Shairi; Mwanzo wa Ngoma

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,207
4,405
MWANZO WA NGOMA

1)Kweli hii ngoma ngumu,kuipiga na kucheza.
Kama unakunywa sumu,chunga watakulegeza.
Ipige hadi idumu,ukiacha watubeza.
Huu ndo mwanzo wa ngoma,ama kiki watafuta ?

2)wengi wazungu wa unga,siyo mchezo mchezo.
Wamevishika viunga,fulusi nyingi wanazo.
Vijana wanojidunga,wamekua hamnazo.

3)Ngoma sasa inadunda,usiache kuicheza
Ya kwamba unavurunda,wapo wataoeleza.
Hivi roho ya kudunda,ama chale la kucheza ?.
Huu ndo mwanzo wa ngoma,ama kiki watafuta.

4)kabla ya kucheza ngoma,kwanza agana na nyonga.
Tena imara simama,hawachelewi kunyonga.
Ngoma iishe salama,hawa jamaa vinyonga.

5)kiki nyingine mikuki,chunga usitoke nduki.
Wanakesha na bunduki,huku wakifuga nyuki.
Huko kuna mamluki,kusaliti hawachoki.
Huu ndo mwanzo wa ngoma,ama kiki watafuta ?.

6)Utamu wa ngoma ni mwisho,mwanzo tuna haja nao
Ama hili furahisho,asikwache baba lao.
Fanya ijewa fundisho,ukija washinda wao.

7)kesha wafanya maombi,dua usiache sala.
Hawa jamaa mazombi,wanang'ata kama ngala.
Umeshapiga filimbi,basi yashinde madhila.
Huu ndo mwanzo wa ngoma,piga hadi ipasuke.

Shairi:MWANZO WA NGOMA.
Mtunzi: Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
 
Back
Top Bottom