Tanzania Nchi Yetu Sote
JF-Expert Member
- Mar 12, 2017
- 505
- 871
NAMBA HII NAMBA GANI
NI NGUMU HAISOMEKI.
Namba hii sio tasa
Wala Ile ya Witiri
Wasomi Inawatesa
Waisoma Siri Siri.
Namba Isiyo someka
Si kichina si kirumi
Wengine inatutesa
Namba isiyo sufuri.
Walitumia mzaha
Kuandika ubaoni
Wakaiona furaha
Kuiimba jukwaani
Namba hii namba gani
Namba isiyo someka
Hata katika kamusi
Vigumu kuelezeka.
Namba haiongezeki
Kupunguza kadhalika
Wala haiuliziki
Mwalimu Akasirika.
Namba Ina maajabu
Haiongezi sufuri
Kuipata sasa tabu
Jasho hujaa mwilini.
Namba hii namba gani
Tumechoka kuisoma
Sasa haina thamani
Ina tunyima uzima.
Wapo waloo taabani
Wengine nao vilema
Namba haionekani
Kuisoma nilazima.
Wengine twefurahia
Kuingia darasani
Mwalimu akatwambia
Namba hii isomeni
Tukaimba kwa vifijo
Namba asome Fulani
Kumbe lilikua fumbo
Namba Haikosekani.
Namba hii namba gani
Inoleta tafrani
Wasomi Wakila fani
Namba hawaoni ndani.
NAMBA HII NAMBA GANI
NAOMBA JIBU NIPENI.
NI NGUMU HAISOMEKI.
Namba hii sio tasa
Wala Ile ya Witiri
Wasomi Inawatesa
Waisoma Siri Siri.
Namba Isiyo someka
Si kichina si kirumi
Wengine inatutesa
Namba isiyo sufuri.
Walitumia mzaha
Kuandika ubaoni
Wakaiona furaha
Kuiimba jukwaani
Namba hii namba gani
Namba isiyo someka
Hata katika kamusi
Vigumu kuelezeka.
Namba haiongezeki
Kupunguza kadhalika
Wala haiuliziki
Mwalimu Akasirika.
Namba Ina maajabu
Haiongezi sufuri
Kuipata sasa tabu
Jasho hujaa mwilini.
Namba hii namba gani
Tumechoka kuisoma
Sasa haina thamani
Ina tunyima uzima.
Wapo waloo taabani
Wengine nao vilema
Namba haionekani
Kuisoma nilazima.
Wengine twefurahia
Kuingia darasani
Mwalimu akatwambia
Namba hii isomeni
Tukaimba kwa vifijo
Namba asome Fulani
Kumbe lilikua fumbo
Namba Haikosekani.
Namba hii namba gani
Inoleta tafrani
Wasomi Wakila fani
Namba hawaoni ndani.
NAMBA HII NAMBA GANI
NAOMBA JIBU NIPENI.