Shaka: Heko Magufuli kwa kuipigania Zimbabwe

SautiYaMnyonge

JF-Expert Member
May 13, 2018
289
1,000
Na Mwandishi Wetu
Morogoro

Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Morogoro kimefurahishwa na msimamo idara uliotolewa na Waziir Mkuu Kassim Majaliwa kwa niaba ya serikali ya Rais Dkt John Magufuli , unaozitaka Nchi wanachama za SADC kusimama pamojao na Zimbabwe mpaka pale vikwazo dhalimu vya kiuchumi nchini humo zitakapoondolwa.

Kimesema wakati huu dunia nzima ikikumbwa na janga la kusambaa kwa virusi vya Corona huku huduma za kibinadamu zikihitajika kwa kiasi kikubwa haipendezi kuishuhudia zimbabwe ikiendelea kuwekewa vikwazo vya kiuchumi.

Matamshi hayo yametamkwa jana na Katibu wa CCM Mkoa Morogoro Shaka Hamdu Shaka ofisini kwake akiipongeza hotuba ya Waziri Mkuu Majaliwa aliyotoa wakati alipofungua kikao cha mawaziri wa Afya wa Jumuiya ya Maendeleo ya kiuchumi Kusini mwa Afrika (SADC).

Shaka alisema vikwazo hivyo vinaapaswa kuondosha kwa hiari kwa kujali haki na kuthamini ubinadanu lakini kipindi hiki wakati dunia ikikabiliwa na mazingira ya kijografia yenye joto kali na mtafaruku, vifo na majanga, vikwazo hivyo ni manyanyaso na dhulma kwa binadamu wasio na hatua.

Amefahamisha kuwa kama serikali ya CCM ilivyoshiriki harakati za kupigania haki na usawa mahali popote dunia ambako haki ,usawa na uhuru wa watu ulifungwa vitanzi, vikwazo vya kiuchumi dhidi zimbabwe pia havipaswi kuwepo.

'Hotuba ya Waziri Mkuu Majaliwa Kwa niaba ya Mhe Rais Magufuli ilikuwa ya kijasiri na kizalendo . CCM mkoa wa Morogoro tunaungana na Mwenyekti wa CCM Dkt Magufuli kwanza tuitaka dunia ijikinge na virusi vya Corona. Pia wito wetu dunia ikatae fedheha inayoipa mateso zimbwebwe dhidi ya vikwazo vya kiuchumi kwa nchi hiyo na kutatiza "Alisema Shaka.

Aidha Katibu huyo alisema vikwazo hivyo vikiendelea kubaki ni kama kuifunga upya Zimbabwe minyororo inayominya uhuru wake, kuinyima fursa muhimu huku vikwazo hivyo vikiwa ni adhabu na ukandamizaji wa haki unaoinyemelea nchi hiyo ya kusini mwa Afrika.

"Kuendelea kuwepo kwa vikwazo vya kiuchumi ni kuilundikia mzigo wa mateso Zimbabwe bila hatia .Kibinadamu haipaswi tena kuwashuhudia wazimbabwe wakiishi kwa mashaka huku nchi za sadc zikiitazama nchi hiyo na watu wake wakiteketea kiuchumi na maradhi" Alisema.

Shaka alisema Rais Emerson Mnangagwa wa Zimbabwe haikustahili arithishwe vikwazo hivyo badala yake ingekuwa uungwana akapewa nafasi na fursa ili atekeleze sera zake , kutoa ushirikianao kidiplomasia na kufanyakazi za kimahusiano na taasisi za kidunia.

"Ni vikwazo haramu vya kiuchumi vyenye maonevu na fedhuli. Wakati huu dunia ilipaswa kujali utu wa kila mmoja duniani .Ni wakati wa kupambana na virusi vya Corona na kuonyesha mshikamano. Vikwazo kwa zimbabwe havijengi ustawi wala havina maana yoyote " Alisisitiza Shaka.

Hata hivyo Katibu huyo alisema ni jambo la kufurahisha kumuona Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt Magufuli, akiendeleza msimamo wa kupigania haki na utu duniani huku ukizitaka nchi za sadc kusimama pamoja na kuzidisha ari ya mapambano na kupinga aina yoyote ya ukandamizaji haki.

#UhuruWaKiuchumi #OndoaVikwazoZimbabwe #TzTunasimamaNaZimbabwe #AfrikaTusimameNaZimbabwe
1585248849615626-0.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
tzkwanza

JF-Expert Member
Dec 27, 2018
1,389
2,000
Hapo Dodoma Bahi na Kondoa kuna watu wanalala njaa na watoto wanakaa chini mashuleni.

Aanzie hapo Dodoma kwanza kabla ya kusaidia Zimbabwe.

Kila mtu anajua ushenzi alioufanya Mugabe hadi nchi ikawekewa vikwazo, wazungu sio wapumbavu wakupewa amri na CCM eti ondoeni vikwazo.

Mugabe alinyang'anya mali kama mashamba na mitambo yakiwemo matrekta kutoka kwa wazungu, kabla ya yote Zimbabwe wanatakiwa walipe fidia ndio vikwazo viondolewe, no short-cut.
 
Elisha2004

JF-Expert Member
Feb 21, 2020
492
1,000
Ukitaka corona kupoteya Bongo just announce kuwa CCM ndio kareta Corona. Finished

"My pain may be the reason for somebody's laugh,but my laugh must never be the reason for somebody's pain"

Charlie Chaplin
 
Ukwaju

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
12,464
2,000
Mambo ya CCM mnayaleta humu jamani wakati watu mishahara haiatoka
,mnawasiaidia wazimbabwe wakati kwenu mafuriko, njaa, uchaguzi wa Serikali za mitaa bado hoi
 
ngusillo

JF-Expert Member
Nov 5, 2019
1,067
2,000
Nawashangaa hawa CCM eti wanawapigania Zimbabwe! Ni aibu sana kwa nchi inayoonekana wazi kudhulumu watu na kuua watu kisha kupora mali zao eti leo sisi tukaipiganie iondolewe vikwazo.

Nchi yenyewe bado inaendesha kampeni ya kutia wapinzani vilema kwa kuwatumia polisi kama mbwa wa kuwalinda wakae madarakani kinyume kabisa na matakwa ya wananchi.

Hata Tanzania siioni ikikwepa vikwazo vya kiuchumi muda si mrefu ujao. Mmewapora watu haki hata ya kuchagua balozi wa nyumba 10 na mjumbe wa mtaa kisha mnapata ujasiri wa kupanua midomo eti musiwekewe vikwazo?

Mtuache, msitutolee takataka zilizowajaa vichwani. Siku mkitaka kuwatetea wazimbabwe mkaombe uraia huko Zimbabwe kwanza kisha muhamie huko. Mtuachie nchi yetu.
 
Valuhwanoswela

JF-Expert Member
Jun 27, 2019
1,207
2,000
Mwenyekiti alionja joto la jiwe alipotukanwa na wananchi wa Zimbabwe alipojaribu kusifia viongozi wa nchi hiyo ikabidi akatishe hotuba yake na kukimbia kurudi huku. Sasa wanajaribu kujikosha uchafu wao mbele ya Wazimbabwe wenye hasira bado. Tukio lile lilikuwa funzo zuri kwa CCM kutosifu viongozi kwa kuwa viongozi bali kwa kustahili sifa.
 
Bishweko

JF-Expert Member
Sep 29, 2011
2,864
2,000
CCM ebu acheni kulialia..yaani mnataka tena mabeberu kushirikiana na nyie wakati wao hamna kitu?
 
JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
21,925
2,000
..sielewi kwanini CCM wanatetea UKATILI unaofanywa na vyombo vya dola vya Zimbabwe.

Los técnicos

JF-Expert Member
Sep 14, 2014
2,805
2,000
Mwenyekiti alionja joto la jiwe alipotukanwa na wananchi wa Zimbabwe alipojaribu kusifia viongozi wa nchi hiyo ikabidi akatishe hotuba yake na kukimbia kurudi huku. Sasa wanajaribu kujikosha uchafu wao mbele ya Wazimbabwe wenye hasira bado. Tukio lile lilikuwa funzo zuri kwa CCM kutosifu viongozi kwa kuwa viongozi bali kwa kustahili sifa.
Mbona sikuisikia hii?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mr Big

JF-Expert Member
Sep 16, 2019
479
1,000
..sielewi kwanini CCM wanatetea UKATILI unaofanywa na vyombo vya dola vya Zimbabwe.

Waliamdama hao kwenda mahakama kuu na bunge licha yakuwa mahakam ilipinga shaur lao,ni kawaida kwa jeshi la polisi kuzuia hali yoyote.
 
bulicheka 4

JF-Expert Member
Mar 22, 2020
916
1,000
Mugabe alinyang'anya mali kama mashamba na mitambo yakiwemo matrekta kutoka kwa wazungu, kabla ya yote Zimbabwe wanatakiwa walipe fidia ndio vikwazo viondolewe, no short-cut.
Huku Tz watu wananyanganywa mali kwa Plea bargain baada ya kuwekwa mahabusu kwa muda mrefu kuna ofauti gani na mbinu aliyo tumia Mugabe?
 
SAGAI GALGANO

JF-Expert Member
Nov 13, 2009
27,105
2,000
Na Mwandishi Wetu
Morogoro

Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Morogoro kimefurahishwa na msimamo idara uliotolewa na Waziir Mkuu Kassim Majaliwa kwa niaba ya serikali ya Rais Dkt John Magufuli , unaozitaka Nchi wanachama za SADC kusimama pamojao na Zimbabwe mpaka pale vikwazo dhalimu vya kiuchumi nchini humo zitakapoondolwa.

Kimesema wakati huu dunia nzima ikikumbwa na janga la kusambaa kwa virusi vya Corona huku huduma za kibinadamu zikihitajika kwa kiasi kikubwa haipendezi kuishuhudia zimbabwe ikiendelea kuwekewa vikwazo vya kiuchumi.

Matamshi hayo yametamkwa jana na Katibu wa CCM Mkoa Morogoro Shaka Hamdu Shaka ofisini kwake akiipongeza hotuba ya Waziri Mkuu Majaliwa aliyotoa wakati alipofungua kikao cha mawaziri wa Afya wa Jumuiya ya Maendeleo ya kiuchumi Kusini mwa Afrika (SADC).

Shaka alisema vikwazo hivyo vinaapaswa kuondosha kwa hiari kwa kujali haki na kuthamini ubinadanu lakini kipindi hiki wakati dunia ikikabiliwa na mazingira ya kijografia yenye joto kali na mtafaruku, vifo na majanga, vikwazo hivyo ni manyanyaso na dhulma kwa binadamu wasio na hatua.

Amefahamisha kuwa kama serikali ya CCM ilivyoshiriki harakati za kupigania haki na usawa mahali popote dunia ambako haki ,usawa na uhuru wa watu ulifungwa vitanzi, vikwazo vya kiuchumi dhidi zimbabwe pia havipaswi kuwepo.

'Hotuba ya Waziri Mkuu Majaliwa Kwa niaba ya Mhe Rais Magufuli ilikuwa ya kijasiri na kizalendo . CCM mkoa wa Morogoro tunaungana na Mwenyekti wa CCM Dkt Magufuli kwanza tuitaka dunia ijikinge na virusi vya Corona. Pia wito wetu dunia ikatae fedheha inayoipa mateso zimbwebwe dhidi ya vikwazo vya kiuchumi kwa nchi hiyo na kutatiza "Alisema Shaka.

Aidha Katibu huyo alisema vikwazo hivyo vikiendelea kubaki ni kama kuifunga upya Zimbabwe minyororo inayominya uhuru wake, kuinyima fursa muhimu huku vikwazo hivyo vikiwa ni adhabu na ukandamizaji wa haki unaoinyemelea nchi hiyo ya kusini mwa Afrika.

"Kuendelea kuwepo kwa vikwazo vya kiuchumi ni kuilundikia mzigo wa mateso Zimbabwe bila hatia .Kibinadamu haipaswi tena kuwashuhudia wazimbabwe wakiishi kwa mashaka huku nchi za sadc zikiitazama nchi hiyo na watu wake wakiteketea kiuchumi na maradhi" Alisema.

Shaka alisema Rais Emerson Mnangagwa wa Zimbabwe haikustahili arithishwe vikwazo hivyo badala yake ingekuwa uungwana akapewa nafasi na fursa ili atekeleze sera zake , kutoa ushirikianao kidiplomasia na kufanyakazi za kimahusiano na taasisi za kidunia.

"Ni vikwazo haramu vya kiuchumi vyenye maonevu na fedhuli. Wakati huu dunia ilipaswa kujali utu wa kila mmoja duniani .Ni wakati wa kupambana na virusi vya Corona na kuonyesha mshikamano. Vikwazo kwa zimbabwe havijengi ustawi wala havina maana yoyote " Alisisitiza Shaka.

Hata hivyo Katibu huyo alisema ni jambo la kufurahisha kumuona Mwenyekiti wa CCM Rais Dkt Magufuli, akiendeleza msimamo wa kupigania haki na utu duniani huku ukizitaka nchi za sadc kusimama pamoja na kuzidisha ari ya mapambano na kupinga aina yoyote ya ukandamizaji haki.

#UhuruWaKiuchumi #OndoaVikwazoZimbabwe #TzTunasimamaNaZimbabwe #AfrikaTusimameNaZimbabwe View attachment 1400246

Sent using Jamii Forums mobile app
Mtoto kwa kurembua tu hujambo. Mombasa hurudi tena?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tigershark

JF-Expert Member
Oct 9, 2018
7,093
2,000
Hili tunakomaa nalo maana Tz inaweza kuwa next kwenye vikwazo,sasa na sisi tutahitaji watu wa kutupambania tuondolewe vikwazo!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom