Chukulia wewe na kaka yako mmerithi shamba kubwa sana la kahawa. Humpendi kaka yako unatamani afe ili shamba libaki mali yako.
Siku moja ukagundua kaka yako amekodisha kwa mzungu shamba lote. Mkataba wa miaka 99 na hela zote za mkataba ameshazitumia. Sasa kaanzisha purukushani za kuvunja mkataba.
Na unajua mkataba huo kuuvunja kisheria itachukua muda mrefu sana na kutakuwa na fine kubwa za kulipa. Na kuna uwezekano wa mzungu kuhujumu hilo shamba kwa hasira.
Wewe utashirikiana na kaka yako kuvunja huo mkataba kinyume cha sheria au kwa sababu humpendi kaka yako, utajipendekeza kwa mzungu abaki na shamba huku ukimtishia kaka yako kuwa atashtakiwa akivunja mkataba.
Inategemea, ila kama kaka hashauriki ina maana kushirikiana naye ni kazi bure. Bora kukaa upande wa mzungu ili kuzuia uharibifu na kuokoa mali ya urithi kwa maslahi mapana ya kizazi cha ukoo wetu.