Shaka Hamdu Shaka: Rais Samia ni mbobezi kwenye uongozi

BWANKU M BWANKU

JF-Expert Member
Jan 12, 2019
328
414
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Itikadi na Uenezi Ndugu Shaka Hamdu Shaka amesema Chama hicho hakijawahi kumsimamisha Kiongozi wa nchi kwa majaribio.

Shaka Hamdu Shaka ameyasema hayo Jana Jumapili Agosti 15, 2021 katika ibada ya kuweka wakfu na harambee ya jengo la utawala na shule ya Biblia katika Kanisa la Pentacostal Moto Moto lililopo Boko, Kinondoni Jijini Dar es Salaam ambapo amesema Rais Samia ameudhihirishia umma ndani na nje kuwa anaielewa vyema nchi anayoingoza lakini pia ana washauri mahiri wenye weledi katika fani mbalimbali pamoja na kuweka mbele maslahi ya Taifa.

Shaka amesema Chama hicho kinaposimamisha Kiongozi kinajiridhisha juu ya uwezo, maarifa, uzoefu na uzalendo wake kwa nchi.

"Niwahakikishie Watanzania kupitia mkusanyiko huu kuwa Rais Samia ni Msomi mzuri katika maendeleo ya utawala na uchumi ambae ametumikia na kushika nyadhifa mbalimbali za Kiserikali (Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) pamoja na Mashirika ya Kitaifa na Kimataifa duniani, ni mtu bingwa kabisa na anatosha hivyo atatuvusha kama alivyoweza kutuvusha Taifa hili lilipopitia katika maumivu na nyakati ngumu katika historia yetu leo tumebaki kuwa wamoja." Alisema Shaka

"Hii ndio faida kubwa ya kuwa na Rais anaeijua nchi yake, anaejua anaowaongoza wanahitaji nini, kwa wakati upi na yeye asimame katika mrengo upi bila ya kuyumbishwa na mikingano ya ndani na nje. Rais Samia amekamilika kwa kila sifa ambayo dunia ya leo inauhitaji mkubwa wa Rais wa nchi wa aina yake. Niseme tena Tanzania Mwenyezi Mungu ametubariki" Alisema Shaka.

Pia Katibu huyo wa Itikadi na Uenezi amewahakikishia viongozi wa dini kuwa Serikali za CCM daima zitaendelea kuheshimu na kuthamini jitihada za waumini wa dini zote katika kusogeza Taifa kiimani na kimaendeleo hivyo viongozi wa dini wanategemewa sana katika kuendelea kuwaunganisha Watanzania.

Katika harambee hiyo Mhe Rais Samia Suluhu Hassan alichangia shillingi Millioni 10 kuunga mkono jitihada za kanisa hilo, Mwenezi Shaka na msafara wake wote wakachangia Millioni 5 na laki mbili ambapo jumla ya shillingi Millioni 24 zilichangwa na waumini wa kanisa hilo.

#KaziIendelee
 
Huyu kinda haijui CCM wala nchi hii Anafanya PR tu! wenye akili tunaelewa hamna kitu hapo! Amuulize Mtemi Anthony Dialo amsaidie! Mpaka wanakabidhi nchi kwa watu wenye vyeti vya Mirembe hospitali ya vichaa! Asitutanie huyu dogo.
 
CCM walishaona Mama Samia anatoa maboko ya kutosha ndo maana wanatumia nguvu kubwa kumtetea. Samia haijui Tanganyika, huo ndo ukweli halafu kichwani ni mtupu hana analojua na katuthibitishia huo utupu wa kichwani alipohojiwa na BBC maana kila mwenye masikio alisikia.
 
Hii si busara ya mjadala. Kwa nini hujadili hoja? Kwa sababu Shaka kaweka hoja kuhusu uzoefu na uwezo mkubwa wa Rais Samia kuongoza nchi. Mimi nakubaliana na Shaka tuna Rais mwenye vision kubwa ya uongozi tumpe muda.
 
Mbona shaka zulu natali unatumia nguvu kubwa kutuaminisha kuwa ni mbobezi?

Tusubiri muda utazungumza wenyewe
 
Naomba kuuliza,hivishaka ni katibu mwenezi wa CCM au ni msemaji wa Ikulu?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom