Shairi: Walipoipata mali

Mo makambako

Member
Dec 13, 2019
30
13
Walipo ipata mali, wakaingia mjini
Wakamtupa jalali, jembe na wake mpini
Wakaponda zote mali, na warembo limbukeni
Wakachana daftari, kupoteza taarifa

Walikula na kusaza, wakaota na vitambi
Meza wakatandaza, kwa peza za rambi rambi
Rambi rambi zake faza, aliewaeleza kwamba
Kama mnataka mali, mtaipata shambani

Wakaanza firisika, wakaipata aibu
Wakaanza ghafirika, na nyoyo kujaza gubu
Shambani wakaibuka, kuliuza kujaribu
Mzabuni akafika, nabei wakaratibu

Wakaondoa kibao, walichokiweka mwanzo,
Wakahama na makao, wakaukimbia mwanzo
Wakahamia mwambao, wakaondoe mawazo
Wakaifaidi Mali waloipata shambani

Wakaanza kuugua, magonjwa dhofu lihali
Wakashindwa kutanua, na sawa kuzikabili
Uchovu ukazidia, kifo kawa dalili
Wameshaichoma Mali, waloipata shambani

Ikawatoka kauli, toka mwao midomoni
Kama unataka mali, mtaipata shambani
Na kuitunza Mali, muhimu daftarini
Wakaifumba midomo, na macho hayakuona

Naiandka tanzia, msiba ulonigusa
Tanzia naikazia, kauli zimenigusa
Umenigusa wosia, machozi nayapangusa
Kama mnataka Mali, mtaipata shambani
 
Back
Top Bottom