VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
HUKU NA KULE
Peni yangu Andanenga, uwino unapotona,
Mantiki huzilenga, na balagha na bayana,
Hufaidika malenga, huvurugika akina,
Nyege
ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.
Msemo wa Kiswahili, nyege ni kunyegezana,
Maana yaki kamili, "wema ni kutendeana',
Wasiojua fasili, hunamba nimetukana,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.
Ni msemo maarufu, ambao shaka hauna,
Kwenye kamusi sanifu, funueni mtaona,
Niwezeje kukashifu, nami mwana muungwana!
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.
Ninataja ukurasa, wazi hapa naunena,
Soma mbili moja tisa, soma bila ya fitina,
Msemo siyo wa sasa, si juzi licha wa jana,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.
Ushairi kubwa fani, mithili yake haina,
Kujua zake bayani, yataka kikubwa kina
Muoneni mwafulani, hata kuku wamguna,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.
Ulipotamkwa mlo, kaja akitunatuna,
Akakabwa koromelo, akabaki kugunaguna,
Kabakia lolololo, uzamani umechina,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.
Alhaji Jitukali, pokea pongezi tena,
Kikubwa chako kilili, hapandi yule mtwana,
Atuache tule wali, yeye ugali wa dona,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.
Kaditama wa Busara, na Mbwezi heko kijana,
Pongezi ndugu Kagera, Yobu has ante sana,
Ndimi Mshairi Bora, kipofu ninaeona,
Nyege ni kunyegezana, msemo wa Kiswahili.
(Mshairi Bora)
Amiri A. S. Andanenga (Sauti ya Kiza)
SLP 4775,
Kinondoni Shamba
Dar es salaam.
Hakuna matusi hapo Mkuu. Kiswahili kina utamu wake...Matusi, sitaki!
Ndio Mkuu.Huoni anwani na jina lake chini?Hili alilitoa mzee Andanenga mwenyewe?
Hakuna matusi hapo Mkuu. Kiswahili kina utamu wake...
Kuna maneno/matendo katika mila na desturi za watu duniani hayasemwi/hayafanywi hadharani .Mfano, huwezi kusimama mbele za watu ukajikuna sehemu za siri. Watu watakushangaa. Si unajua Nyege ni neno la ngono, na ngono ni taboo in african customs. Au wamasemaje Mkuu?
Hakuna matusi hapo Mkuu. Kiswahili kina utamu wake...
Andanenga amenena lililo mwake moyoni
mwasema ametukana kwenu lipi lilo geni
nani hapa alo mwana mnalaumu kwanini
kiswahili lugha pana utamu wake lahajani
Tusi katukana nani alosema lipi baya
kipi ni tusi jamani tukisute bila haya
nijuze nipate amani kipi kimeleta haya
kiswahili lugha pana utamu wake lahajani
naamini ungetumia kiswahili ungeeleweka vizuri zaidi!ni katika kuitetea tu lugha hii tamu!It looks good as wewe sio mwandishi try to make it more serious, big up "YES YOU CAN"
naamini ungetumia kiswahili ungeeleweka vizuri zaidi!ni katika kuitetea tu lugha hii tamu!
Samahani kwa kukwazika, binafsi nakipenda sana kiswahili kwani kiingereza nimeanza kusoma kidato cha kwanza.....Nashukuru kwa kunikumbusha
Matusi, sitaki!
Ndio Mkuu.Huoni anwani na jina lake chini?