la uuzaji wa mashine na ufisadi mwingine wa namna hiyo basi Kangi Lugola aje kuchukua wateja wake apeleke mahakama ya mafisadi.
 
Back
Top Bottom