Bujibuji Simba Nyamaume
Platinum Member
- Feb 4, 2009
- 78,123
- 165,988
Shalom!
Unaendeleaje?, asubuhi ya leo nilikuwa natafakari, Yoh15; Yesu anasema mimi ni mzabibu,
Yeye ni Mzabibu na sisi ni matawi, tawi linalozaa hulikatia vizuri, na lile lisilo zaa hulikata na kutupwa motoni,
Tafakari;
Ø Unamzaliaje Yesu matunda mahali pa kazi
Ø Unamzaliaje Yesu matunda ukiwa nyumbani,
Ø Watu wanao kuona wanamuonaje Yesu ndani yako,
Paulo anazungumza kitu katika rom 15:8, mahali pote alipofika alizungumza yale Yesu aliyomtendea,
Je wewe unazungumza nini ukikutana na watu wa kwenu, au marafiki, ni nini kinatoka ndani ya moyo wako,
Kile unachokisema ndicho kilichojaa ndani ya moyo wako
Maombi,
Mwaambie Bwana akupe neema ya kumzalia matunda,
Mwaambie Bwana akuumbie shauku/kiu ya kutaka kumjua yeye,
Mahali ulipo ni yeye aliyekupeleka, muuliza kusudi la kuwepo hapo ni nini?
Nakuombea Mungu aiumbe Roho ya uchaji ndani yako
Barikiwa