Shairi:Tunda la ajabu

Shairi:Tunda la ajabu

Joined
Jan 24, 2015
Posts
29
Reaction score
20
TUNDA LA AJABU.

Nimetulia mtini, nala tunda liso kokwa.
Laini shinda maini, ladha kuku wa kupakwa.
Chumvi nitake ya nini, nala bivu si kidakwa.
Naulinda mti wangu, unatunda la ajabu.

Tunda sikukuta chini, liangani likadakwa.
Ladha yake ulimini, akili zangu zarukwa.
Ladha zazidi sabini, nala huku naropokwa.
Naulinda mti wangu, unatunda la ajabu.

Tunda halishi kinywani, wala ladha kupungukwa.
Nala leo na mwakani, tena bila ya kuokwa.
Tunda linafichwa ndani, haliwezi kuanikwa.
Naulinda mti wangu, unatunda la ajabu.

Sikumbuki ya zamani, fahamu zimeshashikwa.
Sizuruli mitaani, mtini nimepachikwa.
Usihoji hadi lini, jibu siwezi kuchokwa.
Naulinda mti wangu, unatunda la ajabu.

Side Sauti nyikani, sitaki tena kusakwa.
Acha nishinde mbugani, mti usije zungukwa.
Wengi wanautamani, nalinda nisije pokwa.
Naulinda mti wangu, unatunda la ajabu.


Sauti ya nyikani.
 
Tunda hukukuta chini, liangani ukalidaka!
Tunda tamu kama nini, midenda inakutoka!
Tunda lafichwa porini, kwenye nyasi na vichaka!!!
Tunda hili la ajabu!!!!!!
 
Andanenga malenga wetu.

Kwa kweli tunda ni tamu, kama umejitwalia,
Sukariye ni adimu, adhimu wengine hulia,
Si mithili kujikimu, pspf chungulia,
Tunda lina baraka, haulipati kondeni.
 
Tunda hukukuta chini, liangani ukalidaka!
Tunda tamu kama nini, midenda inakutoka!
Tunda lafichwa porini, kwenye nyasi na vichaka!!!
Tunda hili la ajabu!!!!!!

Zingatia vina na mizani tafadhali
 
Zingatia vina na mizani tafadhali

Ndugu yangu Jogi hata wewe kwenye ubeti wako katika mshororo (mstari) wa pili umeweka mizani 9 badala ya 8? pale ulipo andika "adhimu wengine hulia". Hakuna mkamilifu sote hughafirika kama alivyo kosea kwa bahati mbaya Mzee Raza.

Ila wote ni wazuri nipenda tungo zenu.
 
Andanenga malenga wetu.

Kwa kweli tunda ni tamu, kama umejitwalia,
Sukariye ni adimu, adhimu wengine hulia,
Si mithili kujikimu, pspf chungulia,
Tunda lina baraka, haulipati kondeni.


Tamu kushinda asali, kalibariki manani!!
Walipenda marijali, wengi huliweka ndani!
Kilimiliki kihalali,utaingia peponi!!
Oa ujifaidie!!!
 
Ndugu yangu Jogi hata wewe kwenye ubeti wako katika mshororo ( mataeri) wa pili umeweka mizani 9 badala ya 8? pale ulipo andika "adhimu wengine hulia". Hakuna mkamilifu sote hughafirika kama alivyo kosea kwa bahati mbaya Mzee Raza.

Ila wote ni wazuri nipenda tungo zenu.

Sijivunii kukosea, nasikitika lakini sitaacha kuhimiza ukamilifu.

NAPENDA MASHAIRI
 
Kwa mujibu wa wanafasihi mambo leo, shairi si lazima lizingatie urari wa vina na mizani mkuu,

Pia uzuri wake hili ni jukwaa la mahuaiano, mapenz nk. si jukwaa la lugha tunalenga kuburudisha na kufundisha yanayohusiana na jukwaa husika ili hata asie mshairi achangie.
 
Ndugu yangu Jogi hata wewe kwenye ubeti wako katika mshororo ( mataeri) wa pili umeweka mizani 9 badala ya 8? pale ulipo andika "adhimu wengine hulia". Hakuna mkamilifu sote hughafirika kama alivyo kosea kwa bahati mbaya Mzee Raza.

Ila wote ni wazuri nipenda tungo zenu.


Swadaktaa!!!!!! Kwenye huo mshororo mizani imezidi 8,ila wanafasihi mambo leo wanasema sio lazma kuzingatia urari wa vina na mizani cha muhimu zaidi ni kuhakikisha shairi linakuwa na muala!!!!
 
Sijivunii kukosea, nasikitika lakini sitaacha kuhimiza ukamilifu.

NAPENDA MASHAIRI


Hii ni fani adhimu, fani yetu manyakanga!!!
Tena ni fani adimu, ya maneno kuyapanga!!
Fani haiishi hamu, toka enzi za Andanenga!!!
Twende kazi mkuu!!!
 
1) Kutunga nlivokumisi,
mwishoni nitaugua,
Mtima wangu yabisi,
nawe ndio lake jua,
Ya moyoni warahisi,
walimwengu kuyajua,
Kutunga sitokudisi,
amani waniletea.

2) Wafanya kwa ufanisi,
jukumu walichukua,
Wawapita wahandisi,
mabonde kuyafukia,
Wafundisha kirahisi,
vipofu wawafungua,
Kutunga sitokudisi,
amani waniletea.

3) Usiku wa alhamisi,
kwa kazi mejichokea,
Bado kelele za bosi,
mambo yananilemea,
Kwa yote sitokuasi,
na moyo ukatulia,
Kutunga sitokudisi,
amani waniletea.

4) Kama mfupa na fisi,
mfano kichulia,
Muda wangu we filisi,
milele sitojutia,
Hatutengi ibilisi,
damu tulishangia,
Kutunga sitokudisi,
amani waniletea.
 
1) Kutunga nlivokumisi,
mwishoni nitaugua,
Mtima wangu yabisi,
nawe ndio lake jua,
Ya moyoni warahisi,
walimwengu kuyajua,
Kutunga sitokudisi,
amani waniletea.

2) Wafanya kwa ufanisi,
jukumu walichukua,
Wawapita wahandisi,
mabonde kuyafukia,
Wafundisha kirahisi,
vipofu wawafungua,
Kutunga sitokudisi,
amani waniletea.

3) Usiku wa alhamisi,
kwa kazi mejichokea,
Bado kelele za bosi,
mambo yananilemea,
Kwa yote sitokuasi,
na moyo ukatulia,
Kutunga sitokudisi,
amani waniletea.

4) Kama mfupa na fisi,
mfano kichulia,
Muda wangu we filisi,
milele sitojutia,
Hatutengi ibilisi,
damu tulishangia,
Kutunga sitokudisi,
amani waniletea.



safi sana mkuu,
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom