Shaka Ssali: Tatizo ni wananchi sio watawala

chikub

Senior Member
Joined
Oct 15, 2015
Posts
110
Reaction score
28
Watawala wako kwenye ajira zao, maisha yao na familia zao yanasonga mbele hata kama yale ya wananchi wao hayasongi mbele.

Shaka Ssali anasema uzembe uko kwa wananchi wenyewe wasiofahamu namna ya kuzidai haki zao mbele ya watawala wao kwa vizingizio tofautitofauti ukiwemo woga, ukosefu wa ujasiri na ufahamu kuhusu haki zao wanazoporwa na namna ya kuzidai.

Kama vile watawala wachache wanavyotumia njia mbalimbali kupokonya haki za wengi ndiyo hivyohivyo wananchi walio wengi wanavyopaswa kutumia njia mbalimbali kuzidai kutoka kwa watawala walio wachache.
 
Na kwa mtindo huu watawala hawa wataendelea kuwaburuza wanainchi sana!
Maana wanajua kuwa wakitishia kidogo tu watu wanagwaya!
Ni hapa danganyika tu mambo haya hutokea!
 
Kama tulivyoitwa malofa na wapumbafu ni sahihi kabisa
 
Kweli aisee.Yani unakuta watu na utimamu wetu tunamshabikıa mtu hawezi kufafanua kwa ufasaha kile anachotaka kuwafanyia Watanzania.Tunashabıkıa watu ambao wana shutuma nyingi za ufısadi kana kwamba kati ya watu mili 52,ndo hao wameonekana kufaa!Hata km tuhuma hazithbitika,inatosha kuwaweka pembeni,tutafute wengne.
 
Pigeni kura kwa wingi ndio dawa yao,watu waamke mapema sana,ikibidi SAA 11 alfajiri ili wakifungua tu vituo watu wamejaa na kuisha haraka ili Zoezi la kuhesabu lianze na kumalizika mapema hata kabla ya SAA moja jioni
 
Watawala wako kwenye ajira zao, maisha yao na familia zao yanasonga mbele hata kama yale ya wananchi wao hayasongi mbele.

Shaka Ssali anasema uzembe uko kwa wananchi wenyewe wasiofahamu namna ya kuzidai haki zao mbele ya watawala wao kwa vizingizio tofautitofauti ukiwemo woga, ukosefu wa ujasiri na ufahamu kuhusu haki zao wanazoporwa na namna ya kuzidai.

Kama vile watawala wachache wanavyotumia njia mbalimbali kupokonya haki za wengi ndiyo hivyohivyo wananchi walio wengi wanavyopaswa kutumia njia mbalimbali kuzidai kutoka kwa watawala walio wachache.

YES, huu ndio ukweli wa wazi ambao hauna ubishi hata kidogo.

Wananchi wa Tanzania ndio "TATIZO", wanapata shida zote lkn hawataki kubadilika.

Ngoja CCM waendelee kubaki madarakani tu.
 
ni kweli, tatizo lipo kwetu sisi wananchi. wengi hatujiamini na tumejaa uoga. ni wachache wanajua matumizi ya ubongo kuwa sehemu kubwa ni kufikiri ili kutoa maamuzi yenye tija na kuleta ufumbuzi kwenye tatizo, wengine tumajua kukariri kaulimbiu na kufata mkumbo.
 
Wengi wanajua ya kwamba ukila wali na maharage ndio haki yako ya msingi
 
Tatizo watanzania wengi uelewa wao ni mdogo na kibaya zaidi hata wenye elimu ya chuo kikuu nao ni ni Yale Yale unakuta mtu anasema HAPA KAZI TU wakati hata kibarua hana! Huu ni ujuha wa ajabu!!!! Kingine watu ambao ndiyo wametopea kwenye umaskini ndiyo mashabiki wa CCM km ripoti ya TWAWEZA ilivyoosema! Maajabu ya Musa!

Yaani Watanzania waliojazana wengi wanaamini huduma za jamii kwao ni fadhira!

Mimi nimefanya maamuzi Kwa mke wangu bora asipige kura kabisa kwani malalamiko kibao lakini mahaba makubwa Kwa chama cha kifisadi!
 
Hiyo yote ni chimbuko la umaskini kupita kiasi, kitendo cha nyerere kutoa huduma za jamii bure na pasipo kuwafafanulia kuwa hiyo ni kodi yenu watu walidumaa wakakosa nguvu ya kudai huduma bora ndio maana hali inakuwa hivi hadi Leo.Utadaije huduma Fulani kwa nguvu na wakat hiyo huduma unapewa bure?
 
Kubadilika ni zaidi ya kutaka ccm itoke tu madarakani,kwangu mimi kubadilika kwanza ni kuacha kuamuliwa mambo na viongozi wetu wa kisiasa kwa masilahi yao wenyewe na kuyafanya ndiyo matakwa ya wananchi.
 
Watawala wako kwenye ajira zao, maisha yao na familia zao yanasonga mbele hata kama yale ya wananchi wao hayasongi mbele.

Shaka Ssali anasema uzembe uko kwa wananchi wenyewe wasiofahamu namna ya kuzidai haki zao mbele ya watawala wao kwa vizingizio tofautitofauti ukiwemo woga, ukosefu wa ujasiri na ufahamu kuhusu haki zao wanazoporwa na namna ya kuzidai.

Kama vile watawala wachache wanavyotumia njia mbalimbali kupokonya haki za wengi ndiyo hivyohivyo wananchi walio wengi wanavyopaswa kutumia njia mbalimbali kuzidai kutoka kwa watawala walio wachache.

Kwa hiyo anachotaka kutwambia Shaka Ssali ni watu kutumia nguvu kuwaondoa watawala madarakani ikibidi? Tumuulize yeye alipokuwa Luteni katika jeshi la Iddi Amin na akashiriki kwenye njama za kumpindua Iddi Amin baada ya jaribio lao kushindwa na baadae yeye na wenzie kufukuzwa jeshini, aliporudi uraiani aliendeleza vipi mikakati ya kudai haki zake (kama mwananchi na pia wananchi wenzie Uganda) kutoka kwa watawala wachache? Sana sana aliufyata kisha akatimkia zake Ujerumani na kisha Marekani.
 
Watawala wako kwenye ajira zao, maisha yao na familia zao yanasonga mbele hata kama yale ya wananchi wao hayasongi mbele.

Shaka Ssali anasema uzembe uko kwa wananchi wenyewe wasiofahamu namna ya kuzidai haki zao mbele ya watawala wao kwa vizingizio tofautitofauti ukiwemo woga, ukosefu wa ujasiri na ufahamu kuhusu haki zao wanazoporwa na namna ya kuzidai.

Kama vile watawala wachache wanavyotumia njia mbalimbali kupokonya haki za wengi ndiyo hivyohivyo wananchi walio wengi wanavyopaswa kutumia njia mbalimbali kuzidai kutoka kwa watawala walio wachache.

shaka sali amekaa Tanzania analijua hili.
 
Hayo ni ya kweli hapa nchi ya mazombi
 
Kubadilika ni zaidi ya kutaka ccm itoke tu madarakani,kwangu mimi kubadilika kwanza ni kuacha kuamuliwa mambo na viongozi wetu wa kisiasa kwa masilahi yao wenyewe na kuyafanya ndiyo matakwa ya wananchi.

Wanena vyema, maana viongozi wa kisiasa wameona sisi watanzania hatujitambui kwa hiyo waweza fanya lolote wanalotaka kufanya pasi kuhoji ni kwa maslai ya nani.
 
Watanzania tumezoea shida maana shida sisi hazitupi shida
 
Back
Top Bottom